Mjina Mrefu
JF-Expert Member
- Dec 6, 2016
- 3,037
- 3,369
Salaam wakuu,
Erolink ni kampuni inayofanya kazi kama recruitment agent hapa nchini. Erolink imepewa mandate katika kampuni mbalimbali hapa nchini hususani katika call centers.
Erolink ndiyo inayoiongoza Call center ya Vodacom Tanzania na kimsingi, call center agents wote wa vodacom wapo chini ya Erolink.
Ktk kabandiko haka, nitaizungumzia erolink iliyoko vodacom call center ambapo undercover research yangu ilipofanyika.
Pamoja na kuwa Erolink imetoa ajira kwa vijana wengi nchini but inawanyanyasa na kwenda kinyume na mkataba iliyoingia na wafanyakazi wake.
Erolink ni kampuni ambayo haiamini katika kukosea na kwamba, mfanyakazi anapotenda kosa dogo sana mfano kuchelewa hata dk 10 huchukuliwa disciplinary measures ikiwa ni kusainishwa warning.
Katika mkataba wa call center agents, muda wa kufanya kazi ni masaa 9, lakini, mfanyakazi analazimishwa kuwahi kazini dk 15 kabla ktk kikao kiitwacho huddle na asipokuja huddle regularly but hajachelewa kazini kulingana n ratiba yake, basi hupata warning au kuandika maelezo.
Pia wafanyakazi wanalazimishwa kufanya kazi nje ya muda wao wa kazi kwa mikwara na wasipofanya hivyo, warning au kutoa maelezo kunamhusu. Mfano mtu anakua ameshafanya kazi masaa tisa kwa mujibu wa mkataba but anaambiwa baada ya kumaliza kazi kuna shughuli nyingine za kikazi kama vikao/training nk anazotakiwa kuzifanya kabla ya kuondoka nyumbani. Kwaiyo unakuta mfanyakazi anafanya overtime ya kufosiwa ya lisaa bila malipo. Hii ni kinyume na sheria kukiuka makubaliano ya mkataba ya kufanya kazi masaa 9.
Mkataba wa call center agent unasema kuwa, ktk shift za jioni, break ni dk 50,but utakuta mfanyakazi ameingia saa 17:00, anapewa break ya dk 10 tu hadi saa tano hivi atakaporuhusiwa kuondoka. Kwaiyo mtu anaweza kufanya kazi masaa sita kwa break ya dk 10 tu.
Pamoja na kazi kuwa ngumu, Erolink haijali haki za wafanyakazi kufanya mambo yao binafsi wakati wakiwa off. Mfanyakazi anaweza kuwa off, ghafla anapigiwa simu aende kazini bila kujali mfanyakazi huyo yupo maeneo gani. Na asipoenda, basi anasainishwa serious warning.
Katika suala la mapumziko, sina uhakika sheria za kazi nchini zinasemaje but mfanyakazi wa erolink anaweza kupumzika siku nne tu kwa mwezi.
Inasemekana kwamba, Vodacom inatoa shilingi 800,000 kwa kila call center agent but huwezi kuamini wafanyakazi wa call center vodacom wanalipwa basic salary ya 400,000 na erolink. Apo kuna makato ya bima ya afya, mafao, pamoja na Paye. Kwaiyo mfanyakazi wa call center anachukua mshahara wa km 320000 hivi take home. Huu ni mshahara mdogo sana kulinganisha na nature ya kazi ambapo kuna shift hadi za usiku.
Ukipiga simu call center vodacom ukaona umejibiwa vibaya na mhudumu, usimlaumu,, ni kazi ngumu na visheria vya ajabu ajabu vya kumkandamiza na mshahara sisimizi.
Kimsingi erolink iache kunyanyasa watanzania. Isitumie kigezo cha ukosefu wa ajira kunyanyasa vijana wetu.
Mamlaka husika ziichukulie hatua hii kampuni kwa kuvunja masharti ya mkataba kwa wafanyakazi.
With due respect..