Eric shigongo ni mnafiki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eric shigongo ni mnafiki?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchakachuaji1, Nov 29, 2010.

 1. m

  mchakachuaji1 Senior Member

  #1
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Napenda kuingia jukwaani leo kwa kuleta hii mada ya huyu ndugu yetu Eric Shigongo. Nilikuwa nikimheshimu na kumkubali sana huyu jamaa kwa kuamini kuwa ni mwanaharakati, mwadilifu, msemakweli na mtetezi wa haki za wanyonge. Lakini kwa bahati mbaya heshima yangu kwake ilianza kushuka tangu kuanza kwa mchakato wa kura za maoni katika mchakato wa kuchagua wagombea ubunge kwa tiketi ya chama cha mapinduzi katika uchaguzi mkuu uliomalizika mwezi uliopita.
  Kwa muda mrefu nilikuwa nikisoma makala la Shigongo hasa ile ya Napasua jipu ya gazeti la uwazi. Nilikuwa naguswa sana na upeo na maono yake na uchungu wake juu ya maisha duni na ukandamizwaji wa raia masikini wa Tanzania.
  Shigongo amewahi kukemea maovu mengi yaliyofanya na serikali ya CCM kuanzia katika mikataba mibovu ya uchimbaji wa madini na sheria katili na kandamizi ya vyombo vya habari, pia aliwahi kupiga kelele kubwa sana kumtetea msanii Joseph Mbilinyi ambaye sasa ni mbunge wa jimbo la Mbeya mjini kwa tiketi ya CHADEMA pale ilipoelezwa kwamba Ruge Mutahaba kwa kumtumia January Makamba ambaye alikuwa msaidizi wa rais kutumia nguvu ya dola kumnyang'anya Mbilinyi mkataba wake wa kusimamia mradi wa malaria haikubaliki ambao alitumia muda na rasilimali nyingine kuhakikisha anafanikiwa kuuleta hapa nchini.
  Cha kushangaza ni kwamba Shigongo huyu huyu ambaye kwa mtazamo wangu alikuwa akiiona CCM kama kichaka cha madhalimu na wanyonyaji akaibuka na kuomba tiketi ya chama hicho hicho kugombea kiti cha ubunge katika jimbo la Buchosa lakini akaenguliwa na CCM kumsimamisha DR. Tizeba huku yeye akiishia kumpigia kampeni kwa shingo upande kupitia magazeti yake ya umbeya.
  Swali langu ni hili, huyu Shigongo wakati anaenda kuchukua fomu kuomba ubunge kwa tiketi ya CCM alisahau kwamba maovu aliyokuwa akikemea yalikuwa yakifanya na serikali ya chama hicho? Au alidhani kwamba yeye anaweza kuingia na kubadili mtizamo wa wana CCM wengine? Au aliamua kuchukua hatua hiyo katika kujipendekeza kwa CCM ili kulinda biashara zake?
  Nashukuru sana CCM walimtoa ili apate kujifunza kuwa na msimamo.
  KWA UKENGEUFU HUU ALIOUONYESHA JE HUYU SHIGONGO NI MNAFIKI?

  NAWASILISHA.
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Nov 29, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Wote wanaganga NJAA - "..Usiogope ukubwa wa samaki, ulizia Bei..."
   
 3. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mh ngoja nisikilize maoni kwani hapa nilipo ni NO COMENT.
  naufatilia mchakato nijue nn cha kuchangia MCHAKACHUAJI1
   
 4. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ni mnafiki wa hatari usimsogelee....
   
 5. Tusker Bariiiidi

  Tusker Bariiiidi JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2010
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 4,757
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Sasa hivi ameanzisha ka-mradi kakuuza DVD zenye risala za kuwainua wananchi kiuchumi kwa bei ya Shs.5000/- sijui kama katasaidia wananchi...

  Rais wa NEC akimuonea huruma atamgea Ukuu wa wilaya Kishapu.
   
 6. Mathias Byabato

  Mathias Byabato Verified User

  #6
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 908
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Hakuna bishara inayolipa Tanzania kama SIASA(Uongo)
  Shigongo ni mfanyabishara na mwanasiasa

  hapo umepata jibu
   
 7. Kahema

  Kahema JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2010
  Joined: May 21, 2010
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  aibu yake, alizani sisiem mchezo, si tulijua mnafiki toka time ago, thus y mi nilifurahi alivyopigwa chini mapeeema.
   
 8. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #8
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  biashara zake zinaendelea kudumaza akili za wananchi akili! uwazi, ijumaa, ijumaa wikienda, nk
   
 9. m

  mpingomkavu Member

  #9
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mnafiki mkubwa
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Nov 29, 2010
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Shigongo sio mnafiki hata kidogo. Sisiem inahitaji watu safi kama yeye. Naamini kama angepita angeweza kufanya mambo mengi mazuri. Msikichukie chama, chukieni watendaji wake. Hakuna namna ya kukibadilisha sisiem zaidi ya kuchagua watu ambao ni wapiganaji wa kweli. Mtoa mada acha kupandikiza mbegu za chuki zidi ya erick.
   
 11. Absolute

  Absolute JF-Expert Member

  #11
  Nov 29, 2010
  Joined: Jan 19, 2007
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo nimeipenda zaidi :)
   
 12. m

  matawi JF-Expert Member

  #12
  Nov 29, 2010
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Zipo namna kibao za kui change ccm ikiwepo kukizaba vibao kupitia chadema. Kuwa nasi 2015 tukiadhibu
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Nov 29, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,590
  Likes Received: 18,573
  Trophy Points: 280
  mchakachuaji1, Erick siyo mnafiki bali mkombozi wa vijana toka katika utumwa wa fikra.

  CCM ni chama, ni taasisi na sio mtu, watu ndio wanachama wa CCM ambao baadhi yao ni wanachama wa kawaida na baadhi yao ni viongozi wao. Kati ya wanachama hao wa kawaida, wako wanachama wa CCM ambao ni wasafi kbisa na hawana mawaa, na wako wanachama wa CCM wachafu, wala rushwa na mafisadi vile vile na vivyo hivyo ndivyo walivyo na viongozi wa CCM kuna viongozi safi, na viongozi wachafu, hivyo huwezi kukiita CCM ni chama kichafu kwa ajili ya uchafu wa viongozi wake. Hivyo tukubali bila emotuions za feelings kuwa CCM ni chama cha siasa kama kilivyo Chadema, CUF, TLP etc.

  Erick kama Mtanzania, anao uhuru wa kujiunga na chama chochote ambacho anaona kinamaslahi ya kumuwezesha kutimiza ndoto yake na ndio maana akachagua CCM.

  Kwa maoni yangu binafsi, kama Erick angegombea kwa tiketi ya Chadema, saa hizi angekuwa ni mbunge siku nyingi, lakin i yeye kwa mapenzi yake na utashi wake tena pia kutumia magazeti pendwa yake (tusiyaite ya udaku), aliamua kusimama na CCM mpaka mwisho na huo pia ni ushujaa na tutashuhudia 2015 akijaribu tena kusimama nayo, na that time ataanguka nayo kabisa na kupotea nayo, maana wananchi wameamka.

  Sina tatizo na upenzi wake, na uanachama wake na ushabiki wake kwa Chama cha Mapinduzi, bali natatizwa na matumizi ya magazeti yake kuegemea upande mmoja hivyo kuwapoteza kabisa wale wasomaji wengine ambao sio mashabiki wa CCM. Nyumbabni kwangu magazeti hayo hununuliwa na Dereva ambaye humletea HG home, kwa vile huwa nakutana yako, from time to time husoma japo headlines tuu, lakini baada ya kujiingiza kwenye siasa, magazeti hayo kwangyu yamegeuka ukoma, japo bado nalinunua na kulisoma gazeti la uhuru, kwa sababu limejitabaisha na CCM.

  Erick kama Erick is good, ana kipaji, ana owezo wa kujieleza na ana convincing powers to make things happen hivyo ni source of inspiration kwa vijana wake, na alipochanganya na siasa za chama tawala, hiyo inspiration yake sasa imejichakachua na inspiration for the better of CCM which is wrong!.
   
 14. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #14
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Taarifa ni kwamba alizidiwa rushwa na Dr Tizeba. Ukweli ni kwamba alitumia pesa nyingi sana ikiwa na kuwatumia wasanii wa bongo fleva pamoja na kina Kanumba. Labda kama atajibu yeye mwenyewe hili swali itafaa zaidi
   
 15. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #15
  Nov 29, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Kama mwanzoni ulimwona anafaa hiyo ni shauri yako. Mtu anayelea familia yake kwa kuuza umbea na udaku sina muda nae. Sikumbuki kama nimewahi kuipongeza ccm, lakini kwa kumwondoa shigongo kwenye kura za maoni napenda nichukue nafasi hii adhimu kukipongeza chama cha mapinduzi.
   
 16. T

  Think Tank JF-Expert Member

  #16
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 234
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kuhusu unafiki no coments.Ila viashiria vya utapeli anavyo!Huyu jamaa alianzishaga kiproject kinaitwa Jikomboe Clubs yaani kikundi cha vjana 50 mara vkundi 90 jumla 4500,kikiwa na lengo la kuibua mabilionea 1000 kwa maelezo yake!Lakini hata ukimwuliza kawawaibua wangapi?Hata 10 sijui kama kawaibua?Leo hii kaja tena na DVD sijui Street College sijui Street University kwa ajili ya wajasiriamali.Jamaa ni mbunifu lakini tatizo ana papara hatulii na mradi mmoja.
   
 17. Deodat

  Deodat JF-Expert Member

  #17
  Nov 29, 2010
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 1,279
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Hii imekaa vizuri Pasco, ume-balance vizuri stori bila kuficha ukweli. I agree with you, if Shigongo were smart enough, he would fly with CHADEMA in this election, no doubt, today we would be calling him "Mheshimiwa". But not every can see with the same specs as you do Pasco, thats needs analytical mind + some game theoretical skills!
   
 18. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #18
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wale waleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 19. m

  mchakachuaji1 Senior Member

  #19
  Nov 29, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 122
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ndugu yangu simchukii Shigongo wala sitaki watu wamchukie ila nahitaji kujua kwa nini anajing'ata mkia kwa kumeza matapishi ilihali anafahamu kansa ya uongozi iliyo ndani ya CCM. Kwa nini asingeingia upande mwingine wenye haki kama kweli alihitaji kuwatumikia watanzania kwa dhati kama alivyofanya Joseph Mbilinyi.
   
 20. wakusoma

  wakusoma JF-Expert Member

  #20
  Nov 29, 2010
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 949
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 180
  msanii tu huyu,halafu anajifanyaga mlokole ila ana matusi kweli,anatukana wfanyakaiz wake matusi ya nguoni kabisaaa
   
Loading...