Epuka tabia hii inayoweza kuzua ugomvi mkubwa kwenye ndoa za watu

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,255
2,000
Wana MMU nawasalimu.

Kuna watu wana tabia hii ambayo ni hatari sana kwa ndoa za
marafiki wao.

Tabia hii inachochewa na kusababishwa na:
1. Kufananisha watu
2. Kujifanya wewe ni mwanahabari mzuri
Tuanze.

Kufananisha watu: Uko kwenye shughuli zako unakatiza mitaa. Kwa mbaali kwenye kona fulani unamwona jirani yako Huseni ameongozana na mwanamke. Sura ya huyo mwanamke hujaiona vizuri ila kwa mawazo yako ya haraka unafikiri ni mkewe Huseni.

Siku mbili tatu baada ya tukio hili unamtembelea Huseni.

Ile unafika huko, unamkuta Huseni na mkewe wapo wakitezama tv,
Baada ya kusalimiana unaanza na Huseni: "Vipi bwana, nilikuona ukiwa na shemeji pale kwenye kona ya mtaa wa xyz mkiwa kwenye mishe.

Mke wa Husein anakukazia macho kwa mshangao kisha anamtazama mumewe kwa hasira.

Ni kweli mwanaume uliyemwona siku ile alikuwa Huseni lakini hakuwa ameongozana na mkewe.

Kwa maneno yako hayo tayari umewapandia mbegu ya ugomvi mkubwa. (Huseni alikuwa kwenye mchepuko!)

Kujifanya mwanahabari mzuri. Bw Huseni ni rafiki yako mkubwa.

Mnaelezana mipango yenu ya maisha
na mambo meengi tu mnaelezana. Siku moja Huseni akakutolea ya moyoni mwake kwamba amechoka na kazi anayofanya, anataka aache ahamie mji mwingine.

Ukiwa kwenye pitapita zako ghafla unakutana na mkewe Huseni.

Unaanza kazi yako ya kupasha habari. "Huseni kaniambia anataka kuacha kazi kisha ahame mji.Mtahamia wapi shem?"
Tayari hapo umeshazua ugomvi kwenye nyumba ya Huseni.

Tabia za aina hii wengi huita umbea. Usiwe mmbea wa aina hii tafadhali, utabomoa nyumba za watu!
 

Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,140
2,000
Huyo atakuwa hana kaba ya ulimi,ila hapo namba mbili sijaelewa unakuwaje karibu na mke/mume wa rafiki yako kiasi cha kukutana barabarani ukaanza kuhoji mambo yao ya kifamilia?
 

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,255
2,000
Huyo atakuwa hana kaba ya ulimi,ila hapo namba mbili sijaelewa unakuwaje karibu na mke/mume wa rafiki yako kiasi cha kukutana barabarani ukaanza kuhoji mambo yao ya kifamilia?
Hiyo ya pili @Enie ni pale mtu anapojifanya anajua kitu ambacho wewe hujui, kwa hiyo anakusaidia kukupasha.Ndivyo alivofanya huyo aliekutana na mke wa Huseni.
 

Ennie

JF-Expert Member
Jan 15, 2011
7,140
2,000
Hiyo ya pili @Enie ni pale mtu anapojifanya anajua kitu ambacho wewe hujui, kwa hiyo anakusaidia kukupasha.Ndivyo alivofanya huyo aliekutana na mke wa Huseni.

Huyo dawa yake kujifanya unajua habari yote hata kama ndio unasikia kwa mara ya kwanza!!
 

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,255
2,000
Kama mimi ndo Husein..... aiseee baada ya hapo utanikoma
Aaah wapi Price. Atakuambia hivi: Samahani bro.Mi navokufahamu nilijua kabisa uko na mke wako.Kwani ulikuwa
na nani siku ile?
 
Last edited by a moderator:

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,255
2,000
Huyo dawa yake kujifanya unajua habari yote hata kama ndio unasikia kwa mara ya kwanza!!
Ennie, wapo wanawake wenye hekima wanaoweza kufanya hivo, ila baadhi wanafyatukia hapohapo anapoelezwa.
 
Last edited by a moderator:

everlenk

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
11,604
2,000
Ni kweli kabisa, pengine mtu uliyeongozana naye anaweza kuwa hata si mchepuko labda ni co-worker lakini ukashangaa mtu anampigia simu mke/ mume wako kwamba amekuona.
 

Mazindu Msambule

JF-Expert Member
Feb 22, 2012
6,198
2,000
Tuliwahi kwenda safari ya kikazi mji fulani, tulikua mtu kama 7 hivi toka kwenye kampuni yetu, mwanamke 1 (yupo single) huko kwenye huo mji, tukakutana na wenzetu wengine toka makampuni mengine (of course it was planned so) nao wakaja na mwanamke 1 (sina hakika kama kaolewa au la). Well tukaanza kupanga nini cha kufanya siku ya pili, hiyo ilikua siku ya Jumapili (ilibidi tufikie hotel 1 pia) nao kwenye hiyo repoti yetu ambayo ilikua tui-submit next day, kuna vitu ambavyo ilitakiwa tukae ki-vikundi cause tuliweka vya kisheria, kimazingira (environmental) n.k, ilibidi kila kikundi kikae according to their profesional, nikapewa mdada yule tuliyekuja nae na yupo single, ilikuepukana na wasema hovyo, nikachukua kamera na kumpa mwenzangu 1 awe anatupiga picha wakati tunafanya hiyo write up cause nihisi mkaanga sumu 1 anaweza kuleta hi story home kwa my wife halafu liwe kasheshe (nilihisi wife anaweza kuambiwa hivi, mm mmeo alikua karibu sana na mtu fulani na jinsia tofauti) so nilipofika home, nikafungua laptop yangu na kuanza kumwonesha wife picha za safari including hiyo. Kwahiyo hata kama mtu angekuja kumweleza shemeji/wifi yenu juu ya ukaribu wetu at least ingekua ime neutralize hiyo kitu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom