Epuka smart phone, smart TV na smart girls ili utajilike haraka

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,295
21,438
Nashauri wizara ya elimu idara ya elimu ya juu iweke somo la matumizi ya mitandao na simu, watu wajuwe faida na hasara, watu wafundishwe ni namna gani mtu alichonacho kimsaidie kimaisha punde anapomaliza chuo.

Changamoto kubwa itakayolikumba taifa hili; ni rundo la vijana Tegemezi, Sasa kuwa na Smart phone ni kawaida Kwa kila mhitimu wa chuo kikuu, na huenda ndio ID ya kuonekana msomi, ingawa kuna faida nyingi sana za kuwa na simu lakini vijana wamekuwa busy na selfie, umbeya, udaku na siasa, mda woooote kazi ni kuchati tu wala hawawazi ni namna gani wajikomboe, wapo radhi washinde njaa ila simu isikose bando! Asilimia 90% ni anasa na umbeya halafu 10% ndiyo mtu anauliza uliza ajira na mambo ya msingi, Sikatai matumizi ya simu bali ni Kwa asilimia ngapi unaitumia hiyo simu Kwa faida lipi!

Kuna mtu leo anashida na mtaji wa laki moja tu ili atoke kimaisha,Mfano; mama ntilie, kuuza mayai, matunda, nyanya, mikate n.k ... ila utashangaa mtu hana ajira ila ana I phone ya 1.5mil huu ni ujinga, hata kama umenunuliwa uza uwe na simu ya tochi nyingine tumia kama mtaji.

Sasa hivi kuna watu ili ukae nao muoongee inabidi umsubiri hadi simu yake inapokuwa imeisha chaji ndiyo atakusikiliza.

Ushauri;
Jitahidi kuachana na ulevi Wa matumizi makubwa ya simu, geuza mda huo kuwaza mambo mengine, tembelea ofisini Kwa ndugu na jamaa zako, uliza kama waweza wasaidia kazi zao hata kama ni bure Fanya! Tembeleeni matamasha na semina za vijana mbalimbali.

EPUKA ULEVI WA SMART ......
SMART TV, SMART PHONE, SMART GIRL/BOYFRIEND......
KAMA WEWE NI MASKINI USIIPE NAFASI, KAMA UNA TV UZA ILI USISHINDE NDANI UKIBADILI CD.Kama una girl/boy anapenda show kila siku mjifungie ndani Mwache! Mwisho mtatiana mimba tu bila hela

Note: Mguu uliotoka ndiyo unaobalikiwa na Mungu"
Bibilia inasema; Ombeni, Tafuteni na bisheni hodi nanyi mtafunguliwa" lakini fahamu kwamba Maombi ni Mungu, lakini kutafta ni juhudi zako mwenyewe!
 
Ulikuwa na lengo zuri lakini umeshindwa kuzipangilia hoja zako na zikawafikia walengwa vizur.

Unaposema mtu anahitaji laki 1 kama mtaji ili atoke kimaisha ni vema ukaiweka iyo biashara ya laki 1 ni ipi.

Nani kakwambia ukiwa na tv ndio utashinda tu ndani kubadirisha cd tu? Ni wapi wanagawa cd za bure? Jibu ni lazima ukanunue na ili ununue ni lazima uchakalike.(kosa lako la pili)

Girl/boy kupenda show ni hulka ya mtu mimba ni mipango iliyopo au isiyokuwepo hela ni majaaliwa yake mungu.kwa usawa huu wa hapa kodi tu mtu kubadirika haiitaji semina.
 
Mbona wewe unamiliki smartphone? Umetumia simu ya tochi kupost huku?
mimi siyo masikini mkuu; nina kampuni nimeajiri watu 15 na natumia smart phone Kwa lengo maalumu tu na inapobidi. Lakini mwisho Wa yote chukua maneno yangu tu usiagalie nachokifanya Mimi naweza lala siku nzima na hela ikaingia THOUGH naumiza kichwa ili niongeze kipato zaidi thus am soo Busy.
 
Kwa mfano yeye katumia cmu ya aina gani kuandika huu ujumbe wake...kuongea kaongea vizuri hila ajatupa biashara ya kufanya kwahiyo laki moja kwasasa.
 
sijui neno ''SMART GIRL/BOYFRIEND.'' umetaka kumaanisha nini.....lakini kama ni literal :D sishauri kumuepuka....
All in all uzi wako ni mzuri
 
Ulikuwa na lengo zuri lakini umeshindwa kuzipangilia hoja zako na zikawafikia walengwa vizur.

Unaposema ukweli mtu anahitaji laki 1 kama mtaji ili atoke kimaisha ni vema ukaiweka iyo biashara ya laki 1 ni ipi.

Nani kakwambia ukiwa na tv ndio utashinda tu ndani kubadirisha cd tu? Ni wapi wanagawa cd za bure? Jibu ni lazima ukanunue na ili ununue ni lazima uchakalike.(kosa lako la pili)

Girl/boy kupenda show ni hulka ya mtu mimba ni mipango iliyopo au isiyokuwepo hela ni majaaliwa yake mungu.kwa usawa huu wa hapa kodi tu mtu kubadirika haiitaji semina.
Kusema ukweli akili kama hizi ndiyo tofuti ya tajili na masikini inapothibitika. Huenda utajili ungefichwa sumbawanga watu wangepanda basi kuufata, ungefichwa Paris watu wangeufuata lakini Ulifichwa kwenye ubongo Wa kila mtu, ndio maana hata ikitokea twende mji Mpya tukiwa watupu, baada ya mwezi tu tajili atajulikana.
 
Aja kataza kutumia simu ila matumizi yaliyo zidi kiwango tena kwa kukesha ukisikiliza umbea ,siasa n.k visivyo na tija kwa maendeleo yako binafsi uondo ulevi anao uzungumzia
 
sijui neno ''SMART GIRL/BOYFRIEND.'' umetaka kumaanisha nini.....lakini kama ni literal :D sishauri kumuepuka....
All in all uzi wako ni mzuri

Ha ha ha, eti SMART GIRLFRIEND umwepuke!

BTW, smartphones zimepunguza ufanisi wa kazi maofisini, watu hawasomi vitabu kama zamani, wanafunzi/vyuo wanatumia muda mwingi kwenye simu zaidi ya muda wa prep, zimepunguza ukaribu kati ya wapenzi na marafiki (unakuta muda mwingi mtu badala ya kuongea na kujadili uko JF/insta, FB etc).

Ni janga kwa wastani.
 
Ni sawa na wale wanaohamasisha kujikita kwenye kilimo cha kibiashara kana kwamba ardhi yote ina rutuba na hali ya hewa inafanana.
 
mimi siyo masikini mkuu; nina kampuni nimeajiri watu 15 na natumia smart phone Kwa lengo maalumu tu na inapobidi. Lakini mwisho Wa yote chukua maneno yangu tu usiagalie nachokifanya Mimi naweza lala siku nzima na hela ikaingia THOUGH naumiza kichwa ili niongeze kipato zaidi thus am soo Busy.
hivi unafikiri kwa nini watu wa vijijini hakuna hata network lakini bado. Ni masikini wa kutupwa?
 
Dunia hii kila kitu kipo ama kwa asili ama kwa bahati mbaya, hatuwezi sote kuwa matajiri na siyo kweli kwamba matajiri wote wamefika hapo baada ya kuacha hivyo vitu. So far, maisha wala si utajiri na utajiri hauwezi kuwa maisha.
 
Kusema akili kama hizi ndiyo tofuti ya tajili na masikini inapothibitika. Huenda utajili ungefichwa sumbawanga watu wangepanda basis kuufata, ungefichwa Paris watu wangeufuata lakini Ulifichwa kwenye ubongo Wa kila mtu, ndio maana hata ikitokea twende mji Mpya tukiwa watupu, baada ya mwezi tu tajili atajulikana.
kwani ungenisoma tu nakupita ungealibikiwa nini? Maana sielewi umenijibu nini.
 
kumshauri mtanzania inataka moyo, jibu lake ni kwa nini na wewe umefanya/ujafanya ivo. badala ya kuchukua ushauri tena wa bure ana kuswalika maswali
 
Maisha ni akili na neema zake mungu, sidhani kuna mtu anaweza nunua simu ya laki saba au million hali hajui kesho itakuaje! Wengine ni zawadi tu, ,pia smart phone ni muhimu utatembea na TV muda wote? Smart phone inakupa habari muda wote na mahali popote, mwenye kutaka kuitumia kwa faida atatumia na asietaka atsishia kupost vitu vya ovyo. Smart phone ni kama shule vile, wapo wanaotumia shule vzuri na wengine wanaona shule ni sehemu ya starehe!
 
Back
Top Bottom