Epuka kuwa miongoni mwa wasaliti bali jitahidi uwe kati ya waliowabadilisha wasaliti na kuwa watu wazuri

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Ukitaka uishi kwa amani pasipo msongo wa mawazo wa mapenzi basi jali mambo yako na sio kumchunguza mwenzako.

Sawa una haki kujua anafanya nini na nani na wapi kwa mda gani na mara ngapi. lakini utaweza mzuia asifanye? Au ukijua itakusaidia nini zaidi ya kukuvunja moyo wako.

Unapo chunguza simu yake kujua sms zilizo ingia au watu anao wasiliana nao ni kujitesa tu maana wapo wengine ambao anakutana nao kazini au shuleni.... Ama ana namba ambayo wewe huijui.

Msaliti hufanya usaliti popote pale na waweza kuta mpangaji mwenzako au ndugu na rafiki wa karibu ndiye mwizi wako.

Huwezi pambana na kumshinda msaliti maana huwa amejiandaa kuhakikisha hajulikani na hata akijulikana bado kuna kuwa na mengi usiyo yajua.. Usipoteze muda wako kutaka kujua yupo na nani, badala yake angalia kama familia ana itunza na anakuheshimu kama mke au mume wake... Usitake kusaliti kisa umesalitiwa maana ni kujikomoa. Jenga tabia ya kuchunguza afya mara kwa mara na kuwa makini kuhusu afya yako.

Usaliti unaumiza pale unaposalitiwa na kudharauliwa na kubadilika kabisa kwa tabia ya mwenza wako. Yote yanataka uvumilivu na ujasiri kuyakabili. Huwezi mfanya aache usaliti mpaka atakapoamua kuacha yeye mwenyewe, ukitaka utumie nguvu na vitisho mtaishia kugombana na kuacha utagombana na kuwaacha wangapi sababu ya hili?? Usitumie nguvu kama hujaolewa au hujamuoa ni bora kuachana nae aendelee na hao anao watamani. Usijidanganye kuwa ukianza kuishi nae ndipo atatulia.. anza kumbadilisha kabla ya ndoa ukishindwa achana nae hata kama unampenda.

Msaliti hana alama na mda wowote anatenda tukio. Kikubwa epuka kuwa miongon mwa wasaliti bali jitahidi uwe kati ya walio wabadilisha wasaliti na kuwa watu wazuri. Usijisifie kuwa wako ametulia wanao mfahamu njia zake watakucheka.

Ramadhaan Qareem
 
somo zuri sana hili.....asante sana.......mmesikia....usiguse simu ya mwenzio....
 
Back
Top Bottom