Epuka Kutatua Tatizo Kwa Njia Zisizo Sahihi.

Meizon

JF-Expert Member
Jan 13, 2014
279
105
Katika upana wa mada hii, nitajaribu kugusia sehemu ndogo sana ambayo ni muhimu sana, namna ya kutatua matatizo kwa njia sahihi. Siandiki hatua za kutatua changamoto zako ila nitakuorodheshea mambo muhimu yakuyazingatia pindi unapo tatua tatizo lililopo mbele yako.


(1) Kuwa na uelewa wa kutosha juu ya tatizo lako. (Hapa utaepuka kukuza athari za tatizo lako)

(2) Lenga kutatua tatizo na sio kuondoa tatizo tu. (Hapa itakufanya usiharakishe katika maamuzi badala yake uwe na maamuzi ya uhakika)

(3) Tazama kesho zaidi. (Usiangalie Leo tu, jaribu kuona matokeo hata baada ya miezi na miaka)

(4) Tunza kumbukumbu. (Hii itakufanya ukue kila baada ya kukumbana na changamoto kwani hutasumbuka endapo changamoto itajirudia tena)

Kwa uelwa mdogo nilionao nimefikia hitimisho kwamba utatuzi wa tatizo ni kipengele cha pili! Cha kwanza ni kuliepuka tatizo au hata changamoto! Japo neno changamoto linameza maana nzima ya neno tatizo na kuleta taswira tofauti kidogo.

Mfano; kama tatizo lako ni madeni sugu basi ni vyema ujue kwanza namna ya kuepukana na madeni ndipo ujifinze kanuni za kujikwamua (utatuzi) kutoka kwenye tatizo la madeni endapo utajikuta katika hali hiyo.

Kukupa urahisi wa kuelewa kile nilichokiwasilisha kwako Leo nimeambatanisha mfano halisi juu ya njia sahihi kutatua tatizo lako.

4b1f2d4e618121f633caf3d3a3635e7c.jpg


Hayati Muammar Gaddafi na Saddam Hussein ni watawala wakubwa kuwahi tokea duniani ambao hakika wengi wetu tumepata kuzisikia habari zao. Niliposoma historia zao na hatima zao nikapata hili; Leo hii ukizitazama nchi walizokuwa wakiziongoza kama maraisi utagundua hali ni mbaya sana zaidi ya mwanzo walipokuwa madarakani.

Tatizo ni kwamba walikuwa ni watawala wasioachia madaraka, wala wasiokubaliana na demokrasia! Lakini tatizo hili utatuzi wake ndio ulinihuzunisha sana kwani haukuwa sahihi. Muamar Gaddafi wa Libya alipewa majina ya dictator, katiri bila kujali mema aliyoyafanya, watu wa Libya wakadhani kumuua ndio suruhisho. (Waliruka vipengele vyote nilivyo orodhesha hapo juu hasa cha 3). Leo hii Libya haina muelekeo.

Saddam Hussein wa Iraq pia alitambulika kama dictator na gaidi mkubwa bila kuyajua mema aliyokuwa akiyafanya mwishowe akanyongwa wakidhani ni suruhisho. Leo hii Iraq ndio kiwanda cha magaidi duniani!

#Do your best to solve problems without dissolving in them.
 

Attachments

  • IMG_20170201_192550_133.jpg
    IMG_20170201_192550_133.jpg
    50.6 KB · Views: 81
Ningepewa sehemu ya kurekebisha, nisingepunguza kitu hapo.
Ila ningeongeza hatua moja na ningeipa kipaumbele zaidi..
kumuomba mungu anijalie hekima , kabla sijaanza kulitatua.
Ni sawa kabisa
 
Back
Top Bottom