Epuka kuingia katika mahusiano ya ndoa kwa sababu hizi

Himidini

JF-Expert Member
May 8, 2013
5,534
4,185
^^
Furaha ya maisha ya ndoa haiji kwa bahati, ni matokeo ya juhudi umakini na kushirikisha imani uliyonayo.Katika mambo unayopaswa kuyaepuka unapotaka kuruhusu maisha ya ndoa ni haya yafuatayo
....
KULIPIZA KISASI JUU YA MAHUSIANO YALIYOVUNJIKA
Kuna watu wana hulka ya kutokubali kushindwa.Wapo tayari kujionyesha au kusema uongo kuwa wana wenzi wapya (hata kama si kweli) ili wawaumize wale waliowaacha. Kwa wale ambao wameamua kuyakubali mahusiano mapya bila kujiridhisha kama yanawafaa au la isipokuwa kujionyesha kuwa X-wao basi watambue wanajiingiza katika ndoa kwa sababu ya hisia za kisasi na sio kuendana (perfect match)
....
UASI DHIDI YA WAZAZI
Ni kweli kuwa si wakati wote wazazi wako sahihi ktk maamuzi juu yako,lakini kutoroka kwenu ili ukaolewe kisa umenyimwa uhuru au kuoa kwa sababu umeamua kujitegemea pasipo kujua uzito wa kumudu maisha ya wawili,huko ni kuasi ndugu,wazazi na kuasi misingi ya ndoa ambayo pamoja na mambo mengine inahitaji ukomavu wa akili,uelewa na kujitegemea kuliko kamilifu.
....
NGUVU YA PESA
Si ajabu ukaona vijana wa kiume wanaoa au kuolewa na wamama wenye pesa kutokana na hali ngumu ya maisha,ugumu wa ajira,upofu wa kuwa wao wanajua mapenzi n.k Lakini ukweli hautayumbishwa daima kuwa KUNA FEDHEHA NYINGI MWANAUME KULISHWA NA MWANAMKE
Upande wa wanawake hususani mabinti ambao wanaamini kuwa pesa ni jawabu la kila kitu ktk ndoa ,kwao pesa italeta amani,pesa ni mume mwema,pesa itanunua upendo wa ndugu,pesa itatibu maumivu ya hisia,pesa italeta tamu ya tendo la ndoa,pesa italea watoto n.k Basi wafikiri upya kwa sababu uzuri wa jambo ni kipimo cha ubaya wake. Hivyo kwa mtu makini,pesa haitakuwa nafasi ya kwanza ktk kumridhisha kuingia katika ndoa
....
MSUKUMO WA FAMILIA,NDUGU na JAMII
Hutokea mara kadhaa mtu akajikuta analinganishwa tu na mwingine ktk jamii,ofisi,jirani,au mtaa basi utawasikia watu wanasema 'oa fulani' au 'olewa na fulani' Huyo mtajwa ame-match na jamii haku-match na wewe!
Vijana wote wa kike na wa kiume hupata msukumo wa nje (social pressure) lakini wanawake huwa zaidi hasa umri unapoanzia miaka 25+ , na zaidi ni kuwaona wenzao waliowaacha nyuma wana watoto hivyo kukubaliana na jamii inayowasukuma.
Tathimini vema,mitihani ya ndoa haiwasubiri hao bali wewe unaekubali bila kutimiza upendo.
...
NAKUTAKIA MAAMUZI BORA HUSUSANI kipindi hichi ambacho tutashuhudia magari ya harusi yakipishana,watu wakienda likizo za kikazi kutafuta wenza wao!
^^
 
Ahsante sana mheshimiwa Himidini mie nimekusoma vyema nadhani ume experience mengi sana katika maisha ya mahusiano.
 
Upo sahihi ndugu japo mapenzi pesa watakupinga ila ukweli ushawapa.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
oa kwa sababu umejiandaa vya kutosha ktk nyanja zote za kimaisha na uwe wakati uliokubalika na Mungu, ndugu umeshauri vema.

Back
Top Bottom