Epuka kuibiwa gari kwa kutumia funguo za ziada

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
May 4, 2020
3,327
9,327
Note:

Uzi huu unawahusu tu watu ambao gari zao zina Immobilizer

Kama una funguo inafanana na hizi hapa chini. Then kaa hapa usome.


images (2).jpeg

images (1).jpeg

images.jpeg






Ipo hivi....

Kuna baadhi ya malalamiko watu wanalalamika kwamba wizi wa magari huenda unasababishwa na watu ambao walikuwa wamiliki wa hayo magari au mafundi wanaoprogram hizo funguo. (Unaweza kutumia akili hiyo pia kwa wanaochonga funguo za kawaida).

Kwa funguo ambazo ni Smart key kama hizo nilizozipost hapo juu. Kuna namna ambayo tunaweza kuangalia na tukaona ni funguo ngapi zimekuwa programmed kwa ajili ya kutumika kwenye hiyo gari.

Mfano

Screenshot_2021-09-24-12-19-40-221_com.us.thinkdiag.plus.jpg



Mfano ukiangalia hiyo picha hapo juu. Kuna sehemu pameandikwa 'Number of Registered key codes' hizo ndio idadi ya funguo zilizokuwa registered kwenye immo ya hiyo gari.

Kwa hiyo kama hapo inakuonesha kuna funguo 5 halafu wewe unayo moja tu, na hizo shida zingine hujui hata kama zipo, then probably kuna watu wanazo.

The gud thing inawezekana kudisable funguo ambazo hazipo mikononi mwako na ukaenable zile tu ambazo tunazitumia.

Kwa lugha nyingine kama kama kuna mtu ana funguo nyingine ya hiyo gari yako. Tukiidisable hatoweza kuitumia kwenye hiyo gari.

Alamsiki.

Karibu tukufanyie Computer diagnosis na tukurekebishie matatizo ya gari lako. Hata kama tatizo umedumu nalo kwa muda mrefu. Gari yoyote ndogo kampuni yoyote.

Instagram: @Car_diagnostic_solutions_tz
Facebook: @Cardiagosticstz

Tupo Dar, Magomeni Mwembechai.

Tupigie 0621 221 606.

images.jpeg
 
Mkuu kama hautojali ni aina gani ya OBD tools za kileo zitumikazo kuangalia matatizo ya magari? Kama utaweza kuniorodheshea tu hapa au PM tafadhali naomba.

Ukiorodhesha au kunipa majina ya kampuni zinazotengeneza hizo tools siyo mbaya.

Just a clarification

OBD2 inapima gari za Japan kuanzia 2008. Ndio maana watu wengi wanazinunua wanaishia kuziweka ndani kama mapambo. Pia haipimi kitu kingine zaidi ya Power train.

I think labda unazungumzia Computer Diagnostic tools.
 
Just a clarification

OBD2 inapima gari za Japan kuanzia 2008. Ndio maana watu wengi wanazinunua wanaishia kuziweka ndani kama mapambo. Pia haipimi kitu kingine zaidi ya Power train.

I think labda unazungumzia Computer Diagnostic tools.
Hizo hizo mkuu, lengo kuu nataka kujifunza japo sina idea yoyote ya magari. Niligoogle nikaishia kupata hilo jina la OBD (on board diagnosis).
 
Diagnostic tools inategemea na bajeti yako zipo hata za zaidi ya 10m
Mimi sihitaji kuzinunua wala sina mpango wa kuzitumia, shida yangu nijue majina yake au jina la kampuni inayotengeneza hivyo vifaa. Au kama unafahamu forum inayohusika na hizo tools niambie tu.
 
Mimi sihitaji kuzinunua wala sina mpango wa kuzitumia, shida yangu nijue majina yake au jina la kampuni inayotengeneza hivyo vifaa. Au kama unafahamu forum inayohusika na hizo tools niambie tu.

Kampuni zipo nyingi Autel, Autoboss, Snap, Xtool, n.k.
 
Swali, Gari yangu nimepoteza funguo wenye remote je inaweekana kupata remote nyingine bola kufunga remote ya hizi security alarm?
Z.jpg
FUNGUO WANGU UNAFANANA NA HUU
 
Back
Top Bottom