MC RAS PAROKO
JF-Expert Member
- Feb 14, 2013
- 622
- 602
Ni matumaini yangu mu wazima wa afya.
Kwa leo naomba kujuzwa na walio wataalamu kwenye sekta ya ujenzi kwa nini teknolojia hii ya kutumia panel za EPS (Expanded Polystyrene) haitumiki sana hapa kwetu Tz?
Sababu za kutaka kupata ufafanuzikatika hili nikwamba, nimeona wenzetu majirani wanatumia sana aina hii ya ujenzi ambayo kwa maelezo ya wengi ni nafuuna salama kutiko ujenzi wa kutumia matofali kama wengi tulivyozoea. Imefika mahali hata taasisi za serikali naona nao wanatumia mfumo huu kujenga nyumba zao za gharama nafuu ila hapa kwetu nimejaribu kutafuta hata wauzaji tu pengine wanijuze mawili matatu ila nimekosa. kwa yeyote mwenye kujua zaidi kuhusu hii teknolojia atusaidie tafadhali wengi tunaweza kuponea hapa sababu inasemekana zinaweza kujenga ghorofa hadi 22 kwenda juu. Uswazi huku nikiweka hata 2 tu inatosha kuwachungulia wenzangu kwa chini. sababu haina gharama nyingi kama mnavyoona katika picha na ni muda mfupi tu jengo linakamilika.
naomba kuwasilisha