Epimedium/horn goat weed yanapatikana Tanzania?

El'son

JF-Expert Member
Jun 3, 2012
380
324
Habari zenu wakuu
images+%2812%29.jpg
images+%2810%29.jpg
horny-goat-weed-epimedium-grandiflorum-img_opt.jpg
katika tembea tembea kwenye mitandao nikakutana aina ya mmea unaitwa EPIMEDIUM au maarufu kama HORN GOAT WEED

Asili ya huu mmea ni China na inasemekana mmea huu miaka mingi ulitumika kama dawa ya kuongeza kiume huko China. Mpaka sasa bado unatumika na umejipatia umaarufu duniani kwa kurejesha heshima kwa wanaume baada ya kufanikiwa kuliamsha DUDE.

Hivyo nikawa nimepata wazo humu humu nchini naamini mimea kama hii inaweza kuwepo ila kutokana na kukosekana watafiti tukashindwa kutambua umuhimu wake. Hivyo nimeambatanisha picha hapo kuomba kama kuna mtu alishawahi kuuona sehemu na anafahamu kwa jina la Kiswahili atuelekeze ili tuweze kuwaokoa wale wanaofedheheka kwa kushindwa kuliamsha dude.

Naomba niwatakie usiku mwema na Natumai jamii forum hakuna linaloshindikana tutapata kile tulichokusudia kwa faida yetu sote. Asanteni naomba kuwasilisha.
 
Umenikumbusha scientific names za Weeds.
Unakariri hadi unashikwa na mafua.
 
Tungepata mtaalamu anaeujua ingekuwa vyema sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom