Epica9 yaliza taasisi serikali, malipo mengi yakwama!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Epica9 yaliza taasisi serikali, malipo mengi yakwama!!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Losambo, Oct 25, 2012.

 1. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wizara ya Fedha huko nuyma hadi kwa mwaka wa fedha 2011/2012 ilikuwa ikitumia mfumo wa malipo Epica7 ambao baadae ulipendekezwa ubadilishwe ili kurekebisha baadhi ya kasoro ilizokuwa nazo. Mfumo huo mpya unaitwa Epica9. Mfumo huo mpya unaotajwa kuwa umeboroshwa kwa kuhusisha;

  1. Fedha kwenda moja kwa moja Hazina badala ya awali kutoka BoT - Hazina kisha BoT kama mlipaji.
  2. Mfumo huo umgehusisha malipo ya moja kwa moja kupitia akaunti ya mlipwaji au wenyewe kuiita TIS
  3 Mfumo huo unadaiwa kudhibiti mianya ya wizi yaani upo "secured" zaidi.

  Kabla ya kuanza kutumika mfumo huo Wizara ya Fedha ilifanya seminar nyingi ili kuwaelimisha wafanyakazi wake ambao ndiyo watumiaji wakuu.

  Nije kwenye mada sasa,

  Tokea mfumo huo uanze umeleta shida kubwa sana kwa kukwamisha malipo ya karibu taasisi zote zinazotegemea malipo toka serikali kuu kupitia hazina!!!!!

  Ingawaje ni mfumo mpya lakini matatizo yake yamevuka mipaka, mfano ni mishahara ya askari polisi ambao bado hawapitii bank baadhi ya mikoa au vituo mpaka leo bado hawajapata!!!!! Ukitoa hilo, hata wadau wengine ambao fedha zao ambazo zimeingizwa huko wanalia kilio maana hawajui lini watapata uhakika wa malipo hayo!!!! Uchunguzi ambao nimeufanya karibu mikoa tisa ya Tanzania Bara umebainisha matatizo yanayofanana,
  1.Taasisi nyingi za serikali huletewa fedha kwa karatasi inayoitwa "Warrant of Fund". Pindi zinapopelekwa hazina karibu zote hazionekani mpaka kwa mbinde sana, jambo ambalo halikuwepo kwenye Epica7!!!!
  2. Hata kama zikionekana bado mfumo huo hautoi uhakika wa kuweza kuprint hundi!!!!
  3. Kucacpture voucher moja hadi nyingine kama mtandao ukiwepo ni rahisi mtu anayetoka Dar - Moro kufika kabla ya mtu wa hazina kukamilisha transaction moja!!!! (Hakuna chumvi katika hilo). Hapo bado huja aprove transaction hiyo!!!!
  4. Pamoja na matatizo yake lakini bado mfumo huo unadaowa kutokuwa "friend user"

  Taarifa ambazo hazina mawaa zinasema hata kuchelewa kupatikana kwa mishahara kwa watumishi wa umma kabla ya sikukuu ya Iddy Mubarak hasa ambao wanategemea kupitia bank kunatokana na mfumo huo mpya kukataa kufanya kazi na kusababisha bank ya NMB kushindwa kugawa fedha kwenye mabanki na akaunti za watu.

  Kutokana na yote hayo nini maoni yangu?????

  Mfumo huo unajenga chuki kubwa sana kwa watu hawaoni sababu ya kupata tabu kwa jambo ambalo wao wanaliita ufisadi wa Epica9. Wadau wanajiuliza kwa nini mfumo huo usifanyiwe kazi kabla ya kuanza kutumika???? Zaidi ya yote, inasadikiwa mafungu ya serikali bado hayajaanza kutoka kama inavyokusudiwa lakini system inasumbua namna hiyo na bado baadhi ya vitu havijawa implemented kama TIS lakini matatizo ni haya je itakuwaje vitavyokuwa intergrated???

  Namalizia kwa kusema "Je Epica9 ni ufisadi mwingine ndani ya Wizara ya Fedha????

  Matatizo ya system hiyo yalizungumziwa kidogo na Raia Mwema - Hazina wakwama kulipa
   
 2. Gogo la choo

  Gogo la choo JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 8, 2012
  Messages: 714
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  usinikumbushe maumivu..mimi toka mwezi wa saba kuna kaDSA kangu kamekwama na huo usenge wa EPICA..!!wanatuua njaa tu huku Halmashauri yetu ya Mpitimbi..
   
 3. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Nchi italipuka kama hili litaachwa liendelee, Epica9 sioni utofauti na kikundi chochote kinachohatarisha amani nchini.
   
 4. bibliography

  bibliography JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 608
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  epic nation aka epica 9 ni usenge mimi toka mwez wa saba sijapokea salariii mpaka leo
   
 5. Gogo la choo

  Gogo la choo JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 8, 2012
  Messages: 714
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Daaahh..acha kabisaaa..njaa tu!!
   
 6. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Watoto wa kishua hawewezi kuelewa hili, ila sisi wasakanyoka ambao ukivusha tarehe mbili natamani niandamane sema naogopa JWTZ watanitoa nyongo!!!!
   
 7. bibliography

  bibliography JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 608
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  njaa haina ushua wala usakanyoka wakishua wote ndio waliokua wakwanza kupata salarii ndani ya epic nation
   
 8. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  kama huo mfumo mpya wa Epica9 kwanini tusirudie ule ule wa zamani Epica7????...kuna haja gani ya kukimbilia vitu vipya ambavyo hatujui ni jinsi gani tuvitumie???...huu ndo uzaifu mwingine wa serikali inaonekana waliopewa semina juu ya Epica9 siyo walengwa, inaweza walichomekwa wakusanya posho tu kama ilivyozoeleka na wanaopaswa kutumia huo mfumo wakaachwa pembeni..na haya madhara yake sasa.
   
 9. Polisi

  Polisi JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 2,087
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Mfumo unaitwa epicor 9.05 na si epica9. Kilichopo ni changamoto na wala si matatizo kama unavyodhani. Kama ulifanya utafiti basi nadhani ni ule wa 'observation' maana ungewahoji watumiaji usingeandika utumbo kama huu.
   
 10. ARV

  ARV JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 6, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 304
  Trophy Points: 180
  Kutumia Epicor 9 ni sharti tulilopewa na nchi zinazotupa mikopo hasa marekani, walisema epicor 7.3 iliyokuwa inatumika mwanzo ilikuwa imepitwa na wakati na ilikuwa inaweza kutumiwa na wajanja kuchota fedha(haikuwa secured vizuri) kwa hiyo epicor 9 tumelazimishwa tutake tusitake kutumia ni lazima.
   
 11. Asante

  Asante JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 18, 2009
  Messages: 1,960
  Likes Received: 297
  Trophy Points: 180
 12. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  poleni sana vijana wa jk (watumishi wa umma)
   
 13. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Walioenda ni wahusika kabisa. Watumiaji ndiyo wanaolalamika sasa sijui unataka nini tena zaidi ya observation???
   
 14. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,148
  Likes Received: 876
  Trophy Points: 280
  Watu kama ninyi ndio janga la kitaifa, mimi ni mmoja wa watumiaji wa huo mfumo ukweli ni kwamba serikali haikujipanga kwenye kuestablish hiyo system. Ni mtu tu ameamua kushinikiza ili apate 10%
   
 15. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Humu tunaishi na watu wengi, kwa jinsi alivyoponda nahisi moja kwa moja labda nae ni miongoni mwa watu walioandika dodoso la kubadilisha mfumo huo na baadae kupata 10%.

  Back to the point, karibu wadau wengi sana wanaulalamikia mfumo huo wa malipo kwa jinsi ulivyo kero, na hapo bado hauja loaded mambo mengine maana walikuwa wanaenda nao kwa hatua,hatua ya kwanza tu umeleta balaa!!!!
   
 16. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Katika hali kama hii akipita mchonganishi akasema hazina nyeupe watu wataamini kumbe tatizo ni mfumo huo.
   
 17. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #17
  Oct 26, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Umenikumbusha maumivu. Maana.mie ni mkandarasi na nadai halamashauri tangu mwezi wa nane mpaka leo mara waniambie mtandao unasumbua na nilipowabana wakaniambia mfumo mpya wa epicor 9 unasumbua ili waprint voucha na cheque
   
 18. D

  Dossa Member

  #18
  Oct 26, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Ni tatizo kweli , the system is very slow alafu ina stuck mara kwa mara imagine kwa wiki inatoa voucher moja au mbili . Kuna mlundikano mkubwa wa mafaili ambapo sasa fedha za utendaji kazi hazipatikani .Bado wakandarasi nao wanadai fedha zao nyingi tu kutoka taasisi za kiserikali kama halmashauri n.k. kimsingi malengo ya miradi na maendeleo ya kiutendaji hayawezi kufikiwa kwa wakati kama malipo ni tatizo .Haya utanipimaje kwa OPRAS wakati targeted goals sijazi meet? Ni tatizo kubwa watumishi wanalia ,madiwani wanalia ,wakandarasi nao wanafanya fujo hawataki kuelewa tatizo tabu tupu .Kama TZ haijajipanga kiteknolojia haina haja ya kukurupukia mambo wakati bado system nyingi zina tumia server...ambazo zenyewe ni ubabaishaji tu
   
 19. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  usemayo ni kwel kuna malipo yanatakiwa kufanywa kwa wananch flani so imekubalika hyo system isitumike coz itachukua mwaka kuyakamilisha!
   
 20. Inanambo

  Inanambo JF-Expert Member

  #20
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,864
  Likes Received: 1,148
  Trophy Points: 280
  Njaa kali NMB hawajapeleka Allowance yangu CRDb ni mwezi sasa Master card inachubuka kwa kuchek salio
   
Loading...