ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,131
- 931
kushindwa kuwataja walioficha Hela Uswisi ni Ujinga,asema Kibonde. Akizungumza katika kipindi cha Jahazi leo tarehe 22.11.2012, bila kutaja jina, Kibonde amedai kuwa yeye anashangaa hata waandishi walioshindwa kumuuliza ukweli kuhusu madai ya kuwepo kwa watanzania wenye fedha nje ya nchi. Yeye anaona yule anaedai kuwa ana ushahidi wa kufichwa mabilioni nje ya nchi bila kuwataja wahusika ili kurahisisha kazi ya uchunguzi hana akili na ana nia ya kujitafutia umaarufu tu. Watangazaji wenzake akina Kayanda na Wasiwasi Mwabulambo wameonekana kukubaliana na mawazo ya Kibonde! na kusema huyu ambae anaropoka tu kuwepo kwa walioficha hela Uswisi bila kuwataja ni "MPUMBAVU"
Kwa tafsri ya moja kwa moja na bila kupinda ukweli, kwa kuwa hoja ya kuwepo kwa watanzania wenye akaunti USWISI ilitolewa Bungeni na Mhe. Zitto Kabwe Mbunge wa Chadema, kauli hii ya Kibonde itakuwa inamhusu sana mtoa hoja huyo (Mhe. Zitto) na sio mwingine.