Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Zipo aina kuu nne za watu ambazo zimegawanyika kutokana na tabia walizo nazo.
Tabia hizo ni kutawala (Choleric – Dominance), mhamasishaji (Sanguine - infuluencing), asiyeyumbishwa (Phlegmatic (steadiness) na mstaarabu (Melancholy - compliane). Ukiweza kujua tabia hizo, utaona ni rahisi kuishi na watu kwa kuwa tayari utakuwa umeshazifahamu tabia hizo.
Leo tutaanza kuangalia tabia ya kutawala. Utawala ni namna ya kuendesha shughuli za kutawala au ni hali ya kupenda enzi.
Kutawala ni tabia kuu ya kwanza ambayo mtu hupenda kutawala.Ni shupavu wa maneno na nadharia, ni mwoga na mwepesi wa kukata tamaa. Mtu huyu anajiamini sana katika maamuzi yake na hajali maoni ya watu wengine hata yakiwa bora kuliko ya kwake. Anapenda kubadilisha mambo bila kushauriana na mtu yeyote.Huongea zaidi ya matendo
Ni vigumu kukubali kama ana shida hata akiwa na shida. Haonyeshi kuhuzunika au kushituka hata akipokea taarifa mbaya. Hata hivyo, mtu huyu si mvumilivu, ni mwepesi wa kukasirika na ni vigumu kumpendeza.
Kama tulivyoona mtu wa tabia hii anapenda kuongoza na kutawala wengine. Huwa hapendi kuongozwa mara kwa mara linapotokea jambo huwa mstari wa mbele kutoa maelekezo. Ndivyo alivyo, hivyo mara nyingine huweza akapendwa na watu kutokana na namna anavyotawala wenzake au akachukiwa.
Huweza kuchukiwa kama akiwa ni mtu anayependa kuamrisha na kuonekana kuwa yeye ni mjuaji kuliko wengine.
Wakati mwingine hupenda kubadilisha mambo bila kushauriwa. Hapa ina maanisha kuwa huwa anajali mtazamo wake binafsi bila kushirikisha wengine. Ni vizuri kupata ushauri wa wengine, kwani wakati mwingine mtu wa tabia hii atabadilisha jambo bila kupata ushauri ambalo litampa wakati mgumu.
Anajiamini katika uamuzi wake na hajali maoni ya wengine. Si vibaya kujiamini katika maisha, ila ni vizuri katika kujiamini kwako wakati mwingine ukasikiliza na maoni ya wengine, kwani waweza kuharibikiwa katika maamuzi yako.
Mtu wa tabia hii akumbuke kuwa pamoja na kujiamini kwake, wako watu wengine wenye maoni ambayo yanaweza kumsaidia. Kwani moja ya sifa za mtawala yoyote awe mtu anayependa kusikiliza maoni ya watu wengine na kuyatendea kazi kwa kuyapima. Katika maoni hayo yapo yanayoweza kumsaidia na mengine yanaweza kumpotosha.