Epa na mambo yake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Epa na mambo yake

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by kinepi_nepi, Oct 30, 2008.

 1. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Vigogo wa Kagoda, Jeetu Patel waogopwa

  Mwandishi Wetu Oktoba 29, 2008

  Yadaiwa ushahidi dhidi yao 'dhaifu'
  'Kondoo wa kafara' ndiyo watakaoshitakiwa


  ZIKIWA zimebakia siku mbili kwisha kwa muda uliotolewa kwa timu ya Rais iliyokabidhiwa jukumu la kuchunguza wizi wa fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania, watuhumiwa wakuu watatu wa wizi huo wanaelekea kuumiza vichwa vya viongozi na watendaji wakuu serikalini na ndani ya chama tawala cha CCM kutokana na nguvu kubwa waliyonayo.

  Wanaoteswa na jinsi ya kuwashughulikia watuhumiwa hao ni pamoja na Rais Jakaya Kikwete, aliyeunda timu na baadaye kuiongezea muda huku akitoa kauli zinazopishana kuhusu hatua za kuchukua ikiwa ni pamoja na kuwashitaki waliohusika na jinai hiyo na ile kauli ya kuwa wasiolipa fedha ndio watakaofikishwa mahakamani.

  Habari za uhakika kutoka serikalini zinaeleza kwamba, suala la kuwachukulia ama kutowachukulia hatua watuhumiwa hao wakuu limekuwa likiisumbua timu ya Rais inayoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, kutokana na kile kinachoelezwa kwamba watuhumiwa hao wakuu walikuwa "makini" katika kuchukua fedha za EPA na hata wakati wa urejeshaji wake.

  Ofisa Mwandamizi wa serikali ameliambia RAIA MWEMA kwamba watuhumiwa wakuu watatu ambao wananchi wengi wanataka wafikishwe mahakamani hawataguswa; angalau kwa sasa kutokana na watuhumiwa hao kuwa makini wakati wa mchakato wa kuchukua fedha za EPA na ndio pekee waliorejesha fedha zote walizochukua kwa wakati, ikiwa ni "kutimiza masharti yaliyotolewa na Rais Jakaya Kikwete".

  "Wakati wa mchakato wa kuchukua fedha za EPA watuhumiwa hao ambao watu wengi, vikiwamo vyombo vya habari, wanataka wachukuliwe hatua walikuwa makini mno kiasi cha kuwafanya wachunguzi wakose makosa ya kijinai ya kuweza kuwafikisha mahakamani na walipopewa muda wa kulipa walilipa kwa wakati na kwa uangalifu mkubwa kiasi cha kuwa vigumu kuwabana," alisema ofisa huyo.

  "Hata hivyo, bado kuna mambo yanayoangaliwa ikiwa yatakamilika lolote linaweza kutokea; hasa ikiwa uongozi wa juu wa serikali utafanya maamuzi magumu kwa kuwa uamuzi wa kisiasa pia ni muhimu katika kufikia maamuzi katika suala la fedha za EPA kwa kuwa linaweza kusababisha mtikisiko mkubwa katika siasa za Tanzania," alisema Ofisa huyo ambaye hata hivyo anakiri udhaifu katika kuwashughulikia wahusika hao.

  Uchunguzi wa RAIA MWEMA kwa muda mrefu sasa umebaini kuwapo kwa watuhumiwa ambao wanaweza kufanywa 'kondoo wa kafara' kutokana na msimamo wao katika kutoa maelezo kwenye timu iliyokabidhiwa jukumu la kuchunguza tuhuma hizo, na pia kwa kile kilichoelezwa "kiburi cha ajabu" walichoonyesha watuhumiwa hao.

  Watuhumiwa wanaotarajiwa kufikishwa mahakamani ni wale ambao wanaelezwa wamegoma kutoa ushirikiano kwa Serikali ikiwa ni pamoja na kushindwa kulipa fedha na baadhi kukataa kutoa maelezo waliyotakiwa kuyatoa, na badala yake wamekuwa wakitoa maelezo kuonyesha kwamba wao walishiriki katika uchukuaji wa fedha za EPA kwa kufuata taratibu na sheria na baadhi walidai kupata fedha hizo kwa kazi walizofanya.

  Utata mkubwa zaidi unaelezwa kutarajiwa kuibuka kuhusiana na fedha hizo kutumika katika uchaguzi wa mwaka 2005 hususan katika kukisaidia Chama cha Mapinduzi (CCM; huku baadhi wakitajwa kuwa na ushahidi wa jinsi fedha hizo zilivyotumika, jambo ambalo tayari limekwisha kukanushwa na viongozi wa chama hicho tawala.

  Imeelezwa kwamba mmoja wa watuhumiwa, ambaye ni mfanyabiashara maarufu mwenye asili ya kiasia, ameelezwa kujitokeza kulipa fedha za kampuni ya Kagoda Agricultural Limited, kampuni iliyochota zaidi ya Shilingi bilioni 40, lakini pamoja na kujitokeza kwake, kumekuwa na kigugumizi cha kumuunganisha na makosa ya jinai yaliyofanywa wakati wa kuchukua fedha hizo.

  "Unajua ni kichekesho, tunaambiwa wahusika wa Kagoda hawajulikani, lakini anakuja mtu analipa fedha za Kagoda na anajulikana kuwa analipa kwa niaba ya nani, halafu tunaendelea kusema hatuwafahamu wahusika wa kampuni hiyo ambayo imethibitika kufanya jinai. Kwa kweli inatuaibisha sana sisi tuliosomea kazi ya upelelezi wa mambo ya jinai na ni aibu pia kwa serikali nzima kuwaogopa watu," anasema ofisa mwingine mwandamizi wa serikali mwenye uzoefu na mambo ya upelelezi wa jinai.

  Kampuni ya Kagoda imekuwa ikitajwa kutofahamika ofisi zake wala wahusika wake wakuu kutopatikana, lakini kitendo cha kujitokeza kwa mtu kulipa fedha za kampuni hiyo kwenye timu ya Rais, kimeelezwa kutokuwa na tofauti yoyote na watuhumiwa wengine wa wizi wanaokutwa na mali, hata wale walionunua mali hiyo kwa wezi.

  "Kuna wafungwa wengi ambao wamefungwa kwa kukutwa na mali za wizi, baadhi hawakuhusika hata na wizi; bali walinunua mali hizo kwa watu wengine tena baadhi bila hata ya kujua kama ni mali za wizi, sasa mtu anakuja analipa fedha zilizoibwa unamwachia, si tungewaambia kina Kasusura (Justine) na wenzake walipe tu fedha walizoiba wakati ule badala ya kuwashitaki?" anasema ofisa huyo ndani ya serikali.

  Habari zaidi zinaeleza kwamba miongoni mwa watuhumiwa ambao Serikali inapata kigugumizi kuwashitaki ni pamoja na mfanyabiashara Jeetu Patel na wenzake wanaofahamika ambao makampuni yao manane ni miongoni mwa makampuni yaliyochukua zaidi ya Shilingi bilioni 90 ambazo zimethibitika kupatikana kwa njia ya udanganyifu na kwa kutumia nyaraka za kughushi.

  Imeelezwa kwamba, pamoja na kuwa katika orodha ya makampuni yaliyopata fedha za EPA kwa kughushi nyaraka, Jeetu Patel, anaelezwa kutoa ushirikiano mkubwa kwa timu ya Rais, huku akiwa na kumbukumbu kubwa ya kuchangia kwa kiwango kikubwa kampeni za CCM za mwaka 2005, ikiwa ni pamoja na kuchangia ununuzi wa magari na misaada mingine, mambo ambayo yameelezwa kumpa kinga mfanyabiashara huyo.

  Wanaotajwa kuwa wanaweza kufikishwa mahakamani, ni wale ambao kampuni zao zimo katika kampuni zilizochukua jumla ya Shilingi bilioni 44, fedha ambazo wakaguzi walisema wameshindwa kuthibitisha kuwapo kwa jinai na kupendekeza kufanyika kwa ukaguzi mpana zaidi wa kutumia kampuni za kimataifa zenye uzoefu katika uhakiki.

  Imeelezwa kwamba kesi zitakazofunguliwa sasa zinalenga kushusha joto la kisiasa lililopanda kutokana na kuonekana kwamba watawala hawachukui hatua thabiti juu ya tuhuma za ufisadi zinazowakabili wanasiasa na matajiri kadhaa walio karibu na chama tawala wakati huu wa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.

  Kwa mujibu wa habari hizo, kesi hizo zinatakiwa ziendelee hadi hata baada ya 2010 ili kutoa picha kwamba utawala umedhamiria kupambana na ufisadi hata kama kesi hizo zitakuwa zikitajwa tu na watuhumiwa, hasa wale wa EPA wakiwa ndani chini ya tuhuma kama za hujuma ya uchumi, kughushi na kula njama kuiba.

  Wanaotajwa kufikishwa mahakamani ni wamiliki wa kampuni za Changanyikeni Residential Complex Limited, Malegesi Law Chambers, G&T International Limited na Karnel Meals Holdings Ltd zinazomilikiwa na Jose Van de Merwe, Samson Mapunda na Charles Mabina, Beredy Maregesi, Octavio Timoth, Johnson Lukaza na Mwesigwa Rutakyamilwa Lukazas.

  Raia Mwema limefahamishwa kwamba watakaofikishwa mahakamani kwanza ni Maregesi, Mapunda na Lukaza katika hatua inayozua minong'ono ya kuwa watuhumiwa wakubwa wa fedha za EPA wanakingiwa kifua kwa kuwa wana uhusiano wa karibu na chama tawala ama kuwapo kwa 'mikono michafu'.

  "Ni kama sasa wanataka kutolewa kafara. Hata muda uliotolewa wa Oktoba 31 ni kama uliwalenga wao. Wamekuwa wakikataa kurudisha fedha wakidai kwamba wao walifanya kazi, walioiba ni hao ambao sasa wanaelezwa kwamba wamerudisha. Kwamba wao sasa wanataka kushitakiwa huku wakubwa wakiachwa maana yake kubwa ni kwamba watawala wanafunika kombe," alisema mmoja wa watu walio karibu na watuhumiwa hao.

  Kampuni zilizokwiba fedha nyingi zaidi kutoka akaunti ya EPA na ambazo sasa kwa utaratibu huu wamiliki wake hawataguswa ni pamoja na ya Kagoda Agricultural Limited kampuni nane za Jeetu Patel.

  Kwa mujibu wa wakaguzi, Kagoda ilighushi nyaraka zilizotumika kuchota zaidi ya Shilingi bilioni 40 wakati Jeetu Patel naye amechota zaidi ya nusu ya fedha zilizoibwa akitumia kampuni nane.

  Maofisa wa Serikali hususan wale wa vyombo vya dola, wakiwamo wajumbe wa kikosi kazi (task force) kilichokabidhiwa kazi ya kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya wahusika waliochota fedha hizo, walipoulizwa kuhusu kushitakiwa kwa wachache tu katika wizi wa EPA wote walidai kwamba muda aliotoa Rais Jakaya Kikwete kukamilika kwa suala hilo haujakwisha na ni yeye mwenye kauli ya mwisho.

  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Jinai (DCI), Robert Manumba, ambaye alitajwa na vyanzo vya habari kwamba ofisi yake ndiyo inakamilisha taratibu za kuwashitaki wahusika aliiambia Raia Mwema wiki iliyopita kwamba hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa msemaji wa kikosi kazi (task force) ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, ambaye naye amenukuliwa akisema suala hilo linapaswa kuzungumziwa na Rais ambaye ndiye aliyetoa muda wa ziada.

  Kauli kama hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hosea ambaye naye hakuwa tayari kuzungumzia hatua ambayo wamefikia katika kuwashitaki wahusika, huku Ofisa Mwandamizi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, akisema kwamba kila kitu kitajulikana siku chache zijazo.

  Hata hivyo, Raia Mwema limethibitishiwa kwamba Maregesi, Mapunda na Lukaza, wanatajwa kuwa watu watakaotolewa kafara kutokana na kile kilichoelezwa kwamba wamekuwa na "jeuri ya Kiafrika" kwa kukataa kulipa fedha wanazotuhumiwa kuzichota.

  Imeelezwa kwamba tokea awali watuhumiwa hao wamekuwa wakigoma 'kutoa ushirikiano' jambo ambalo limeelezwa kuwakera baadhi ya wanasiasa na watendaji wa Serikali walioamua sasa kuwaburuza mahakamani.

  Raia Mwema imethibitisha kwamba bado akaunti na hati za kusafiria za watuhumiwa hao zinaendelea kushikiliwa hata baada ya muda wa miezi sita kisheria kupita kwa maelekezo ya ofisi ya Mwanasheria Mkuu.

  Habari zinaeleza kwamba awali watuhumiwa hao walikuwa wafikishwe mahakamani sambamba na maofisa wa BoT waliohusika katika mchakato wa EPA, lakini uamuzi huo ulibadilishwa baada ya tishio kutoka kwa watumishi hao kwamba 'wataanika' kila kitu hadharani wakitolewa kafara.

  "Baada ya watumishi hao wa BoT kutishia kumwaga kila kitu hadharani, mwelekeo umebadilika na sasa wataitwa kama mashahidi wa upande wa serikali kesi hizo zitakapofikishwa mahakamani, lakini bado wanaweza kuiharibia serikali watakapoamua kutaja watu ambao wamefichwa," anasema mtoa habari wetu aliye karibu na vyombo vya dola.

  Raia Mwema imefahamishwa kwamba kesi hizo zinatarajiwa kutumika kama mwavuli wa kuivusha serikali kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, kukwepa wimbi la manung'uniko ya wazi kwamba serikali ya CCM imekuwa ikiwalea watuhumiwa wa ufisadi, wengi wakiwa ni wafadhili wa chama hicho.

  Wakaguzi wa ndani na wale wa nje, walibaini kuwapo kwa wizi mkubwa wa fedha katika akaunti ya EPA katika kipindi cha mwaka mmoja pekee wa 2005/2006 ambako zilipotea zaidi ya Shilingi bilioni 133.

  Wakaguzi hao walibaini kwamba kati ya fedha hizo shilingi bilioni 90 ni zile ambazo zimethibitika kuchotwa kwa kutumia nyaraka za kughushi, sehemu kubwa zikiwa zimekwenda kwa wafanyabiashara wawili, wamiliki halisi wa Kagoda Agricultural Limited na Jeetu Patel kupitia kampuni zake nane.

  Ripoti ya Wakaguzi wa Kampuni ya Ernst and Young waliofanya kazi kwa niaba ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ilionyesha kwamba kiasi cha Shilingi 90,359,078,804.00 zililipwa kwa kampuni 13 ambazo zilitumia kumbukumbu, nyaraka na hati zilizo batili na za kugushi na kwamba kampuni hizo hazikustahili kulipwa chochote.

  Wakaguzi hao na Ikulu, kupitia taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wake, Philemon Luhanjo, Januari 9, 2008, walipendekeza moja kwa moja bila kuuma maneno kwamba wahusika wa kampuni hizo 13 wachukuliwe hatua za kisheria mara moja, kauli ambayo Rais Kikwete aliirejea katika hotuba yake bungeni, lakini bila ukali tena.

  Makampuni ambayo Jeetu Patel anahusika nayo na ambayo yamethibitika kughushi nyaraka na kuchota fedha BoT ni Navycut Tobacco (T) Limited, Ndovu Soaps Limited, Bina Resorts Limited, Bencon International Limited, Maltan Mining Company Limited, Bora Hotels & Apartments Limited, Venus Hotels Limited, and B.V. Holdings Limited.

  Pamoja na kampuni hizo za Jeetu Patel, kampuni nyingine zilizohusika na jinai ya kughushi nyaraka ni pamoja na Kagoda Agriculture Limited ambayo wanaoonekana katika nyaraka ni John Kyomuhendo mwenye hisa 40 na Francis William anayemiliki hisa 60 katika kampuni hiyo.

  Kampuni nyingine ni V.B & Associeties Company zinazomilikiwa na Devendra Patel na Jantkumar Chandubhai Patel na Changanyikeni Residential Complex Limited inayomilikiwa na Jose Van de Merwe, Samson Mapunda na Charles Mabina ikiwa na makao yake, Sinza, Kumekucha, Dar es Salaam.

  Pia katika orodha hiyo ya kampuni 13 zilizoghushi nyaraka ambazo wahusika wake wamependekezwa kuchukuliwa hatua za kisheria mara moja ni Money Planners & Consultants inayomilikiwa na Paul Nyingo na Fundi Kitungi na kampuni ya Njake Hotel & Tours Limited inayomilikiwa Japhet Lema, Anna Lema, Abel Lema, Derick Lema na Benard Lema wa Arusha.

  Jeetu Patel katika baadhi ya kampuni anashirikiana na wafanyabiashara wengine wa Dar es Salaam ambao wanatajwa kushiriana naye katika kuhamisha fedha hizo kwenda nje kwa kuzibadili kutoka shilingi za Kitanzania kwenda Dola za Merakani ama Euro bila kufuata mkondo halali wa fedha kinyume cha Sheria ya Udhibiti wa Fedha Haramu.

  Miongoni mwa wanaotajwa kushirikiana na Jeetu Patel ni Sidik Yacoubu kupitia kampuni yao ya Ndovu Soap Limited ambayo kwa mujibu wa nyaraka za Wakala wa Leseni na Usajili wa Kampuni (BRELA), kampuni hiyo yenye namba ya usajili 20536 ya Februari 3, 1992, wamiliki wake ni Jayantulal Chandubhai Patel na Sidik Yacoubu.

  Katika kampuni ya Bora Hotels and Apartments iliyosajiliwa Septemba 8, 2005 inaonyeshwa katika orodha ya BRELA kwamba wamiliki wake wamo Jayantkumar Chandubhai Patel na Devandra Patel wakati Bina Resort Limited iliyosajiliwa Machi 31, 2005, wamo Jayantikumar Chandubhai Patel na Devendra Patel.

  Kampuni ya Maltan Mining Company iliyosajiliwa Machi 8, 1993 inamilikiwa na Jantkumar Chandubhai Patel na Hariharier Radhakrishna wakati Navy Cut Tobacco iliyosajiliwa Oktoba 12, mwaka 1995 inamilikiwa na Jantkumar Chandubhai Patel na Radakrishna.

  Kampuni nyingine ni Bencon Limited, B.V Holdings, Venus Hotels na V.B & Associeties Company zinazomilikiwa na Devendra Patel na Jantkumar Chandubhai Patel, ambazo zote zilisajiliwa Aprili 4, 2005.

  Katika orodha ya BRELA imo pia kampuni ya Excellent Service Limited inayomilikiwa na Emil Samanya, Peter Sabas na Elisifa Ngowi ambaye anatajwa kuwa ni Ofisa Mwandamizi wa Idara ya Usalama wa Taifa, ambaye yumo katika task force inayochunguza wizi huo. Kampuni hiyo ilisajiliwa Mei 13, 1992 na kupewa namba 26959.

  Ngowi anahusishwa pia katika kampuni nyingine ya Clyton Marketing iliyosajiliwa Juni 6, 2005 akiwa na mwenzake Edwin Mtoi, ambaye haikuweza kufahamika mara moja anafanya shughuli gani zaidi ya kuwa katika kampuni hiyo.

  Wamiliki wengine waliofahamika ni Rajabu Maranda na Thabit Katunda ambao wanatajwa kumiliki kampuni ya Liqiud Service Limited ambayo usajili wake ulifanyika Desemba 12, 2004 na kupewa namba 15007.

  Wamiliki wengine waliofahamika ni Johnson Lukaza na Mwesigwa Rutakyamilwa Lukaza ambao wao wanamiliki kampuni ya Karnel Meals Holdings Ltd ambayo usajili wake ulipatikana Agosti 4, 1998, Mibale Farm iliyosajiliwa Septemba 2, 2005 na kupewa namba 154039 ambayo inamilikiwa na Kizza Selemani na Farijala Hussein, Malegesi Law Chambers inayomilikiwa na Beredy Malegesi ambayo ilisajiliwa Septemba 24, 2001.

  Wamiliki wengine ni Paul Nyingo na Fundi Kitungi, wanaomiliki Kampuni ya Money Planners & Consultants iliyosajiliwa Machi 22, 2005 na Kiloloma & Bros Enterprises inayomilikiwa na Charies Kissa, ambayo ilisajiliwa Aprili 8, 2005.

  Katika ukusanyaji wa fedha hizo, task force ya serikali inaelezwa kukusanya shilingi 53,738,835,392/= fedha ambazo Rais Kikwete ameagiza ziingizwe katika mfuko maalumu kwa ajili ya kusaidia sekta ya kilimo zikichanganywa na nyingine zinazotarajiwa kufikia shilingi 64,844,770,688/=
   
 2. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #2
  Oct 30, 2008
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nimetonywa kuwa pesa za EPA hazirudishwi kama Kikwete na waziri wa Fedha Mkullo alivyoliambia Bunge.

  Kinachofanyika ni wezi wa pesa za EPA kuelezea hizo pesa walizoiba wamezitumiaje ( KU-ACCOUNT FOR) siyo kurudisha fedha taslimu na kuingiza katika Akaunti ambayo waweza ona pesa zile pale zimerudishwa.Kikwete na waziri wake wa Fedha Mkullo walilidanganya bunge waliposema zimerejeshwa|?
  Kazi kwa bunge kuthibitisha.Habari ndo hiyo.

  Wale mnaosubiri Pesa za EPA ziingie kwenye Account ziende kwenye pembejeo au zilipe malimbikizo ya madai walimu au wastaafu wa jumuiya ya Afrika mashariki mnaota ndoto za mchana hakuna pesa taslimu zilizorejeshwa zinazolingana na hayo mabilioni yaliyosemwa na Akina Mkullo bungeni.

  Wezi wanatoa tu maelezo ya walitumiaje pesa walizokwiba.

  Hotuba ya Kikwete kuwa zinaenda kwenye pembejeo sijui zitawekwa
  Benki ya TIB inaelekea ilikuwa danganya toto jinga au kauli ya funika kombe mwanaharamu apite? Wabunge wampigie makofi kwa hoja hewa? Habari ndo hiyo.

  Anayebisha aihoji serikali hizo pesa ziko Account gani?
  Benki ipi? na waombe wakaguzi huria wahakiki ukweli huo kuona kama hizo pesa zipo na zimerudishwa na hao maruhuni vibaka wa EPA.Ili wabunge kabla ya kupiga makofi wawe na uhakika wa wanachopigia makofi badala ya kupiga makofi tu kama mabwege mtozini yasiyojua bee wala tee ndani ya bunge kwa ushabiki tu vya vyama bila kuwa na vitu kichwani mwao.
   
 3. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Mmiliki wa Kagoda na Jeetu wasiposhitakiwa basi tufuate nyayo za wazee wa EA, yaani tuandamane kutoa hisia zetu kuwa haki hakuna wakati sheria ipo
   
 4. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Jamani napata taabu kidogo na takwimu hizi za the citizen kuhusu fedha zinazokusanywa, zilizokusanywa na zilizosemwa zimekusanywa.

  EPA scam: Who among these will be charged ?

  Source: TheCitizen Newspaper
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  Nami nakubaliana na hilo...maana tangu 2005 hadi leo eti warudishe hapana hy sio kwelii hata kidogo wanatudanganya kama wajinga na watoto wadogo
   
 6. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,487
  Likes Received: 81,782
  Trophy Points: 280
  EPA scam: Who among these will be charged ?

  By Mkinga Mkinga
  THE CITIZEN
  30.10.2008 @22:51 EAT

  Time is running out for the 19 suspects expected to be arraigned over the Sh133 billion Bank of Tanzania External Payments Arrears (EPA) account fraud, as the deadline given to them to refund the stolen money expires today.

  Having keenly followed the saga of the monumental rip-off, the public's attention will be riveted on finding out who were behind the 13 companies that scooped a whopping Sh90 billion from the central bank through fraudulent payments.

  The special task force, which President Jakaya Kikwete appointed in February to investigate the massive theft and recover the money, reportedly failed to trace nine other companies that received the balance of the money.

  The presidential task force, which is led by Attorney-General Johnson Mwanyika, includes the Director of the Prevention and Combating of Corruption Bureau, Dr Edward Hosea, and the Inspector-General of Police, Mr Said Mwema, is expected to haul the suspects to court as they failed to take advantaged of a presidential amnesty window to hand back the loot.

  However, there were reports yesterday that two of the nine companies, G&T International Limited and Excellent Services Limited, may have been traced in the past few days.

  The Citizen can today reveal some of the suspects behind the 13 companies, and the names of the 19 individuals who could face prosecution from Monday.

  Those within the sights of the presidential task force, include Mr Jantkumar Chandubhai Patel, who is popularly known as Jeetu Patel, Mr Jayantulal Chandubhai Patel and Mr Devendra Patel, who between them own nine of the 13 companies suspected of involvement in the fraud.

  The three are listed at the Registrar of Companies in Dar es Salaam as joint directors in Bencon International Limited, V.B. & Associates Company Limited, Bina Resorts Limited, Venus Hotels Limited and Maltan Mining Company Limited.

  They also are directors in Bora Hotels and Apartments Limited, B.V Holdings Limited, Ndovu Soap and Navy Cut Tobacco (T) Ltd.

  The others are Mr John Kyomhendo and Mr Francis William of Kagoda Agricultural Limited, Mr Japhet Lema, Ms Anna Lema, Mr Derrick Lema, Mr Abel Lema and Mr Bernard Lema, all directors of Njake Hotels and Tours and Mr Harierier Radhakrishna, who is a joint director at Maltan Mining Company Limited and Navy Cut Tobacco (T) Ltd with Mr Patel.

  Mr Sadik Yacoub of Ndovu Soap, Mr Jose Van De Merwe, Mr Samson Mapunda and Mr Charles Mabina of Changanyikeni Residential Complex Ltd and Mr Paul Nyingo and Mr Fundi Kitungi of Money Planners & Consultants, are also targeted.

  A prominent Dar es Salaam advocate associated with the firm, Malegesi Law Chambers, is also implicated in the scandal.

  The Mwanyika team is holding the business registration files all of these companies as investigations continue.

  There was conflicting information from inside the Government and the corridors of justice over what is likely to happen on Monday.

  One view that has gained credence over the past two days is that the Mwanyika team might charge some of the suspects, and the names of three people, whose passports have been impounded, were being mentioned.
  A source close to the task force told

  The Citizen that the team was also considering seeking another extension of the presidential amnesty to give the suspects more time to continue repaying the money. This school of thought was pegging its argument on President Kikwete's apparent insistence that the team give priority to recovery instead of litigation, which he feared could last for several years.

  It's true that there has been a directive to that effect. The team is reportedly consulting widely before reaching a decision that will not raise eyebrow, another well-connected source said.

  In his keynote address to Parliament in August, when he extended the amnesty to the suspects, President Kikwete declared that the Government would use the recovered funds to finance an expanded fertiliser subsidy programme for farmers.
  He also said part of the money would be spent on re-capitalising the State-owned Tanzania Investment Bank (TIB) to offer loans to farmers.

  The Mwanyika team managed to recover only Sh234 million from the suspects during the two- month presidential amnesty period.

  The amount was way below the more than Sh10 billion they had hoped to rake in.

  President Kikwete granted the amnesty for the 13 companies to refund Sh10.7 billion before today.

  "If any of the suspects fails to repay the money by the set deadline, then the authorities are under instructions to begin criminal prosecution as of November 1," President Kikwete told Parliament.

  He said he had accepted an appeal from the Mwanyika team to extend the time to recover at least 73 per cent of the EPA loot.

  The President said then that Sh53.7 billion had so far been recovered but that the team expected more, to bring the figure to Sh64.8 billion by the expiry of the October deadline.

  However, sources close to the team have confided to The Citizen that only Sh43 billion had been recovered, most of it from one company.
   
 7. K

  Kazi ipo Member

  #7
  Oct 31, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka sana mama Anne Kilango alipokuwa anachangia hotuba ya bajeti alisema kuwa anataka kuona hizo fedha za EPA zinarudishwa kwenye viroba. Sijui kama wezangu mlimuelewa, mimi nafikiri alikuwa na maana kuwa pawe kweli na uthibitisho kuwa hizo fedha zimerudi.

  Lakini aliongeza kuwa kama hazitarudi basi bungeni hapatakalika. Tusubiri tuone,kwani mpaka sasa hazijarudi na bado Mama Kilango yupo tu Bungeni.
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Alipewa kalipio na kamati za chama (sisiem) aache longo longo!
   
 9. M

  Mama JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  JK: "Watanzania eh"

  WTZ: "Eh"

  JK: "Mimi Rais wenu!"

  WTZ: "eh!"

  JK: "Sina nguvu tena!"

  WTZ: "Eh"

  JK: "Ya kukamata mafisadi"

  WTZ: "Eh"

  JK: "Mafisadi ni wajanja"

  WTZ: "Eh"

  JK: "Wamekomba Benki Kuu"

  WTZ. "Eh" kwa shauku!

  JK: "Wamelangua na Rada"

  WTZ. "Eh" kwa shauku!

  JK: "Wameiba Meremeta"

  WTZ. "Eh" kwa shauku!

  JK: "Wamechota nayo EPA"

  WTZ. "Eh" kwa shauku!

  JK: "Sasa kimbieni!

  Watanzania kila mmoja anaanza kutimka kivyake na mwenye kuweza kufanya ufisadi zaidi anaendelea kufanya tu kwani rais keshashindwa; na kupelekea ufisadi kuendelea kukomaa siku hadi siku. Hivyo ndivyo anvyoonekana Rais Kikwete.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,487
  Likes Received: 81,782
  Trophy Points: 280
  Imetolewa mara ya mwisho: 31.10.2008 0020 EAT

  Hatma ya EPA:Marekani: Kikwete awe mkali
  *Yataka sheria ziachwe zifuate mkondo wake
  *Yasubiri uamuzi kuhusu sakata la ufisadi
  *Yaguswa na usanii wa kampuni ya Richmond
  *Yaahidi Rais Obama au McCain kuja nchini


  Na Hassan Abbas

  BALOZI wa Marekani nchini, Bw. Mark Green amekuwa mwanadiplomasia wa kwanza nchini kumshauri Rais Jakaya Kikwete kuhusu nini anachopaswa kukifanya saa chache kabla hajaamua hatima ya waliokwapua mabilioni kwenye Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).

  Balozi Green aliyesisitiza kuwa mafisadi si watu wa kuachwa hata kama ni vigogo na kutaka sheria zichukue mkondo wake, ameifafanulia Majira jinsi alivyoguswa baada ya kuona kampuni ya kimarekani ya Richmond ilivyohusika katika utata kwenye sekta ya umeme nchini.

  Balozi Green alisema hayo jana katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini kwake Dar es Salaam kuzungumzia masuala mbalimbali kuhusu uchaguzi wa Marekani, mtikisiko wa uchumi, hali ya kisiasa nchini na mtazamo wake kuhusu wagombea, maseneta Barack Obama na John McCain.

  EPA na Richmond

  Balozi Green alisema hawezi kujinasibu kuwa Marekani ni Taifa la mfano katika kupambana na rushwa, lakini alisisitiza kuwa katika miaka 232 ya Uhuru wa Taifa hilo, ujenzi wa jamii yenye kuwajibika kwa kufuata utawala wa sheria usiomwogopa mtu ndio msingi.

  "Rais Kikwete anafanya kazi kubwa ya kujenga Taifa. Lakini vita dhidi ya ufisadi inahitaji kutowaacha watu wakatamba. Sheria ichukue mkondo wake hata kama mtu ni mashuhuri kiasi gani.

  "Sisi Marekani tumekuwa na azma ya wazi kuwa kiongozi wa umma akiiba fedha za watu, anachunguzwa na kuchukuliwa hatua. Wamarekani ni wakarimu sana kutoa fedha zao kusaidia watu, lakini ni wakali sana wanapoona inafanyiwa ufisadi. Rais Kikwete akitumia sheria atafanikiwa," alisema Balozi Green na kusisitiza kuwa katika sakata la EPA, waliopoka fedha hizo wanapaswa kuwajibishwa.

  Akifafanua kuhusu hilo, Balozi Green alisema Rais Kikwete alitaja mikakati mizuri alipozungumza bungeni kuhusu namna atakavyowashughulikia mafisadi wa EPA.

  "Rais alitaja mikakati mizuri. Tunasubiri kuona atakavyoitekeleza," alisema. Akizungumza bungeni Agosti 21 mwaka huu, Rais Kikwete aliwapa mafisadi hao hadi Oktoba 30 (jana) wawe wamerejesha fedha hizo, vinginevyo ifikapo Novemba mosi (kesho) wawe wameburutwa kortini.

  Sakata la Richmond, kampuni iliyoshinda zabuni ya kufua umeme wa mamilioni nchini ikijieleza kuwa ilitokea Marekani, ni moja ya matukio yaliyoitikisa Serikali ya Rais Kikwete mwanzoni tu mwa utawala wake.

  Akilizungumzia sakata hilo, Balozi Green alisema Serikali ya Tanzania katika kupambana na rushwa inapaswa kufuata sheria bila kujali mhusika au kampuni husika imetoka nchi gani.

  "Suala la Richmond najua ilikuja ikafanya kazi kupitia kampuni iliyosajiliwa nchini. Lakini bila kujali kampuni hiyo ilitoka wapi, Serikali inapaswa kuchukua sheria haraka inapoona kuna ufisadi," alisema huku akikiri kuwa ukweli kwamba kampuni hiyo ilijieleza kutoka Marekani, ulimsumbua wakati wa sakata hilo, ingawa ubalozi wake hauwajibiki moja kwa moja katika mikataba inayohusu kampuni binafsi.

  Uchaguzi wa Marekani

  Balozi Green alikiri kuwa uchaguzi wa mwaka huu wa nchi hiyo umekuwa na hamasa kubwa hasa kutokana na ushiriki wa Seneta Obama, Mmarekani mwenmye asili ya Afrika wa kwanza kuteuliwa na chama kikuu kuwania urais.

  "Ni kweli kwamba ushiriki wa Seneta Obama umeibua hamasa miongoni mwa Wamarekani wengi, hilo ni suala lisilo na ubishi. Lakini pia hata uteuzi wa Seneta McCain naye umeibua ushawishi katika baadhi ya nchi.

  "Wakati huku Afrika Obama anaonekana kuwa na ushawishi, McCain naye ni kivutio hasa katika nchi za Mashariki ya Mbali ambako kutokana na historia yake ya kushiriki vita ya Vietnamu na kwa miaka mingi aliyokaa kwenye Kamati ya Mambo ya Nje kwenye Bunge la Seneti, alishiriki masuala mengi yanayohusu eneo hilo," alisema Balozi Green ambaye ni mfuasi wa Republican.

  Alisema, akiwatathmini wagombea hao wawili, anaona kuwa wote kwa sera zao, wana uwezo wa kuisaidia Marekani iwapo mmojawapo ataingia Ikulu.

  "Ukiangalia sera zao, hakuna shaka kwamba wote (McCain na Obama) wana mikakati ya dhati kuisaidia Marekani na historia zao zinaonesha wana uwezo mkubwa," aliongeza.

  Akizungumzia somo ambalo nchi za Afrika zinaweza kujifunza kutokana na kampeni zinazoendelea sasa nchini Marekani, Balozi Green alisema kubwa ni umuhimu wa watu kujadiliana masuala ya kitaifa kwa uwazi na mwishowe kila mwananchi akawa na fursa ya kupiga kura na kumchagua kiongozi anayemtaka.

  "Siwezi kusema kuwa Marekani ina demokrasia ya kuigwa, sote bado tunajifunza kutoka kwa kila mmoja. Lakini kama ilivyoonekana, mijadala ya wazi ni kitu muhimu ili kujadili masuala ya kitaifa na mwishowe kuheshimu uhuru wa kupiga kura. Naamini mkiimarisha hili, Afrika na Tanzania zitafanikiwa," aliongeza.

  Msukusuko wa uchumi na Afrika

  Balozi Green alikiri kuwa uchumi wa Marekani umetikisika, lakini akazitoa wasiwasi nchi za Afrika hususani Tanzania, kuwa kiwango cha misaada ya Marekani hakitaathirika kutokana na hali hiyo.

  "Kwa mfano, miradi ambayo tumekubali kuisaidia Tanzania ilishapitishwa na fungu lake lipo, kwa hiyo haitaathirika, sioni sababu ya Watanzania kuwa na wasiwasi," alisisitiza.

  Pia alisema hofu ya miradi mingi iliyoanzishwa chini ya utawala wa chama cha Republican nayo kubatilishwa, iwapo kitaingia madarakani chama cha Democrat haina msingi, kwani wakati wa upitishaji wa miradi hiyo Wamarekani hukubaliana kwa pamoja bila kujali itikadi ya vyama.

  "Kwa bahati nzuri nilikuwa kwenye Baraza la Wawakilishi, ni mmoja wa wawakilishi waliopigania kupitishwa kwa sheria iliyounda shirika la Millenium Challenge Account, linalotoa misaada mbalimbali kwa Afrika ikiwamo Tanzania.

  "Bahati nzuri wakati wa kujadili masuala haya, wabunge walikuwa wamoja bila kujali itikadi. Kwa hiyo hakuna atakayeweza kuzuia miradi hii, iliamuliwa kwa sauti ya Wamarekani wote," alisema.

  Obama au McCain kuja Tanzania

  Akizungumzia ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na Marekani, Balozi Green aliisifu kazi nzuri iliyofanywa na Rais wa zamani wa Marekani, Bw. Bill Clinton, ambaye ujio wake nchini na kazi za taasisi zake, ziliwafanya Wamarekani wengi kuijua au kuwa na nia ya kuijua Tanzania.

  "Hata ujio wa Bush, watu wanaweza kunipongeza kwa kufanikisha kuja kwake, lakini historia nzuri iliyowekwa na Clinton ndiyo iliyowazindua Wamarekani wengi kisha akaja Bush na baadaye mkutano wa Sullivan, lakini pia wadhifa wa Rais Kikwete kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, vimeifanya Tanzania kujulikana zaidi.

  Akizungumzia uwezekano wa ofisi yake kuhakikisha Rais ajaye wa Marekani anafuata nyayo hizo kwa kufika nchini, Balozi Green alisema:

  "Nitafurahi kuona siku moja Rais ajaye wa Marekani awe Seneta McCain au Seneta Obama anaitembelea Tanzania, kuimarisha uhusiano mzuri uliopo. Niko tayari kushughulikia hilo ili afike hapa.

  "Bahati nzuri Seneta McCain nimeshawahi kukutana naye wakati nikiwa kwenye Baraza la Wawakilishi, Obama hatujaweza kukutana kwa sababu wakati huo nikiwa kwenye siasa, yeye alikuwa bado yuko chini, lakini naamini wote watakuwa tayari kuja kuiona nchi hii nzuri," aliahidi.

  Balozi Green kitaaluma ni mwanasheria aliyepata kujaribu kuwania ugavana wa jimbo la Wisconsin kupitia chama cha Republican mwaka juzi akapoteza.
   
 11. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2008
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Sio kweli. Gazeti linapotosha. Rais hakutamka maneno "mashitaka ya jinai."

  "Lakini tumekubaliana kwamba itakapofika tarehe 31 Oktoba, 2008 mwisho, ambaye hakulipa mpaka tarehe 1 Novemba, 2008 awe amefikishwa Mahakamani ili Mahakama itusaidie kupata fedha za watu. Kwa hiyo, kuanzia tarehe 1 Novemba, 2008 mshike mshike."

  Kwa hiyo wanashindwa hata kunukuu alichosema Rais wa nchi Bungeni. Wanapotosha Umma. Nikisema hatuna waandishi wa habari Tanzania usidhani ninakuwa nimetoka kunywa wanzuki. Nina maana yangu.
   
 12. Netanyahu

  Netanyahu Senior Member

  #12
  Oct 31, 2008
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 148
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nimeota ndoto ya ajabu sijui ni kweli?

  Nimeota mahojiano kati ya Kamati Raisi na vibaka wa EPA yalikuwa kama ifuatavyo.

  KAMATI:Mtuhumiwa wa wizi wa pesa za EPA tueleze ulivyotumia hela ulizoiba za EPA.

  JIBU:Za kwanza NILIHONGA BILLIONI 1 kwa mahawara zangu

  KAMATI: hizo ulizohonga itabidi urudishe kabla ya October 30.Zingine ulitumiaje?

  JIBU: Nilitoa mabilioni msaada kwa wakati wa Kampeni za uchaguzi kusaidia ushindi

  KAMATI: Sawa hizo ulitumia vizuri tunahesabu zimerejeswa.Zilizobaki ulitumiaje.

  JIBU: Nilijenga ghorofa ZA KUPANGISHA na kuanzisha kampuni feki zisizolipa kodi TRA ambazo mimi mwenyewe nakisia kuwa zilitumika Shilingi bilioni zilizosalia.

  KAMATI: Safi sana umetoa ushirikiano.Kwa hiyo tunaenda kutoa taarifa kuwa jumla ya Pesa ulizorudisha ni zile ulizohonga mahawara ambazo umepewa muda urudishe kujumlisha ulizotoa kwenye Kampeni kujumlisha ulizotuambia unakisia ndizo ulizojenga maghorofa na kuanzisha kampuni feki jumla zitakuwa billioni zinazolingana na ulizokwiba.OK.Uko huru kuendelea na maisha yako kama kawaida.Tutawakilisha Ripoti hii safi kwa Raisin a Waziri awasomee wananchi na bunge.Una oni,lalamiko au chochote?

  JIBU KIBAKA WA EPA:.Asante.Sana wanakamati .Nashukuru sana kwa ushirikiano.Tuko pamoja.Mkihitaji msaada tena 2010 karibuni.

  Kama ndoyo hiyo ni kweli Raisi na Waziri wa fedha watueleze zimerudi shilingi ngapi taslimu ziko akaunti gani benki gani kama wakijiuma meno basi nakubaliana na Mama Kilango watuhumiwa wazibebe kwenye viloba wapeleke bungeni akahesabu spika.

  Bunge lishupalie hili jambo kuna usanii mkubwa.Hata kama wakisema kuna mali wamekamata zenye thamani fulani wabanwe waeleze nani aliwaambia hizo mali zina thamani hiyo isije kuwa mtu anasema kajumba kake kana thamani ya bilioni moja wakati ni ka milioni moja ili atoroke mikono ya sheria au pengine kahonga kamati ili wakubali thamani hivyo kuzalisha EPA ingine.
   
 13. Ether

  Ether Senior Member

  #13
  Oct 31, 2008
  Joined: Mar 16, 2008
  Messages: 137
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  huyu balozi green alitupige mchanga wa macho cause they are the ones who allowed these mafisadis to swindle and steal the EPA $$$.
   
 14. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Niko Tviinii hotuba imemalizika, na hotuba ndiyo kama alivyo tuleta mkulu Halisi....
   
 15. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2008
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  kazi kweli kweli
   
 16. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #16
  Nov 1, 2008
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  dodoso kama zipo kuna mpya
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Nov 3, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,487
  Likes Received: 81,782
  Trophy Points: 280
  Date::11/2/2008
  Wizi wa EPA: Nitachambua faili moja baada ya jingine asema DPP
  Na Ramadhan Semtawa
  Mwananchi


  MKURUGENZI wa Mashtaka ya Umma (DPP) amesema atachambua kwa makini "faili moja baada ya jingine" baada ya kukabidhiwa rasmi mafaili ya wezi wa fedha kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na hivyo kufanya uwezekano wa watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani katika siku chache zijazo kuwa mdogo.

  Kuwasilishwa kwa mafaili ya mafisadi hao walioshindwa kurejesha Sh64 bilioni kati ya Sh133 bilioni zilizochotwa kwenye akaunti hiyo, kunafanya mzigo huo sasa uelemee kwa DPP, Eliezer Felesh ambaye ofisi yake ilikabidhiwa mafaili hayo jana na Mwanasheia Mkuu wa Serikali.

  Hatua hiyo imekuja wakati hali ikiwa tete kutokana na wananchi wa kada mbalimbali, wakiwemo wabunge na wasomi kutaka wezi wote wa fedha hizo wafikishwe mahakamani tofauti na agizo la Rais Jakaya Kikwete kuwa wale ambao wangeshindwa kurejesha fedha hizo kabla ya Oktoba 31 tu ndio wafikishwe mahakamani.

  Kwa mujibu wa duru mbalimbali za kiserikali, kazi kubwa iliyopo sasa inafanywa na Kurugenzi ya Upelelezi ya Makosa ya Jinai ambayo imeelezwa kuwa tayari imewaweka chini ya ulinzi watuhumiwa ikisubiri kuwafikisha mahakamani wakati wowote kwa maelekezo ya DPP, ambaye hana budi kujiridhisha kwanza dhidi ya tuhuma hizo za ufisadi kabla ya kuruhusu sheria ichukue mkondo wake.

  Wakati Wizara ya Sheria na Katiba ikitoa taarifa rasmi ya kuwasilishwa majalada yote ya watuhumiwa kwa DPP, Feleshi alilithibitishia gazeti hili jana kwamba tayari ameanza kuyachambua majalada hayo.

  "Kila jalada linalokuja lazima nilisome, nilipitie kwa umakini... ndiyo utaratibu huo, hatupindishi sheria, lakini hadi sasa (jana) siko katika nafasi ya kueleza idadi ya majalada ambayo yamekuja," alifafanua DPP Feleshi.

  Feleshi, ambaye ni mmoja wa watendaji serikalini wasio na urasimu wa kutoa habari, alisema hakuna mtu atapona au kuonewa katika mchakato huo.

  "Hakuna namna ya mtu kuweza kupona au kuonewa, lazima nifanye Legal Analysis (uchambuzi wa kisheria) kwanza, cha msingi usiulize majalada mangapi, niulize afya yangu tu, niombe uzima tu, kila kitu utaona kitakavyokwenda," alisema DPP Feleshi.

  Feleshi alisisitiza kuwa jambo kubwa na la msingi analoomba ni kuwa na afya njema kwani ana uhakika wa kufanya kazi kwa mujibu wa sheria bila kupindisha.

  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba, aliliambia gazeti hili kwamba polisi sasa inamsikiliza mkuu huyo wa mashitaka.

  Kamishna Manumba alisema DPP ndiyo kiongozi wa kazi hiyo atakolosema polisi itafanya kwa mujibu wa taratibu.

  "Hivi sasa kiongozi wetu ni DPP, atakachosema polisi tutafanya, kazi hii inahusisha taasisi nyingi hivyo mkurugenzi wa mashitaka ndiyo kiongozi wetu," alisisitiza Kamishna Manumba.

  Wakati vigogo hao kutoka ofisi ya DPP na Polisi wakitoa misimamo hiyo, taarifa nyingine kutoka wizara hiyo ya sheria na Katiba iliyotolewa jana mchana na msemaji wake, Omega Ngole, ilisema timu ya rais imetimiza maelekezo yote ya mkuu wa nchi.

  Timu ilisema kiasi cha fedha cha Sh69.3 bilioni alichotaja rais hakijaongezeka hadi kufikia Oktoba 31 na majalada yote ya kesi yameshawasilishwa kwa DPP.

  "Timu inapenda kuarifu umma kuwa maelekezo yote mawili yametekelezwa. Kiasi cha fedha kilichorejeshwa hadi mwishoni mwa Ijumaa (Oktoba 31,2008) ni kilekile kilichotajwa na Mheshimiwa Rais, yaani sh 69.3 bilioni. Aidha, majalada ya kesi yamewasilishwa kwa DPP kwa ajili ya kuyafanyia kazi kama ilivyoelekezwa," alifafanua Ngole.

  Akihutubia taifa Ijumaa, Rais Kikwete alisema ameagiza timu yake kwamba wamiliki wa makampuni 13 ambayo yalichota sh 90.3 bilioni na kisha yakashindwa kurejesha fedha zilizobaki, majalada yao yapelekwe kwa DPP ambaye kikatiba ndiye mwenye mamlaka ya kuandaa taratibu za kufungua mashitaka.

  Hata hivyo, kauli hiyo bado ilionekana kupingwa na baadhi ya Watanzania wa kada mbalimbali ambao walisema wana imani na wanamuunga mkono Rais Kikwete, lakini wakataka mashitaka yasiwe kwa baadhi ya watuhumiwa, bali kwa wote walioiba.

  Lakini, duru nyingine zinadai kuwa uamuzi huo huenda ukawa ni mbinu ya kuwatega mafisadi hao ili warejeshe fedha wote ili kiwe kidhibiti cha kuburuza nacho mahakamani kwa urahisi.

  Ufisadi wa EPA ulibainika katika hesabu za BoT za mwaka 2005/06, baada ya ukaguzi wa kampuni ya Deloitte&Touche ya Afrika Kusini, ambayo ilisitishwa ghafla na Benki Kuu (BoT) kufanya kazi bila sababu za msingi baada ya kubaini Sh40 bilioni zilizochotwa na kampuni ya Kagoda Agriculture Limited.

  Hata hivyo, mwaka jana serikali ilimwagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kutafuta kampuni ya kimataifa ya kufanya tena ukaguzi.

  Ofisi ya CAG iliteua kampuni ya kimataifa ya Ernst&Young, ambayo ilibaini ufisadi huo wa Sh133 bilioni, ambazo zilichotwa na makampuni 22.

  Makampuni 13 yalijichotea sh 90.3 bilioni, ni pamoja na Bencon International LTD of Tanzania, Vb & Associates LTD of Tanzania, Bina Resorts LTD of Tanzania, Venus Hotel LTD of Tanzania, Njake Hotel &Tours LTD, Maltan Mining LTD ya Tanzania.

  Mengine ni Money Planners & Consultants, Bora Hotels & Apartment LTD, B.V Holdings LTD, Ndovu Soaps LTD, Navy Cut Tobacco (T) LTD, Changanyikeni Residential Complex LTD na Kagoda Agriculture LTD.

  Kwa upande wa makampuni tisa yaliyochota Sh42.6 bilioni yanasubiri uchunguzi zaidi unaofanywa kwa kuhusishwa serikali za nchi nyingine baada ya hatua za awali kutotoa majibu mazuri.

  Makampuni yaliyo kwenye sakata hilo ni G&T International LTD, Excellent Services LTD, Mibale Farm, Liquidity Service LTD, Clayton Marketing LTD, M/S Rashtas (T) LTD, Malegesi Law Chambers (Advocates), Kiloma and Brothers na KARNEL LtD.

  Kumbukumbu ya makampuni mengine mawili- Rashtas (T) na G&T International LTD, pamoja na nyaraka za usajili kwa Msajili wa Majina ya Makampuni na Biashara (BRELA), hazikuweza kupatikana.

  Kufikia mwaka 1999 deni katika EPA lilifikia dola 623 milioni, ambazo kati ya hizo dola 325 milioni zilikuwa ni deni la msingi na dola 298 ni riba na baadaye deni likaongezeka hadi kufikia dola 677 milioni.

  Hata hivyo, chini ya Mpango wa Kununua Madeni (Debt Buy Back Scheme) wa mwaka 1994 kati ya serikali na Benki ya Dunia (WB), waliokuwa wanaidai BoT waliombwa wakubali kulipwa sehemu tu ya fedha wanazodai. Wapo waliokubali na wengine kukataa na kuongeza hadi mwaka 2004 taarifa zinaonyesha jumla ya dola 228 zililipwa chini ya mpango huo.

  EPA ni akaunti ya madeni ambayo ilitumika wakati wa Mfumo wa Ujamaa, ambayo akaunti yake ilikuwa katika iliyokuwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) chini ya usimamizi wa BoT.

  Mwaka 1985, EPA ilihamishiwa moja kwa moja BoT, na ndipo mwaka juzi kulipoibuka utata wa tuhuma za ufisadi katika akaunti hiyo kwa mahesabu ya mwaka 2005/06, ambayo utata huo ulisababisha Ernst&Young kufanya ukaguzi kuanzia Septemba sita na kukabidhi ripoti yake kwa CAG mapema Desemba mwaka jana.
   
 18. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #18
  Nov 3, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,233
  Likes Received: 5,619
  Trophy Points: 280
  Kikwete na Usanii wa EPA

  Saturday, 01 November 2008


  HOTUBA ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa kwa Taifa jana jioni imepokelewa kwa hisia tofauti na wananchi wengi huku ikishambuliwa vikali na wapinzani kwa madai ya kushindwa kukidhi matarajio ya wengi hususani katika suala la watuhumiwa wa ufisadi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) Wakizungumza na gazeti hili leo asubuhi, baadhi ya wanasiasa wamesema alichoeleza Rais Kikwete kwenye hotuba yake ni kinyume cha matarajio ya wananchi wengi huku wakidai, amembebesha mzigo mkubwa Mkurugezi ya Mashitaka ya Umma (DPP) kwa jambo ambalo ana uwezo wa kulishughulikia na kudai kuwa kauli aliyoitoa, ni sawa na mchezo wa kuigiza.

  "Tulitarajia Rais atakuja na majina ya hao watu waliorejesha fedha hizo sh. bilioni 69 na sio kutuambia kuwa kampuni tisa hazijulikani zilipo," alisema Mwanasheria wa CHADEMA, Tindu Lisu.

  Amesema watu waliohusika kuchota fedha hizo wanakabiliwa na kosa la jinai, hivyo katika makosa ya aina hiyo haishitakiwi kampuni bali wamiliki na wakurugenzi wake.

  Amesema inashangaza kumsikia Rais akishikilia msimamo wa kutaja makampuni yaliyoshindwa kurejesha fedha hizo kwa lengo la kutaka yafunguliwe kesi ya madai wakati wamiliki wake wanakabiliwa na makosa ya jinai.

  "Haya makampuni yanamilikiwa na watu, yana wakurugenzi wake, kwa nini Rais anaogopa kuwataja majina yao?" Amehoji Lissu. Ameongeza kuwa DPP amepewa mamlaka ya kutekeleza wajibu wake wa kufikisha mbele ya sheria watuhumiwa wa makosa mbalimbali hivyo hapaswi kupata maelekezo kutoka kwa Rais kama alivyofanya kwenye hotuba ya jana.

  "DPP ana uhuru gani kama anasubiri maelekezo kutoka kwa Rais Kikwete?" Amehoji Lissu na kudai kuwa watuhumiwa wa ufisadi katika akaunti ya EPA walipaswa kushughulikiwa siku nyingi, lakini inavyoonekana yeye (Rais) ndiye alizuia.

  Lisu ameenda mbali na kuhoji, " Mbona Rais anazungumzia makampuni, ni kwa nini hataji wakurugenzi na wamiliki wake ni akina nani? Katika makosa ya jinai haishitakiwa kampuni, wanaoshitakiwa ni watu?"

  Amesema kama kweli fedha hizo zimerejeshwa Rais Kikwete alipaswa kuwaeleza Watanzania zimerudishwa na akina nani na tarehe gani." Kwa mazingira haya hatuna sababu yoyote ya kumwamini Rais Kikwete ikiwa hatawaambia Watanzania waliorejesha fedha hizo ni akina nani" amesisitiza.

  Mbunge wa Karatu, Dkt. Wilbroad Slaa, amedai hotuba aliyoitoa Rais ni dalili za wazi za kushindwa kuongoza nchi.

  "Hizi ni dalili za wazi za Rais Kikwete kushindwa kuongoza nchi kwa sababu wezi wanajulikana yeye anawasamehe," amesema na kuongeza kuwa: "Rais hana mamlaka ya kusamehe watu ambao hawajahukumiwa."

  Dkt. Slaa amesisitiza kuwa kwa kauli ya jana tayari Rais Kikwete ametangaza kuwasamehe watuhumiwa wa ufisadi waliorejesha sh. bilioni 69.

  "Hii inaonesha kuwa wapo watu walio juu ya sheria, makosa yote waliyotenda yanajulikana isipokuwa hawafikishwi mahakamani kwa sababu wanalindwa," amesema.

  Amesema Rais Kikwete ameonesha jinsi anavyoongoza nchi kwa upendeleo, ubaguzi na kujenga matabaka. "Kama anaweza afungue magereza yote ili wanaotumikia kifungo waweze kutoka," amesema.

  Dkt. Slaa amesema ni jambo la kushangaza kwa Rais Kikwete kufumbia macho vigogo wa Serikali walioidhinisha fedha hizo, badala yake anataka makampuni yaliyochota kiasi hicho cha fedha kurejesha.

  Kuhusu kauli ya Rais Kikwete kuwa kuna kampuni tisa ambazo hadi sasa Kamati aliyoiunda ikiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jonhson Mwanyika, haijui yalipo, Dkt. Slaa amesema hiyo inaonesha wazi kuwa Rais Kikwete hatulii ofisini na kusoma.

  Amesema wataalamu washauri wote waliochunguza sakata la EPA wameweka wazi kuwa kampuni hizo tisa zimetafutwa na imethibitika zote ni hewa hazijulikani zilipo duniani kote.

  "Kwa nchi masikini kama Tanzania inayotumia kiasi cha asilimia 34 ya misaada iendelee kutumia fedha nyingi kutafuta kampuni ambazo hazipo ni aibu na inaonesha jinsi gani Rais asivyotulia ofisini kwake na kujisomea makabrasha hayo," amesema.

  "Mimi kuanzia sasa sina imani naye, kama wabunge wa upinzani wangekuwa wengi tungeenda mbali zaidi na kuangalia uwezekano wa kumpigia kura ya kutokuwa na imani ndani ya Bunge," amesema.

  Amesema kama katika kikao cha Bunge kijacho hotuba ya Rais itawekwa kwenye ratiba ya mambo yatakayojadiliwa itakuwa ni vizuri kwa wabunge kutumia fursa hiyo kuomba ipigwe kura ya kutokuwa na imani.

  "Kwa sasa haiwezekani kwa sababu kuna kanuni inayokataza kutaja jina la Rais, lakini hotuba yake ikiletwa ili ijadiliwe tutaomba apigiwe kura ya kutokuwa na imani," amesema Dkt. Slaa.

  Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP) Augustino Mrema, amesema inavyoonekana Rais Kikwete ameanza kuiga utaratibu kama aliokuwa nao ambapo alikuwa akiwataka watu wote walioiba kurejesha mali walizoiba.

  "Nilikuwa na utaratibu uliojulikana kama Tajirika na Mrema, naona Rais Kikwete ameanza kufuata nyayo zangu," amesisitiza Bw. Mrema.

  Rais Kikwete katika hotuba yake ya jana alisema suala hilo ameliacha kwa DPP ili aweze kuwachukulia hatua za kisheria.
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Nov 4, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,487
  Likes Received: 81,782
  Trophy Points: 280
  Marekani: Wezi wote wa EPA waadhibiwe

  2008-11-04 12:12:22
  Na Mashaka Mgeta

  Marekani imesema pamoja na watuhumiwa wa kashfa ya wizi wa fedha kwenye Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kurejesha fedha walizoiba, bado wanapaswa kuwajibishwa na kuadhibiwa.

  Kauli hiyo imetolewa siku tatu tu baada ya Rais Jakaya Kikwete, kuhutubia Taifa na kusema idadi kubwa ya wahusika katika kashfa hiyo, wamerudisha fedha walizoiba kutoka EPA.

  Kwa mujibu wa Rais Kikwete mafisadi hao walirejesha Sh 69,326,437,650 kati ya Sh 90,359,078,804 walizoiba kwenye EPA, kwa maana hiyo hawatafikishwa mahakamani kwa kuwa wametekeleza agizo lake la kurejesha fedha kwa muda aliowapa hadi ilipofika Oktoba 31, mwaka huu.

  Badala yake, mafisadi walioshindwa kurejesha Sh 21,032,641,154, ndio tu watakaofikishwa mahakamani, baada ya mchakato wa mashitaka kukamilishwa na Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP).

  Katika majibu yake kwa Nipashe, kuhusu hatua ya serikali kusamehe wezi ambao wamerejesha fedha bila kuwapeleka kortini, Balozi wa Marekani nchini, Mark Green, alisema wote waliohusika na wizi wa EPA wanapaswa kuadhibiwa kwa mujibu wa sheria.

  ``Tunaamini kwamba wahusika wa rushwa, bila kujali nafasi za uongozi ama hadhi yao, wanapaswa kuwajibishwa na kuadhibiwa,``alisema

  Taarifa ya majibu ya Balozi huyo, ilitumwa kwa Nipashe kupitia kwa Ofisa Uhusiano wa Umma katika balozi huo, Jeffery Salaiz.

  Green alisema Marekani inaamini katika uwazi na vita dhidi ya rushwa, kuwa ni misingi mikuu kwa serikali ya Taifa hilo lenye nguvu kubwa za kiuchumi duniani.

  Alisema hakuna Taifa lisilokabiliwa na kashfa za rushwa ikiwemo Marekani, ambapo baadhi ya kesi zinachunguzwa zinawahusisha watu wa ngazi za juu katika utumishi wa umma.

  ``Kwa hakika, jaribio la kweli kwa nchi inayoendeleza utawala bora, uwazi na ukweli, inatekeleza yanayopaswa kufanywa dhidi ya rushwa iliyobainika.

  Kwa mujibu wa tamko la Rais wa Marekani, maarufu kama (PP7750) la mapema mwaka huu, maofisa wa umma wanaokabiliwa na kashfa za rushwa, wategemezi wao wanaonufaika na matunda ya kosa hilo, watazuiliwa kupata `makazi bora’ nchini humo.

  Alisema kufikiwa kwa hatua hiyo kunategemea, ikiwa vitendo vya wahusika wa rushwa vinaathiri maslahi ya Marekani.

  Aliyataja maslahi hayo kuwa ni shughuli za kimataifa za uchumi wa biashara za Marekani, malengo ya misaada ya nje inayotolewa na nchi hiyo, uimarishaji wa taasisi za kidemokrasia na sheria mpya ya rushwa ya mwaka 2008 ya Taifa hilo.

  ``Tamko hilo la Rais linazuia watu fulani waliohusika katika rushwa wasiingie Marekani na kufurahia matunda ya rushwa zao, na linatuma ujumbe mkuu kwamba tumejitolea kusaidia jitihada za kimataifa kutokomeza rushwa popote inapotokea,`` alisema Green.

  Kwa mujibu wa Green, tamko hilo linawahusu viongozi wa umma wanaopokea rushwa ya fedha au kwa namna nyingine, matumizi mabaya ya fedha za umma, kuingilia utendaji wa mahakama, uchaguzi na michakato mingine ya umma.

  Tamko hilo linagusa pia sekta binafsi, kwa watu waliohongwa ama waliokusudia kuwahonga viongozi wa umma, wenzi wao, watoto ama wategemezi wao.

  ``Tutaendelea kufanya kazi kwa karibu na Tanzania, kuondoa mizizi ya rushwa na kuwafikisha katika mkondo wa sheria watuhumiwa wote wa rushwa,`` alisema.

  Warioba ashikilia msimamo dhidi ya rushwa

  Naye Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba, ameendelea kushikilia msimamo wake wa kuwafikisha kortini watuhumiwa wote wa wizi wa EPA, anaripoti mwandishi wetu, Simon Mhina.

  Jaji Warioba jana alikataa kuzungumzia hutuba ya Rais Jakaya Kikwete juu ya mafisadi, na kusema msimamo wake alioutoa siku za nyuma unafahamika hivyo hana cha kuongeza.

  Akizungumza na Nipashe ofisini kwake jijini Dar es Salaam, mwanasiasa huyo alinayeheshimika nchini, alisema hana chakuzungumza ambacho kitazidi yale ambayo ameyazungumza siku za nyuma.

  Awali alipotakiwa kutoa maoni yake kuhusu mafisadi wa EPA juzi, Warioba alisema bado hajasoma kwa kina hutuba ya Rais na akaahidi kwamba atakapokamilisha kazi hiyo, ndipo atatoa maoni yake.

  Hata hivyo, jana alipofuatwa ofisini kwake na mwandishi wa habari hizi, alisema ameisoma hutuba hiyo, lakini hana chakuongeza.

  ``Nyinyi (Nipashe) nimeshazungumza nanyi, msimamo wangu mnaujua, sina cha kuongeza wala cha kupunguza. Siwezi kuzungumza tena juu ya suala la EPA au watuhumiwa wake kwa vile nilishatoa msimamo wangu na wote mnaujua,``alisema.

  Warioba alikiri kwamba tangu Rais atoe hutuba yake waandishi wengi wa habari wamemfuata kwa lengo la kutaka msimamo wake juu ya msimamo wa serikali kuhusu suala hilo.

  ``Lakini mbona mnanifuata mimi tu, kuna nini? Msimamo wangu nilishautoa tena kwa kurudia, sina lingine la Ku-coment,`` alisema.

  Akizungumza na Nipashe katika mahojiano maalum miezi miwili iliyopita, Warioba alisema mafisadi waliochota fedha hizo wafikishwe mahakamani hata kama wamezirejesha.

  ``Tutakuwa tumefanya makosa makubwa na ya kihistoria, kutowafikisha wezi kortini eti kwa sababu ni matajiri.

  Kosa hili litakuwa limeitikisa Tanzania kama nchi taifa. Watu wakijajua kwamba katika nchi yao matajiri hawafikishwi mbele ya sheria (Mahakamani) hawatakuwa na imani na serikali yao, hawataiheshimu serikali,`` alisema na kuongeza:

  ``Kama matajiri wasipofikishwa mahakamani eti kwa ajili ya fedha walizo nazo, basi dola itakuwa imeweka rehani uwezo, madaraka na mamlaka yake kwa mafisadi.``

  Katika mahojiano hayo ambayo yalichapwa kwenye gazeti hili Warioba alikaririwa akisema baada ya kusikiliza mlolongo wa tatizo hilo, ni wazi kwamba waliofanikiwa kuiba fedha za EPA walifanya hivyo baada ya kughushi.

  ``Na kughushi kwenyewe ni kosa la jinai, achilia mbali wizi walioufanya,`` alisema.

  Mbali na hivyo Warioba alisema Watanzania wanayo haki ya kuwajua kwa majina watuhumiwa wa fedha za EPA na kujua kwa undani walitumia mbinu gani na kwa wakati upi, kutekeleza uovu huo.

  Lipumba ashangaa mwalimu kufungwa miaka 240, mafisadi kuwa huru

  Kutoka Tanga Lulu George, PST, anaripoti kuwa Chama cha Wananchi (CUF) kimeeleza kusikitishwa kutokana na Serikali kusita na kushindwa kuchukua hatua za haraka kwa waliochota mabilioni ya shilingi ndani ya BoT badala yake kuwaadhibu wanyonge wachache kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria zisizolingana na makosa yanayowakabili.

  Mwenyekiti wa CUF, Prof Ibrahimu Lipumba, alitoa kauli hiyo mjini hapa akihutubia wafuasi wa Chama hicho kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Mpirani iliyopo katika Kata ya Chongoleani ndani ya Halmashauri ya Jiji la Tanga.

  Alisema hali hiyo imeonyesha udhaifu mkubwa kwa Serikali na kuondoa imani kwa wananchi wake na kwamba sheria ipo kwa ajili ya wanyonge wachache na alitoa mfano wa kufungwa kwa Mwalimu mmoja wa Sekondari ya Mbinga miaka 240 jela kwa kuiba Sh. milioni 24 tu.

  Profesa Lipumba alisema kutokana na hali hiyo hivi sasa Taifa la Tanzania limeonekana kuendeshwa kimatabaka ambapo walionacho ndio wenye nguvu na maskini wanabaki kuwa wanyonge.

  ``Ndugu zangu wa Chongoleani...kuna Mwalimu Mmoja wa Sekondari huko Mbinga kafanya ujanja ujanja wake akaiba Sh. milioni 24, amekamatwa na kusomewa mashitaka 60 ya rushwa...lakini leo tunaelezwa kuwa walioiba bilioni 133 wanazirejesha kana kwamba walikwenda kukopa Saccos,`` alisema Prof.Lipumba na kuongeza.

  ``Hivi kweli hebu tuulizane huyu aliyeiba Sh milioni 24 kafungwa miaka 240 na huyu aliyeiba bilioni 133 na kusamehewa yupi aliyetenda kosa,`` alihoji kiongozi huyo.

  Aliwataka wananchi kutokata tamaa na badala yake waungane kwa pamoja kujipanga vizuri kwenye uchaguzi ujao wa mwaka 2010 kwa kumchagua viongozi bora watakaojali na kuzingatia zaidi maslahi ya nchi badala ya kukimbilia kujilimbikizia mali kwa manufaa yao.


  SOURCE: Nipashe
   
 20. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #20
  Nov 4, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  This is an interesting IR conundrum, naona ndiyo inaweza kuwa financial / legal version ya "R2P".

  On the one hand watu wanaweza kuuliza kwa nini Marekani inaingilia mambo ya ndani ya Tanzania, on the other hand serikali ya Tanzania haifanyi wananchi wanachotaka, na it takes the Americans to voice what the people want, it is interference anyway, but does good interference make the stigma of "big brother" interference go away?

  Above all, wamarekani wametupa msaada mkubwa sana hivi karibuni, wanaweza kujisikia rightly empowered kuangalia tunavyokuwa responsible fiscally, a beggar cannot be sovereign.In this case, sovereignty is hardly high up on the list of priorities since the Americans, whatever their motives (and it pays to be suspicious) are actually advocating a sensible, popular issue, the application -not irregular suspension- of rule of law.

  What's not to like about that?
   
Loading...