EPA: Minyukano ya mafisadi imemwamsha mwenye mali (2)

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,003
EPA: Minyukano ya mafisadi imemwamsha mwenye mali (1)

Joseph Mihangwa Aprili 2, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Kitendo

MBWA mwitu ni mnyama mwindaji hatari kwa wanyama wadogo wadogo porini. Silaha zake ni mbio, meno makali mithili ya kisu chenye ncha kali na ujanja wa porini. Kwa sababu hii ni nadra kwa mnyama huyo kulala njaa kama ambavyo hutokea kwa wanyama wengine wala nyama kama fisi, simba na wengineo.

Kundi dogo la Mbwa mwitu laweza kuvamia kijiji mithili ya "askari wa miavuli" wakateketeza mamia ya mifugo kama kondoo, mbuzi, na ndama kwa kasi ya kutisha na kwa kilio cha wafugaji. Hivyo Mbwa mwitu ni adui mkubwa kwa wafugaji; isitoshe yeye huua mawindo hata asiyoyahitaji mradi tu amepata nafasi ya kufanya mazoezi kudhibitisha ukali wake

Palipo na mizoga mnyama fisi hafi njaa; kawni yeye hujishibisha kwa kile kinachowindwa na kusazwa na Mbwa mwitu. Akitosheka "ataimba" kwa sauti ya juu kana kwamba ndiye mfalme wa mwituni. Ulaji wa fisi ni wa kushangaza kidogo kila akatapo bonge la nyama ya windo na kumeza, hujifuta damu pua na mdomo ardhini kisha huendelea hivyo mpaka ameshiba.

Haifahamiki vyema ni kwa nini mnyama huyo hufanya hivyo, lakini kuna dhana moja isiyothibitishwa kwamba asipojifuta pua na mdomo vikabaki na alama ya damu wakati mzoga umemalizika, Mbwa mwitu wenzake wenye njaa watamshambulia na kumla kama wanyama wengine.

Tabia ya Mbwa mwitu mawindoni inafanana na ile ya majambazi yanayopora mali za raia wema. Wao wanapopora mali kwa lengo la kugawana, hufanya hivyo kwa umoja na nguvu moja; lakini ikitokea kwamba mmoja wao amejinyakulia "kitita" kikubwa zaidi kwa uchu na ujanja kuliko wenzake mara nyingi ugomvi hutokea na wakati mwingine wanauana wao kwa wao.

Iwe kwa Mbwa mwitu kuraruana kwa kukiuka kanuni za ulaji au iwe kwa majambazi kutwangana risasi wakigombea "mzigo"; yote ni sawa tu kwamba kama kuraruana huko au kunyukana risasi kutafanyika mahala karibu na tukio bila ya shaka yoyote, minyukano hiyo itamwamsha mwenye mali kama alikuwa usingizini.

Kujulikana kwa sakata la ufisadi wa fedha za mfuko wa malipo ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu nchini ni matokeo ya Mbwa mwitu au majambazi kunyukana kwa kugombea mawindo, na mwangwi wa minyukano yao umeweza kuuamsha umma wa Kitanzania. Tunadhani vivyo hivyo kwa sakata la Richmond, lakini leo tuzungumzie tu hili la EPA.

Kabla ya EPA wananchi wamekuwa wakisikia kwa mbali tu, kama vile wamo usingizini na kama wako nusu macho kwa maluweluwe, juu ya matendo ya kifisadi hususan lile sakata la mkataba wa IPTL ambapo wananchi wamebebeshwa mzigo wa kulipa deni kwa kampuni la kimataifa , Mechmar la Malaysia – Sh. bilioni 4.6 kwa mwezi kwa miaka 20.

Umma ulikuwa usingizini pia pale wajanja walipovuna mawindo haramu kupitia mkataba wa ununuzi wa ndege ya anasa ya Rais, na chombo cha kijeshi cha kuona mbali (Radar) kisichoweza kumulika nje ya mkoa wa Dar es salaam na Morogoro kwa zaidi. Hiki, kilinunuliwa kwa Sh. zaidi ya bilioni 40.

Aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Uingereza, Clare Short alipiga kelele kutuamsha usingizini - "jamani eeh, Mbwa mwitu yumo chumbani mwenu", lakini hatukuweza kuamka tukaendelea kuuchapa usingizi.

Wenzetu fisi wenye kunyemelea mizoga walijua mapema mawindo ya Mbwa mwitu; yaani kampuni moja ya Uingereza ya BAE inayouza zana za kijeshi na wakala wao hapa nchini, Salleth Vithlani ambaye ametoweka ghafla.

Wenzetu hao walipinga kwa nguvu zote bungeni wakisema Mama Short hakuwa na uhalali wowote wa kuzungumzia biashara hiyo na pale kikosi madhubuti nchini Uingereza cha upelelezi wa makosa ya kugushi, uhujumu na ufisadi (SFO) kilipopiga kelele kusema "Watanzania wanaibiwa", wenzetu hao hao waliionya Uingereza isiingilie mambo ya Tanzania na kwamba Watanzania ni watu huru wasioweza kutishwa na nchi tajiri na kwamba hata kama ni kula nyasi (kwa umaskini wetu) watakula, lakini rada na ndege ya Rais zinunuliwe ima faima.

Licha ya tahadhari ya jumuiya ya kimataifa juu ya ufisadi huu, wenzetu wakatia pamba masikioni na kusema "twende kazini". Rada ikanunuliwa na ndege ya Rais ikaletwa; zote kwa pamoja zikatafuna zaidi ya Sh. bilioni 80.

Katika nchi maskini ya Dunia ya Tatu yenye deni la nje lisilopungua Shilingi trilioni saba linalopaswa kulipwa pamoja na riba, mwenye mali aliendelea kuutandika usingizi.

Mkataba wa IPTL ulipotiwa sahihi pamoja na jumuiya za kimataifa, yakiwamo mashirika ya fedha kama vile WB na IMF, kupinga na kututahadharisha, vigogo wetu waliendelea kula na kufuta pua na midomo mithili ya Mbwa mwitu

Mark Dodd wa Shirika la Habari la Reuters la Uingereza alihoji uhalali wa Mwanasheria Mkuu na Waziri wa Madini na Nishati kutia sahihi mkataba huo ambao IFM iliuelezea kuwa ni "mzigo usiobebeka kwa uchumi wa taifa", alisema "Sakata la IPTL linazua swali ni kwa nini kikundi kidogo cha wasomi nchini kilichokosa uzalendo, ubinadamu na huruma kwa wengine, kiruhusiwe kuwanyonya kikatili wananchi maskini wa kutupwa kwa sababu tu ya maslahi binafsi.

Dodd aliendelea kusema: Viongozi wa Tanzania ni wanyonyaji wakubwa wa Watanzania" (Daily Mail, Julai 15, 1998).

Jambo mbalo hakulielewa Dodd ni kwamba kulikuwa na kundi la Mbwa mwitu wawindaji linaloua hata kile kisilohitaji kwa shibe mradi tu kujivunia ukali wa meno yake. Kundi dogo hili la Watanzania (wasomi) analosema ni kama fisi tu anayefuatilia kujishibisha kwa mizoga ya mawindo ya Mbwa mwitu na kutetea utamaduni huo unaolipatia shibe kwa maangamizi ya viumbe visivyo na hatia.

Kwa mwezi Mei 1995 pekee zaidi ya makala 50 ziliandikwa na magazeti mbalimbali nchini kukosoa mkataba huo; huku magazeti ya serikali ya Daily News na Sunday News yakiukingia kifua mkataba huo wa IPTL licha ya kelele hizo (za wapiti njia ambazo hazikumnyima usingizi mwenye mali)

Ufisadi huo uliendelea kimya kimya kwa sababu tu mafisadi walikula na kufuta pua na midomo kama Mbwa mwitu. Uliendelea kwa sababu wahusika walifahamu kuwa mwenye mali bado anaendelea kuuchapa usingizi.

Mwenye mali aliendelea kuuchapa usingizi pia juu ya mkataba mibovu na yenye kuangamiza taifa kama ile ya madini, ubinafsishaji na uwekezaji usiojali maslahi ya taifa, kwa sababu tu majambazi wa mikataba hiyo hawajakosana wala kufyatuliana risasi kuweza kumwamsha mwenye mali kutoka usingizini.

Yapo mengi ya aina hii, lakini la EPA limekuwa tofauti na mengine kiasi cha mwenye mali kuamka kutoka usingizini kutokana na kelele za mafisadi kugombea kile yalichopora.

Awali ya yote tukiri kwamba sakata hili lina mtandao mkubwa wa kundi la "Mbwa mwitu" ndani na nje ya nchi, mtandao huo ukiongozwa na Jeetu Patel.

Inasemekana, Jayant Kumar Patel, maarufu kwa jina la Jeetu Patel ana mtandao wa kijambazi ambao umedumu kwa miongo minne hapa nchini.

Mtandao huo unawajumuisha pamoja wengi wengineo akiwemo mfanyabiashara mmoja maarufu anayeishi katika kasri lake karibu na Hotel Slipway, jijini Dar es salaam. Anapokuwa Dubai mfanyabiashara huyu huendesha gari la kifahari aina ya Rolls Royce ambako pia anamiliki jumba lenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni saba.

*Itaendelea toleo lijalo

EPA: Minyukano ya mafisadi imemwamsha mwenye mali (2)

Joseph Mihangwa Aprili 9, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Kitendo

MTANDAO wa ufisadi wa EPA unawajumuisha pamoja wafanyabiashara kadhaa akiwemo mmoja maarufu anayeishi katika kasri lake karibu na Hotel Slipway, jijini Dar es salaam.

Wengine katika mtandao huo ni pamoja na Salleth Vithlani, yule wakala wa uuzaji wa rada, vifaa vya kijeshi na ndege ya Rais aliyekuja kutoroka baadaye.

Huyo Bwana anayeishi karibu na Slipway Hotel ndiye anayesimamia mtandao mdogo unaohushisha makampuni kadhaa yaliyochota fedha za EPA. Inadaiwa pia kuwa ana hisa katika Benki M.

Wengine wenye hisa katika benki hiyo inaaminika kuwa ni pamoja na Jeetu Patel (alijitoa baadaye), Daudi Balali, Vima Meha, Sanjeer Kumar, Bhasker Narayan, Anna Muganda na wengineo.

Pia mtandao wa Jeetu Patel unamhusisha mfanyabiashara mmoja aishie nchini Kenya aliyewahi kumiliki Benki tata nchini humo "Delphis Bank"
iliyowahi kuwapora wateja zaidi ya dola milioni 90.

Aliwahi pia kumiliki nchini humo kampuni ya kuuza magari iitwayo "Marshalls Kenya Limited" na kuliuzia Jeshi la Kenya magari kwa mkataba wenye utata kama ilivyotokea hapa nchini kwetu kwa Sailesh Vithlani na Serikali yetu (mauzo ya rada).

Ni mfanyabiashara huyo pia ambaye amewahi kuwapora wateja wa Benki ya "Trust Bank" iliyosimamiwa na BOT chini ya dhamana ya Delphis Bank mwaka 1999, na hadi sasa angali anasakwa na polisi.

Wengine katika mtandao huo ni Bharat Patel, raia wa Uingereza ambaye ni mdogo wake Jeetu Patel anayeishi mjini London mwenye kumiliki kampuni iitwayo Motorsense. Yupo pia mtoto wa Bharat Patel, raia wa Uingereza anayeishi hapa nchini aitwaye Mitul Patel ambaye pia ndiye Mkurugenzi wa baadhi ya makampuni yanayodaiwa kushiriki kuchota fedha za EPA.

Pengine sakata la pesa za EPA lisingejulikana na kulipuka kama mmojawao aitwaye Jitesh Ladwa asingewashambulia na kuwararua wenzake kwa kusahau kufuta pua na midomo yao!

Mapema 2005, Jitesh Ladwa, mfanyabiashara na mdaiwa mkubwa wa vyombo vya fedha hapa nchini, alisambaza ujumbe kwa njia ya E-mail duniani kote kuibua ufisadi uliokithiri BOT. Inasemekana Jitesh alikuwa anadaiwa na EuroAfrican Bank kiasi cha Sh. bilioni moja, IFC Sh. bilioni 7 na Barclays Bank Sh. bilioni 2.5, ambapo hoteli za Golden Tulip na Karibu Hotel zilikuwa chini ya rehani.

Hapo Machi 7, 2005 Jitesh Ladwa aliomba mkopo kutoka BOT kwa ajili ya kupanua Hoteli yake iitwayo Indian Ocean Hotels kwa lengo la kuvutia watalii nchini. Ombi lake lilikataliwa na BOT kwa barua ya Septemba 1, 2005 kwa maelezo mafupi tu kwamba Benki hiyo haikuwa na uwezo wa kushughulikia ombi lake.

Kabla ya hapo, Jitesh alikuwa "mteja mzuri" na mahiri wa EPA na alinufaika kwa kiasi kikubwa yeye na "Mbwa mwitu" wengine. Sababu kubwa ya kukataliwa kwa maombi ya Jitesh ni utata wa baadhi ya hati alizowasilisha Benki kwa kudhaniwa kwamba hazikuwa halisi.

Kunyimwa mkopo kwa Jitesh kulizua vita kali kati yake na uongozi wa BOT, chini ya Daudi Ballali, pamoja na wafanyabiashara wenzake (Mbwa mwitu) wenye asili ya Kiasia na akaanza kuanika nje uozo ndani ya Benki na sakata zima la pesa za EPA ambazo yeye alikuwa mnufaika pia.

Jitesh alimshambulia pia Jeetu Patel kwa kushindwa kumwokoa alipowasilisha kwake ombi la mkopo binafsi kufuatia BOT kumwekea ngumu.

Inasemekana baada ya kugonga mwamba BoT na kwa Jeetu Patel, Jitesh Ladwa alimwendea mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ambaye aliweza kumpatia mkopo aliotaka. Inadhaniwa pia kuwa, pengine ni kwa sababu ya kumsaidia Jitesh, kwamba Rostam Aziz hakutajwa katika E-mails alizosambaza Jitesh duniani pamoja na kuwa mbunge huyo naye alinufaika na pesa za EPA.

Kuokolewa kwa Jitesh na Rostam Aziz kulijenga kambi mbili za "Mbwa mwitu" katika ufisadi wa EPA, kati ya kundi la wafanyabiashara "wapendwa" walioendelea kunufaika na BOT na kundi la "walioteuliwa" likiongozwa na Jitesh ambalo liliapa kuwalipua wale wa kundi la "wapendwa" isipokuwa Rostam Aziz kwa sababu ya umaarufu wake.

Ukweli ni kuwa, ilifika mahali kulikuwa na Serikali mbili ndani ya Serikali ya Tanzania, yaani Serikali halali chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na "Serikali nyingine" chini ya wafanyabiashara hao wakiongozwa na Rostam Aziz.

"Serikali" hiyo ya wafanyabiashara ilionekana kuwa na nguvu kuliko ya Rais Kikwete kwa sababu (iliundwa na wafanyabiashara wakubwa matajiri) na ilikuwa na pesa zilizotakiwa na wanasiasa.

Inadhaniwa kwamba ni "Serikali" hii ya pili (ya Rostam Aziz) iliyohamasisha wafanyabiashara wa Kitanzania wenye asili ya Kiasia kupigania nafasi za kisiasa ili kupata habari toka ndani ya Serikali ya namna ya kutoa ushawishi jinsi ya kufikiwa maamuzi yaliyopendelea tabaka la wafanyabiashara, ubepari wa kimataifa na kikundi kidogo cha watawala waliotekwa nyara na ubepari huo.

Kwa hili, kwa nini umma usiamini unapoona kwamba mafisadi hawakamatiki ambapo Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act), Sheria ya Udhahidi (Evidence Act) na Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) zimesitishwa dhidi ya mafisadi ili waonekane kama wadaiwa wa kawaida chini ya Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai (Civil Procedure Act), tena bila kutozwa riba?

Kwa nini umma usiamini hivyo unapoona kwamba fedha za ufisadi zinarejeshwa na mizuka (ghosts) isiyoonekana, lakini Serikali inakiri kuzipokea kutoka kwa "watu" ("serikali ya pili") wasiojulikana?
Je, zinatupwa na kuokotwa barabarani?

Ajabu, yote haya yanatendeka mbele ya Tume iliyoundwa na Rais, ikijumuisha Mwanasheria Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, na Mkuu wa TAKUKURU ambao wote ni wanasheria kwa taaluma.

Sakata la EPA ndani ya BoT liliibuka kutokana na Mbwa mwitu kuraruana wao kwa wao kiasi kwamba minyukano yao iliwaamsha wananchi wenye mali kutoka usingizini na kujionea jinsi wanavyoporwa mali zao.

Rais Kikwete aliunda Tume kuchunguza uporaji huo baada ya umma kupiga yowe muda mrefu kuwa unaibiwa. Ukichunguza kwa makini huwezi kushindwa kubaini kuwa wale wanaounda Tume, baadhi yao ni wale wale wanaonufaika na mizoga iliyoachwa na Mbwa mwitu wawindaji. Je, fisi anaweza kumhukumu mbweha anayempa chakula? Ili iweje na akale wapi?

Na kwa kuwa umma wa Kitanzania umeamshwa na minyukano ya mbweha mafisadi na kukuta umeporwa mali zake kwa muda mrefu kabla ya hapo, je kuna sababu gani kunyamazia uporaji wa kale iwapo ushahidi upo? Kwa nini Rais asiunde Tume kama ile ya EPA kufuatilia uporaji wa kale?

Tuna Serikali ya wananchi moja tu ambayo tumeambiwa haina ubia na mtu au kikundi chochote cha watu katika kuongoza nchi. Kama hivyo ndivyo, hatutarajii kuona "Serikali" ya kikundi cha mafisadi walio juu ya dhana ya utawala wa sheria wanaoweza kupora na kuyeyuka "kimiujiza" wasiweze kuguswa na mkondo wa sheria.

Inapokuwa hivyo, umma hauwezi kujizuia kuamini kwamba baadhi ya viongozi wetu wananufaika na mizoga inayotemwa na kundi la mbwa mwitu wawindaji ndani ya nchi yao.
0713-526972
 
EPA: Minyukano ya mafisadi imemwamsha mwenye mali (1)

Joseph Mihangwa Aprili 2, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Kitendo

MBWA mwitu ni mnyama mwindaji hatari kwa wanyama wadogo wadogo porini. Silaha zake ni mbio, meno makali mithili ya kisu chenye ncha kali na ujanja wa porini. Kwa sababu hii ni nadra kwa mnyama huyo kulala njaa kama ambavyo hutokea kwa wanyama wengine wala nyama kama fisi, simba na wengineo.

Kundi dogo la Mbwa mwitu laweza kuvamia kijiji mithili ya “askari wa miavuli” wakateketeza mamia ya mifugo kama kondoo, mbuzi, na ndama kwa kasi ya kutisha na kwa kilio cha wafugaji. Hivyo Mbwa mwitu ni adui mkubwa kwa wafugaji; isitoshe yeye huua mawindo hata asiyoyahitaji mradi tu amepata nafasi ya kufanya mazoezi kudhibitisha ukali wake

Palipo na mizoga mnyama fisi hafi njaa; kawni yeye hujishibisha kwa kile kinachowindwa na kusazwa na Mbwa mwitu. Akitosheka “ataimba” kwa sauti ya juu kana kwamba ndiye mfalme wa mwituni. Ulaji wa fisi ni wa kushangaza kidogo kila akatapo bonge la nyama ya windo na kumeza, hujifuta damu pua na mdomo ardhini kisha huendelea hivyo mpaka ameshiba.

Haifahamiki vyema ni kwa nini mnyama huyo hufanya hivyo, lakini kuna dhana moja isiyothibitishwa kwamba asipojifuta pua na mdomo vikabaki na alama ya damu wakati mzoga umemalizika, Mbwa mwitu wenzake wenye njaa watamshambulia na kumla kama wanyama wengine.

Tabia ya Mbwa mwitu mawindoni inafanana na ile ya majambazi yanayopora mali za raia wema. Wao wanapopora mali kwa lengo la kugawana, hufanya hivyo kwa umoja na nguvu moja; lakini ikitokea kwamba mmoja wao amejinyakulia “kitita” kikubwa zaidi kwa uchu na ujanja kuliko wenzake mara nyingi ugomvi hutokea na wakati mwingine wanauana wao kwa wao.

Iwe kwa Mbwa mwitu kuraruana kwa kukiuka kanuni za ulaji au iwe kwa majambazi kutwangana risasi wakigombea “mzigo”; yote ni sawa tu kwamba kama kuraruana huko au kunyukana risasi kutafanyika mahala karibu na tukio bila ya shaka yoyote, minyukano hiyo itamwamsha mwenye mali kama alikuwa usingizini.

Kujulikana kwa sakata la ufisadi wa fedha za mfuko wa malipo ya nje (EPA) ndani ya Benki Kuu nchini ni matokeo ya Mbwa mwitu au majambazi kunyukana kwa kugombea mawindo, na mwangwi wa minyukano yao umeweza kuuamsha umma wa Kitanzania. Tunadhani vivyo hivyo kwa sakata la Richmond, lakini leo tuzungumzie tu hili la EPA.

Kabla ya EPA wananchi wamekuwa wakisikia kwa mbali tu, kama vile wamo usingizini na kama wako nusu macho kwa maluweluwe, juu ya matendo ya kifisadi hususan lile sakata la mkataba wa IPTL ambapo wananchi wamebebeshwa mzigo wa kulipa deni kwa kampuni la kimataifa , Mechmar la Malaysia – Sh. bilioni 4.6 kwa mwezi kwa miaka 20.

Umma ulikuwa usingizini pia pale wajanja walipovuna mawindo haramu kupitia mkataba wa ununuzi wa ndege ya anasa ya Rais, na chombo cha kijeshi cha kuona mbali (Radar) kisichoweza kumulika nje ya mkoa wa Dar es salaam na Morogoro kwa zaidi. Hiki, kilinunuliwa kwa Sh. zaidi ya bilioni 40.

Aliyekuwa Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Uingereza, Clare Short alipiga kelele kutuamsha usingizini - “jamani eeh, Mbwa mwitu yumo chumbani mwenu”, lakini hatukuweza kuamka tukaendelea kuuchapa usingizi.

Wenzetu fisi wenye kunyemelea mizoga walijua mapema mawindo ya Mbwa mwitu; yaani kampuni moja ya Uingereza ya BAE inayouza zana za kijeshi na wakala wao hapa nchini, Salleth Vithlani ambaye ametoweka ghafla.

Wenzetu hao walipinga kwa nguvu zote bungeni wakisema Mama Short hakuwa na uhalali wowote wa kuzungumzia biashara hiyo na pale kikosi madhubuti nchini Uingereza cha upelelezi wa makosa ya kugushi, uhujumu na ufisadi (SFO) kilipopiga kelele kusema “Watanzania wanaibiwa”, wenzetu hao hao waliionya Uingereza isiingilie mambo ya Tanzania na kwamba Watanzania ni watu huru wasioweza kutishwa na nchi tajiri na kwamba hata kama ni kula nyasi (kwa umaskini wetu) watakula, lakini rada na ndege ya Rais zinunuliwe ima faima.

Licha ya tahadhari ya jumuiya ya kimataifa juu ya ufisadi huu, wenzetu wakatia pamba masikioni na kusema “twende kazini”. Rada ikanunuliwa na ndege ya Rais ikaletwa; zote kwa pamoja zikatafuna zaidi ya Sh. bilioni 80.

Katika nchi maskini ya Dunia ya Tatu yenye deni la nje lisilopungua Shilingi trilioni saba linalopaswa kulipwa pamoja na riba, mwenye mali aliendelea kuutandika usingizi.

Mkataba wa IPTL ulipotiwa sahihi pamoja na jumuiya za kimataifa, yakiwamo mashirika ya fedha kama vile WB na IMF, kupinga na kututahadharisha, vigogo wetu waliendelea kula na kufuta pua na midomo mithili ya Mbwa mwitu

Mark Dodd wa Shirika la Habari la Reuters la Uingereza alihoji uhalali wa Mwanasheria Mkuu na Waziri wa Madini na Nishati kutia sahihi mkataba huo ambao IFM iliuelezea kuwa ni “mzigo usiobebeka kwa uchumi wa taifa”, alisema “Sakata la IPTL linazua swali ni kwa nini kikundi kidogo cha wasomi nchini kilichokosa uzalendo, ubinadamu na huruma kwa wengine, kiruhusiwe kuwanyonya kikatili wananchi maskini wa kutupwa kwa sababu tu ya maslahi binafsi.

Dodd aliendelea kusema: Viongozi wa Tanzania ni wanyonyaji wakubwa wa Watanzania” (Daily Mail, Julai 15, 1998).

Jambo mbalo hakulielewa Dodd ni kwamba kulikuwa na kundi la Mbwa mwitu wawindaji linaloua hata kile kisilohitaji kwa shibe mradi tu kujivunia ukali wa meno yake. Kundi dogo hili la Watanzania (wasomi) analosema ni kama fisi tu anayefuatilia kujishibisha kwa mizoga ya mawindo ya Mbwa mwitu na kutetea utamaduni huo unaolipatia shibe kwa maangamizi ya viumbe visivyo na hatia.

Kwa mwezi Mei 1995 pekee zaidi ya makala 50 ziliandikwa na magazeti mbalimbali nchini kukosoa mkataba huo; huku magazeti ya serikali ya Daily News na Sunday News yakiukingia kifua mkataba huo wa IPTL licha ya kelele hizo (za wapiti njia ambazo hazikumnyima usingizi mwenye mali)

Ufisadi huo uliendelea kimya kimya kwa sababu tu mafisadi walikula na kufuta pua na midomo kama Mbwa mwitu. Uliendelea kwa sababu wahusika walifahamu kuwa mwenye mali bado anaendelea kuuchapa usingizi.

Mwenye mali aliendelea kuuchapa usingizi pia juu ya mkataba mibovu na yenye kuangamiza taifa kama ile ya madini, ubinafsishaji na uwekezaji usiojali maslahi ya taifa, kwa sababu tu majambazi wa mikataba hiyo hawajakosana wala kufyatuliana risasi kuweza kumwamsha mwenye mali kutoka usingizini.

Yapo mengi ya aina hii, lakini la EPA limekuwa tofauti na mengine kiasi cha mwenye mali kuamka kutoka usingizini kutokana na kelele za mafisadi kugombea kile yalichopora.

Awali ya yote tukiri kwamba sakata hili lina mtandao mkubwa wa kundi la “Mbwa mwitu” ndani na nje ya nchi, mtandao huo ukiongozwa na Jeetu Patel.

Inasemekana, Jayant Kumar Patel, maarufu kwa jina la Jeetu Patel ana mtandao wa kijambazi ambao umedumu kwa miongo minne hapa nchini.

Mtandao huo unawajumuisha pamoja wengi wengineo akiwemo mfanyabiashara mmoja maarufu anayeishi katika kasri lake karibu na Hotel Slipway, jijini Dar es salaam. Anapokuwa Dubai mfanyabiashara huyu huendesha gari la kifahari aina ya Rolls Royce ambako pia anamiliki jumba lenye thamani ya zaidi ya Shilingi bilioni saba.

*Itaendelea toleo lijalo

EPA: Minyukano ya mafisadi imemwamsha mwenye mali (2)

Joseph Mihangwa Aprili 9, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Kitendo

MTANDAO wa ufisadi wa EPA unawajumuisha pamoja wafanyabiashara kadhaa akiwemo mmoja maarufu anayeishi katika kasri lake karibu na Hotel Slipway, jijini Dar es salaam.

Wengine katika mtandao huo ni pamoja na Salleth Vithlani, yule wakala wa uuzaji wa rada, vifaa vya kijeshi na ndege ya Rais aliyekuja kutoroka baadaye.

Huyo Bwana anayeishi karibu na Slipway Hotel ndiye anayesimamia mtandao mdogo unaohushisha makampuni kadhaa yaliyochota fedha za EPA. Inadaiwa pia kuwa ana hisa katika Benki M.

Wengine wenye hisa katika benki hiyo inaaminika kuwa ni pamoja na Jeetu Patel (alijitoa baadaye), Daudi Balali, Vima Meha, Sanjeer Kumar, Bhasker Narayan, Anna Muganda na wengineo.

Pia mtandao wa Jeetu Patel unamhusisha mfanyabiashara mmoja aishie nchini Kenya aliyewahi kumiliki Benki tata nchini humo “Delphis Bank”
iliyowahi kuwapora wateja zaidi ya dola milioni 90.

Aliwahi pia kumiliki nchini humo kampuni ya kuuza magari iitwayo “Marshalls Kenya Limited” na kuliuzia Jeshi la Kenya magari kwa mkataba wenye utata kama ilivyotokea hapa nchini kwetu kwa Sailesh Vithlani na Serikali yetu (mauzo ya rada).

Ni mfanyabiashara huyo pia ambaye amewahi kuwapora wateja wa Benki ya “Trust Bank” iliyosimamiwa na BOT chini ya dhamana ya Delphis Bank mwaka 1999, na hadi sasa angali anasakwa na polisi.

Wengine katika mtandao huo ni Bharat Patel, raia wa Uingereza ambaye ni mdogo wake Jeetu Patel anayeishi mjini London mwenye kumiliki kampuni iitwayo Motorsense. Yupo pia mtoto wa Bharat Patel, raia wa Uingereza anayeishi hapa nchini aitwaye Mitul Patel ambaye pia ndiye Mkurugenzi wa baadhi ya makampuni yanayodaiwa kushiriki kuchota fedha za EPA.

Pengine sakata la pesa za EPA lisingejulikana na kulipuka kama mmojawao aitwaye Jitesh Ladwa asingewashambulia na kuwararua wenzake kwa kusahau kufuta pua na midomo yao!

Mapema 2005, Jitesh Ladwa, mfanyabiashara na mdaiwa mkubwa wa vyombo vya fedha hapa nchini, alisambaza ujumbe kwa njia ya E-mail duniani kote kuibua ufisadi uliokithiri BOT. Inasemekana Jitesh alikuwa anadaiwa na EuroAfrican Bank kiasi cha Sh. bilioni moja, IFC Sh. bilioni 7 na Barclays Bank Sh. bilioni 2.5, ambapo hoteli za Golden Tulip na Karibu Hotel zilikuwa chini ya rehani.

Hapo Machi 7, 2005 Jitesh Ladwa aliomba mkopo kutoka BOT kwa ajili ya kupanua Hoteli yake iitwayo Indian Ocean Hotels kwa lengo la kuvutia watalii nchini. Ombi lake lilikataliwa na BOT kwa barua ya Septemba 1, 2005 kwa maelezo mafupi tu kwamba Benki hiyo haikuwa na uwezo wa kushughulikia ombi lake.

Kabla ya hapo, Jitesh alikuwa “mteja mzuri” na mahiri wa EPA na alinufaika kwa kiasi kikubwa yeye na “Mbwa mwitu” wengine. Sababu kubwa ya kukataliwa kwa maombi ya Jitesh ni utata wa baadhi ya hati alizowasilisha Benki kwa kudhaniwa kwamba hazikuwa halisi.

Kunyimwa mkopo kwa Jitesh kulizua vita kali kati yake na uongozi wa BOT, chini ya Daudi Ballali, pamoja na wafanyabiashara wenzake (Mbwa mwitu) wenye asili ya Kiasia na akaanza kuanika nje uozo ndani ya Benki na sakata zima la pesa za EPA ambazo yeye alikuwa mnufaika pia.

Jitesh alimshambulia pia Jeetu Patel kwa kushindwa kumwokoa alipowasilisha kwake ombi la mkopo binafsi kufuatia BOT kumwekea ngumu.

Inasemekana baada ya kugonga mwamba BoT na kwa Jeetu Patel, Jitesh Ladwa alimwendea mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ambaye aliweza kumpatia mkopo aliotaka. Inadhaniwa pia kuwa, pengine ni kwa sababu ya kumsaidia Jitesh, kwamba Rostam Aziz hakutajwa katika E-mails alizosambaza Jitesh duniani pamoja na kuwa mbunge huyo naye alinufaika na pesa za EPA.

Kuokolewa kwa Jitesh na Rostam Aziz kulijenga kambi mbili za “Mbwa mwitu” katika ufisadi wa EPA, kati ya kundi la wafanyabiashara “wapendwa” walioendelea kunufaika na BOT na kundi la “walioteuliwa” likiongozwa na Jitesh ambalo liliapa kuwalipua wale wa kundi la “wapendwa” isipokuwa Rostam Aziz kwa sababu ya umaarufu wake.

Ukweli ni kuwa, ilifika mahali kulikuwa na Serikali mbili ndani ya Serikali ya Tanzania, yaani Serikali halali chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na “Serikali nyingine” chini ya wafanyabiashara hao wakiongozwa na Rostam Aziz.

“Serikali” hiyo ya wafanyabiashara ilionekana kuwa na nguvu kuliko ya Rais Kikwete kwa sababu (iliundwa na wafanyabiashara wakubwa matajiri) na ilikuwa na pesa zilizotakiwa na wanasiasa.

Inadhaniwa kwamba ni “Serikali” hii ya pili (ya Rostam Aziz) iliyohamasisha wafanyabiashara wa Kitanzania wenye asili ya Kiasia kupigania nafasi za kisiasa ili kupata habari toka ndani ya Serikali ya namna ya kutoa ushawishi jinsi ya kufikiwa maamuzi yaliyopendelea tabaka la wafanyabiashara, ubepari wa kimataifa na kikundi kidogo cha watawala waliotekwa nyara na ubepari huo.

Kwa hili, kwa nini umma usiamini unapoona kwamba mafisadi hawakamatiki ambapo Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act), Sheria ya Udhahidi (Evidence Act) na Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Penal Code) zimesitishwa dhidi ya mafisadi ili waonekane kama wadaiwa wa kawaida chini ya Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai (Civil Procedure Act), tena bila kutozwa riba?

Kwa nini umma usiamini hivyo unapoona kwamba fedha za ufisadi zinarejeshwa na mizuka (ghosts) isiyoonekana, lakini Serikali inakiri kuzipokea kutoka kwa “watu” (“serikali ya pili”) wasiojulikana?
Je, zinatupwa na kuokotwa barabarani?

Ajabu, yote haya yanatendeka mbele ya Tume iliyoundwa na Rais, ikijumuisha Mwanasheria Mkuu, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, na Mkuu wa TAKUKURU ambao wote ni wanasheria kwa taaluma.

Sakata la EPA ndani ya BoT liliibuka kutokana na Mbwa mwitu kuraruana wao kwa wao kiasi kwamba minyukano yao iliwaamsha wananchi wenye mali kutoka usingizini na kujionea jinsi wanavyoporwa mali zao.

Rais Kikwete aliunda Tume kuchunguza uporaji huo baada ya umma kupiga yowe muda mrefu kuwa unaibiwa. Ukichunguza kwa makini huwezi kushindwa kubaini kuwa wale wanaounda Tume, baadhi yao ni wale wale wanaonufaika na mizoga iliyoachwa na Mbwa mwitu wawindaji. Je, fisi anaweza kumhukumu mbweha anayempa chakula? Ili iweje na akale wapi?

Na kwa kuwa umma wa Kitanzania umeamshwa na minyukano ya mbweha mafisadi na kukuta umeporwa mali zake kwa muda mrefu kabla ya hapo, je kuna sababu gani kunyamazia uporaji wa kale iwapo ushahidi upo? Kwa nini Rais asiunde Tume kama ile ya EPA kufuatilia uporaji wa kale?

Tuna Serikali ya wananchi moja tu ambayo tumeambiwa haina ubia na mtu au kikundi chochote cha watu katika kuongoza nchi. Kama hivyo ndivyo, hatutarajii kuona “Serikali” ya kikundi cha mafisadi walio juu ya dhana ya utawala wa sheria wanaoweza kupora na kuyeyuka “kimiujiza” wasiweze kuguswa na mkondo wa sheria.

Inapokuwa hivyo, umma hauwezi kujizuia kuamini kwamba baadhi ya viongozi wetu wananufaika na mizoga inayotemwa na kundi la mbwa mwitu wawindaji ndani ya nchi yao.
0713-526972

Hii nchi inaliwa na wenye meno ...... Narudia tena kutoa wito kwa Kikwete afute safari za nje na arudi Tanzania kushughulikia haya yote kabla hajachelewa!
 
sawa viongozi tugeuzeni mnavyotaka,hata huku nyuma ikibidi, ila iko siku ninyi viongozi mtaihama hii inchi kwa uta au kwa nchale, endeleeni kuwaaelimisha watoto wenu ili waje watutawale, ila muda utawahukumu tu.
 
Kijana wa Mwita naona una hasira sana! yana mwisho tu haya na muda mwingine mwisho unakuja mapema sana kuliko kawaida!
 
sawa viongozi tugeuzeni mnavyotaka,hata huku nyuma ikibidi, ila iko siku ninyi viongozi mtaihama hii inchi kwa uta au kwa nchale, endeleeni kuwaaelimisha watoto wenu ili waje watutawale, ila muda utawahukumu tu.

Nakubaliana na wewe partly au totaly kwa kutumia mfano mwingine, Mimi kugeuzwa No. What goes around comes around.
 
Back
Top Bottom