John Mnyika
JF-Expert Member
- Jun 16, 2006
- 712
- 1,239
Huko ulaya, vuguvugu la wanaharakati linazidi kupamba moto kupinga EU na serikali zao kuingia makubaliano na nchi zinazoitwa masikini chini ya EPA. Huku Afrika na hata kwetu Tanzania mjadala unakwenda kimya kimya. Pamoja na kuwa na kundi la NSA wakiwa na ufadhili wa kutosha wa harakati hizi bado sauti ya wasio na sauti haisikiki kuhusu masuala haya. Huku serikali yetu ikisema kwamba hatutasaini mpaka baada ya mwezi mmoja; huku serikali tayari imeshaini hatua zote za msingi chini ya EAC. Swali la kujiuliza. EPA ipi namna ya kukwepa kunyonywa? Ipi namna ya kuepuka kuendelea kuwa soko holela. Ipi namna ya kuepuka kuendelea kuviza uzalishaji wa ndani? Zipi ni fikra mbadala kuhusu EPA? Tujadili!
JJ
JJ