Enzi zetu: Mpenzi wangu nikupendaye kwa dhati

Dhaaaaaa!!! Ebana eeeh
Mako n pale barua inafunguliwa mbele ya kadamnas af mwl kama anataka kuanza kuisoma hv

Nlikua kidogo nizime aisee
Bahat nzur haikusomwa

Siwema weee popote
Ulipo salam zkufkie


Barua yako ya mwisho nakumbuka uliniwekea na
Dedication ya ray c

Uko wap nikuone,,,,,,
 
Enzi zetu bhana, daaah sie kitaa tulikua hadi na nguli wa haya masuala, yaani kila mtu alikua anamfuata Rashid amuandikie barua ya mapenzi, Rashid alikua hatari hatari ana maneno mazuri sanaa af ana muandiko mzuriii, anyway nlipata simu when i was 14 nikakosaga hata wa kuwapigia au kuwatumia meseji yaani nlikuaga kama Lil Romeo flani iv, ila mwisho wa siku ni barua tu simu haina maana.
 
Hahahahhahaha, hatari sana..!! Nilikua na Counter book quire 3 nilikua nimeijaza mistari ya haja, lyrics za nyimbo..Nilikua nalitunza kuliko kitu choochote..!!

Lilinisaidia sana kuwa na mistari ya kuwang'oa warembo..!!
Kipindi hiko, nilikuwa ni CHIZI MAGAZETI...

Ili mradi tu nipate kurasa yenye nyimbo ya UMOMBO, nichane/nichonge vizuri na WEMBE na kuhifadhi kipande.

Lengo likiwa ni kukariri na kung'olea WAREMBO...

Zamani vijana tulikuwa more talented katika kuyaingia MAHUSIANO...

Kwa sasa ni PESA YAKO TU...
 
Sorry kwa kukukosoa, ila walioandika barua shallow hivi wengi walipata IV na O.

Barua ya kiswahili kitupu hivi? Sekondari? mh sijui...

labda mimi nilisoma mjini sana aisee. Sawa basi, lakini hata katerminology kamoja ka Biology ama kemia kweli? Sekondari?

Hapana aisee...hata hiyo introduction iko very shallow huyo mpenzi mlipomaliza shule ni lazima alikuacha tu! Barua haina uchangamfu, haina ubunifu...

Mh sijui labda ni mimi tu nimeona shida na hii barua lakini hii si barua ya kijana barobaro wa sekondari ndugu yangu.

Naomba samahani tena kwa kukukosoa!
 
Mi nilikuwa nasoma madongo kuporomoka huko, sina hili na hili kumbe DSM ngoma iliokuwa inahit ni NIWE NA WEWE MILELE ya Ray C.

Sa nikatumiwa barua na mtoto wa tuit mwanafunzi wa Kisutu. Nikaisoma afu nikapuuzia, coz hata wimbo wenyewe sikuwa naujua.

Sa kurudi likizo si ndio kuiskia ile ngoma! Eeeeh bana Eeeh. Kiuno bila mfupa.

Daah. Nikaanza kwenda race kwa yule bint. Daaah. Zamani.
 
Hahahaaa,uko wapi Bertha wangu,nakumbuka baada ya kuonana na wewe Iringa Girls wakati wa likizo,nilijitahidi sana kuitafuta chance ya kuongea nawe,ilikuwa ukitetemeka sana japo tulikuwa tumekaa na rafiki yako Agnes,baada ya mazungumzo marefu tuliishia kuagana,wakati tunaagana kila mmoja wetu mikono yake ilikuwa imelowa jasho,(sijui kwanini).

Nikiwa safarini kurudi shule,(Minaki high school) akili yangu yote ilikuwa ilikuwa inawaza Bertha,Bertha Bertha tuuu!!!
Nilipofika shule nikaandika boonge la barua,na dedications za kutosha kama,

1.Show me the meaning the meaning of being lonely.......Backstreet boys
2.Love you more that..,..

Baada ya wiki mbili nikapokea barua ya mrejesho chanya,hahahaaa,nahisi ilichangia mimi kupata div.three aisee,maana asilimia kubwa ya muda wangu nlikuwa nawaza nkikutana Bertha itakuwaje,nikapunguza kazi ya kukoboa PCB.

Bertha na EGM yake akapata div.2,mtu mzima na li-PCB language nikaandika division 3.
Naomba ujinga ule usijirudie kwa wanangu kwa kweli!!!!
 
Hahahhaha jaman niseme tu wazi vijana wa zaman mlikua wazembe jaman na ofu yangu wengi wenu adi sasa mtakua bado ni wazembe duh!.........

Mlikua na shida ata ivo hahahah polen sana
 
Hapo unaulizia jibu lako wiki mbili unaambiwa subiri kumbe mdada wa watu yupo anatafuta lyrics za ngoma atupie zaman raha sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom