Enzi zetu: Mpenzi wangu nikupendaye kwa dhati

Basi unaonyesha ulikuwa mtukutu
Enzi hizo walipewa mamlaka ya kutucharaza fimbo halafu mimi na fimbo ni maji & moto! hata nikiona anachapwa mwingine hasira zinanijaa kama koboko! Nikipiga kelele naandikwa ila nikigundua nitafanya kila njia Yale majina yasimfikie ticha, class kulikuwa uwanja wa vita
 
Barua yangu ilishawahi kufikia mikononi mwa mama mkwe, demu kaisoma kisha kaificha kwenye daftari, kufika home mama kamwambia lete daftati nikague, mbaya zaidi mama ananifahamu na kwenye barua nimeandika jina langu, kilichofuata demu alikula bakora za kutosha kisha akaletwa home na kidhibiti mkononi, sitaisahau siku hiyo, ila baada ya siku2 demu kaja mwenyewe geto kumaliza hasira za kupigwa huku akisema"nifanye unavyotaka ili nimalize machungu ya kupigwa".
dahhh!
 
Du mm enz hy nyimbo ya mb dog inatoka ya Latifa nipo moshi kipindi hch kuna dem alikua anasoma shule nyingine rafiki yake tunasoma nae siku akaja nae kwny graduu shulen kwt enz nilikua kdg mjanjamjanja siunajua ukiwa mjanja lzm madem wakushibokee akawa amenielewa yule dem aliniandikia huo wimbo mzima kwny barua mwsh akanambia mm Amina unaambiwa barua niitunza mby na dem kila jmos nilikua lzm nile
 
enzi hizo walipewa mamlaka ya kutucharaza fimbo halafu mimi na fimbo ni maji & moto! hata nikiona anachapwa mwingine hasira zinanijaa kama koboko! nikipiga kelele naandikwa ila nikigundua nitafanya kila njia Yale majina yasimfikie ticha, class kulikuwa uwanja wa vita
Ndiyo maana.
 
Du mm enz hy nyimbo ya mb dog inatoka ya Latifa nipo moshi kipindi hch kuna dem alikua anasoma shule nyingine rafiki yake tunasoma nae siku akaja nae kwny graduu shulen kwt enz nilikua kdg mjanjamjanja siunajua ukiwa mjanja lzm madem wakushibokee akawa amenielewa yule dem aliniandikia huo wimbo mzima kwny barua mwsh akanambia mm Amina unaambiwa barua niitunza mby na dem kila jmos nilikua lzm nile
Hahaha! Hongera sana Mkuu. Ila unatakiwa umtafute sasa umuoe maana nikizihesabu hizo jumamosi kwa mwaka mzima ni kama ulioa bila kutoa mahari
 
Wasichana wengi wakipigwa na wazazi kwa ajili ya mtu fulani ambaye ni mpenzi wake, ujue ndo umemchochea azidi kumpenda jamaa tena ndo anampelekea yt.

Aaa basi mie tofauti.. nilikua nawakwepa hatari na hvyo nilitishiwaga mwanaume akikugusa tu hata mkono unapata mimba..weee pata picha!!! ila nikaishia kua tom boy mpk nilivyokua nikaacha
 
aaa basi mie tofauti.. nilikua nawakwepa hatari na hvyo nilitishiwaga mwanaume akikugusa tu hata mkono unapata mimba..weee pata picha!!! ila nikaishia kua tom boy mpk nilivyokua nikaacha
Ulikuwa bado hujaonjeshwa dyudyu, binti aliyeonjeshwa mara nyingi huwa haelewi chochote, huyu bint wakati namchombeza alikuwa anaenda kunishtaki kwa mama yake, ila nilivyokata utepe ikawa yupo tayari muda wwt hata ukimwambia usiende shule tukutane sehemu, yupo tayari. Hata mida mingine ile alfajr anawahi kuamka anaondoka kama anaenda shule anapita geto anapata ki1 ndo anakwenda shule.
 
ENZI ZETU

Mpenzi wangu nikupendaye kwa dhati.

Salamu nyingi sana zikufikie huko ulipo. Utakapo kujua khali yangu mie ni bukheri kabisa. Hofu na mashaka ni juu yako ewe mpenzi wangu uliye mbali na upeo wa macho yangu.

Dhumuni la barua yangu ni kutaka kukusabahi na kukushukuru kwa barua yako niliyoipata leo mchana. Ahsante sana kwa barua yenye maneno matamu kweli mpenzi wangu. Ama hakika moyo wangu ulijawa shauku kubwa niliposikia jina langu likiitwa pale assemble wakati barua zikigawiwa. Wajua ni namna gani nakupenda ewe kidani cha moyo wangu, chakula cha ubongo wangu, na tulizo la nafsi yangu.

Umeniambia kuwa shuleni kwenu huwa wanafungua barua wakiona ina mwandiko wa kiume. Safari hii nitamwomba monitress wetu aniandikie juu ya bahasha ili nisikuponze mpenzi wangu ukafukuzwa shule. Najua jinsi baba yako alivyo mkali mithili ya mbogo asije akakuchapa bure kishtobe wangu nikupendaye kiasi cha kukosa usingizi kwa ajili yako hadi naiona taswira yako kwenye bilauri ninywapo maji.

Mwezi ujao shule yetu itakuja shuleni kwenu kwenye debate. Ingawa mimi sijui mambo hayo ya debate nitafanya mchongo na msela wangu kiongozi wa debate aniandike jina ili nami nije. Nimekukumbuka sana. Nakumbuka wakati wa likizo tulivyokuwa tunakaa juu ya jiwe lile pembeni ya mto huku nikivichezea vidole vyako nawe ukiniimbia nyimbo za taratibu. Yaani sauti yako ni tamu utadhani kinanda. Kila siku huwa naisikia sauti yako ikiniimbia kwa mahaba ya dhati.

Nisikuchoshe kwa barua ndefu mpenzi wangu. Ila fahamu kuwa mwenzio juu yako sina hali. Nakupenda hadi nimepitiliza maana yenyewe ya neno kupenda. Daima umo mawazoni mwangu.

Msalimie sana yule rafiki yako uliyekuwa naye siku ile. Kuna rafiki yangu anampenda sana. Nitakuja naye kwenye debate.

Ndimi nikupendaye daima,
Mahabuba wako.

HD Wako peke yako

UJUMBE:
If you love three, you are not free,
If you love two, you are not true,
Love only one, that one is ME.

DEDICATION:
(1) Always Be My Baby - by Mariah Carey
(2) I Swear - by All 4 One.

#Zamani_raha_sana
 
Hahahahhahaha, hatari sana..!! Nilikua na Counter book quire 3 nilikua nimeijaza mistari ya haja, lyrics za nyimbo..Nilikua nalitunza kuliko kitu choochote..!!

Lilinisaidia sana kuwa na mistari ya kuwang'oa warembo..!!
enzi zetu izo mkuu
 
Wa ushuani mnaonekana tu!
Watoto wadogo mnawajua hata akina mariah Carey wakati si huku kwetu dedication ilikuwa RayC- uko wapi au afande sele -mkuki moyoni(ingawa ulikua haihusiani na mahaba ila unaweka hivo hivo)
 
Wa ushuani mnaonekana tu!
Watoto wadogo mnawajua hata akina mariah Carey wakati si huku kwetu dedication ilikuwa RayC- uko wapi au afande sele -mkuki moyoni(ingawa ulikua haihusiani na mahaba ila unaweka hivo hivo)
Aiseee!! Hyo ya ray c ilikua
Inagusa penyewe mkuuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom