Enzi zetu mapenzi yalikuwa hivi

Jozee mkunaji

JF-Expert Member
Jun 11, 2017
457
1,000
ENZI ZETU

Mpenzi wangu nikupendaye kwa dhati.

Salamu nyingi sana zikufikie huko ulipo. Utakapo kujua khali yangu mie ni bukheri kabisa. Hofu na mashaka ni juu yako ewe mpenzi wangu uliye mbali na upeo wa macho yangu.

Dhumuni la barua yangu ni kutaka kukusabahi na kukushukuru kwa barua yako niliyoipata leo mchana. Ahsante sana kwa barua yenye maneno matamu kweli mpenzi wangu. Ama hakika moyo wangu ulijawa shauku kubwa niliposikia jina langu likiitwa pale assemble wakati barua zikigawiwa. Wajua ni namna gani nakupenda ewe kidani cha moyo wangu, chakula cha ubongo wangu, na tulizo la nafsi yangu.

Umeniambia kuwa shuleni kwenu huwa wanafungua barua wakiona ina mwandiko wa kiume. Safari hii nitamwomba monitress wetu aniandikie juu ya bahasha ili nisikuponze mpenzi wangu ukafukuzwa shule. Najua jinsi baba yako alivyo mkali mithili ya mbogo asije akakuchapa bure kishtobe wangu nikupendaye kiasi cha kukosa usingizi kwa ajili yako hadi naiona taswira yako kwenye bilauri ninywapo maji.

Mwezi ujao shule yetu itakuja shuleni kwenu kwenye debate. Ingawa mimi sijui mambo hayo ya debate nitafanya mchongo na msela wangu kiongozi wa debate aniandike jina ili nami nije. Nimekukumbuka sana. Nakumbuka wakati wa likizo tulivyokuwa tunakaa juu ya jiwe lile pembeni ya mto huku nikivichezea vidole vyako nawe ukiniimbia nyimbo za taratibu. Yaani sauti yako ni tamu utadhani kinanda. Kila siku huwa naisikia sauti yako ikiniimbia kwa mahaba ya dhati.

Nisikuchoshe kwa barua ndefu mpenzi wangu. Ila fahamu kuwa mwenzio juu yako sina hali. Nakupenda hadi nimepitiliza maana yenyewe ya neno kupenda. Daima umo mawazoni mwangu.

Msalimie sana yule rafiki yako uliyekuwa naye siku ile. Kuna rafiki yangu anampenda sana. Nitakuja naye kwenye debate.

Ndimi nikupendaye daima,
Mahabuba wako.

HD Wako peke yako

UJUMBE:
If you love three, you are not free,
If you love two, you are not true,
Love only one, that one is ME.

DEDICATION:
(1) Always Be My Baby - by Mariah Carey
(2) I Swear - by All 4 One.

#Zamani_raha_sana
 

Jozee mkunaji

JF-Expert Member
Jun 11, 2017
457
1,000
Hahahahhahaha, hatari sana..!! Nilikua na Counter book quire 3 nilikua nimeijaza mistari ya haja, lyrics za nyimbo..Nilikua nalitunza kuliko kitu choochote..!!

Lilinisaidia sana kuwa na mistari ya kuwang'oa warembo..!!
enzi zetu izo mkuu
 

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,080
2,000
Wa ushuani mnaonekana tu!
Watoto wadogo mnawajua hata akina mariah Carey wakati si huku kwetu dedication ilikuwa RayC- uko wapi au afande sele -mkuki moyoni(ingawa ulikua haihusiani na mahaba ila unaweka hivo hivo)
 

usser

JF-Expert Member
Sep 25, 2015
12,196
2,000
Wa ushuani mnaonekana tu!
Watoto wadogo mnawajua hata akina mariah Carey wakati si huku kwetu dedication ilikuwa RayC- uko wapi au afande sele -mkuki moyoni(ingawa ulikua haihusiani na mahaba ila unaweka hivo hivo)
Aiseee!! Hyo ya ray c ilikua
Inagusa penyewe mkuuu
 

usser

JF-Expert Member
Sep 25, 2015
12,196
2,000
Dhaaaaaa!!! Ebana eeeh
Mako n pale barua inafunguliwa mbele ya kadamnas af mwl kama anataka kuanza kuisoma hv

Nlikua kidogo nizime aisee
Bahat nzur haikusomwa

Siwema weee popote
Ulipo salam zkufkie


Barua yako ya mwisho nakumbuka uliniwekea na
Dedication ya ray c

Uko wap nikuone,,,,,,
 

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,474
2,000
Enzi zetu bhana, daaah sie kitaa tulikua hadi na nguli wa haya masuala, yaani kila mtu alikua anamfuata Rashid amuandikie barua ya mapenzi, Rashid alikua hatari hatari ana maneno mazuri sanaa af ana muandiko mzuriii, anyway nlipata simu when i was 14 nikakosaga hata wa kuwapigia au kuwatumia meseji yaani nlikuaga kama Lil Romeo flani iv, ila mwisho wa siku ni barua tu simu haina maana.
 

Mgodo visa

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
3,304
2,000
Hahahahhahaha, hatari sana..!! Nilikua na Counter book quire 3 nilikua nimeijaza mistari ya haja, lyrics za nyimbo..Nilikua nalitunza kuliko kitu choochote..!!

Lilinisaidia sana kuwa na mistari ya kuwang'oa warembo..!!
Kipindi hiko, nilikuwa ni CHIZI MAGAZETI...

Ili mradi tu nipate kurasa yenye nyimbo ya UMOMBO, nichane/nichonge vizuri na WEMBE na kuhifadhi kipande.

Lengo likiwa ni kukariri na kung'olea WAREMBO...

Zamani vijana tulikuwa more talented katika kuyaingia MAHUSIANO...

Kwa sasa ni PESA YAKO TU...
 

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,344
2,000
Sorry kwa kukukosoa, ila walioandika barua shallow hivi wengi walipata IV na O.

Barua ya kiswahili kitupu hivi? Sekondari? mh sijui...

labda mimi nilisoma mjini sana aisee. Sawa basi, lakini hata katerminology kamoja ka Biology ama kemia kweli? Sekondari?

Hapana aisee...hata hiyo introduction iko very shallow huyo mpenzi mlipomaliza shule ni lazima alikuacha tu! Barua haina uchangamfu, haina ubunifu...

Mh sijui labda ni mimi tu nimeona shida na hii barua lakini hii si barua ya kijana barobaro wa sekondari ndugu yangu.

Naomba samahani tena kwa kukukosoa!
 

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,766
2,000
Mi nilikuwa nasoma madongo kuporomoka huko, sina hili na hili kumbe DSM ngoma iliokuwa inahit ni NIWE NA WEWE MILELE ya Ray C.

Sa nikatumiwa barua na mtoto wa tuit mwanafunzi wa Kisutu. Nikaisoma afu nikapuuzia, coz hata wimbo wenyewe sikuwa naujua.

Sa kurudi likizo si ndio kuiskia ile ngoma! Eeeeh bana Eeeh. Kiuno bila mfupa.

Daah. Nikaanza kwenda race kwa yule bint. Daaah. Zamani.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom