Enzi za Mwinyi mambo yalikuwa mazuri sana

Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
7,552
9,528
Hii imekuwa kama wimbo wa taifa
Tangu awamu ya 5 ishike hatamu hakuna ambaye hajaguswa kwa namna moja au nyingine
Kwa wenye umri kama wangu ambao tumeziishi awamu zote mtakubaliana nami kila awamu ilikuwa na mazuri yake na magumu yake na maisha yalisonga wenye kujenga walijenga kila mtu kwa wakati wake kuna watu tulikuwa nao awamu zote hawa kujenga hata chumba na sebule leo hii ndiyo waimbaji wakubwa utasikia ooooh wakati wa mwinyi mkapa jk pesa ilikuwa nje nje tu na ukiangalia hakuna cha maana alichokifanya awamu zote sasa najiuliza hizo pesa nje nje mlikuwa mnazipeleka wapi na mlikuwa mnazitoa wapi ambapo leo hii hamzipati tena?
 
Biashara zilikuwa zina lipa. Tulikuwa tunauza kahawa kilogram 1 elfu 2000 wakati huu serekali imetupangia bei tumeuza kilogram 1 elfu 1000 tena siyo Cash kwa mkopo Ahsante.
 
Unaikumbuka kashfa ya loliondo?

Unamkumbuka KATABALO?

alipotezwa na huo utawala

Haya mambo ya kupitezana hayajaanza leo, hivo hakuna utawala uliokuwa bora ,

Wadanganye watoto wa juzi kuwa utawala wa mwinyi ulikuwa bora,
 
Hakika,Pumzika kwa amani mzee Ruksa,ila tunaomba busara zako kwa bwana Yule. Anaharibu umoja na amani wa Taifa letu.
 
Hata kama kuna makosa JPM amefanya, lakini tuwe wakweli.

Wakati wa awamu ya Mwinyi uchumi ulikuwa mbaya kuliko kipindi chochote. Ni kipindi ambacho hatukuweza kujenga hata mradi mmoja mkubwa.

Inflation ilipanda hadi kufikia 30%. Pesa ikawa inakosa thamani kwa namna ya ajabu.

Alipoingia dola 1 ilikuwa sh 20, anaondoka dola 1 ikawa sawa na sh 800!

Tusiwadanganye vijana, uchumi ulikuwa mbaya sana kipindi hicho japo ndicho kipindi tulichoongoza kwa kupewa misaada mingi.
 
We
Unaikumbuka kashfa ya loliondo?

Unamkumbuka KATABALO?

alipotezwa na huo utawala

Haya mambo ya kupitezana hayajaanza leo, hivo hakuna utawala uliokuwa bora ,

Wadanganye watoto wa juzi kuwa utawala wa mwinyi ulikuwa bora,
Wewe naye umesoma ila hujanielewa
 
Hii imekuwa kama wimbo wa taifa
Tangu awamu ya 5 ishike hatamu hakuna ambaye hajaguswa kwa namna moja au nyingine
Kwa wenye umri kama wangu ambao tumeziishi awamu zote mtakubaliana nami kila awamu ilikuwa na mazuri yake na magumu yake na maisha yalisonga wenye kujenga walijenga kila mtu kwa wakati wake kuna watu tulikuwa nao awamu zote hawa kujenga hata chumba na sebule leo hii ndiyo waimbaji wakubwa utasikia ooooh wakati wa mwinyi mkapa jk pesa ilikuwa nje nje tu na ukiangalia hakuna cha maana alichokifanya awamu zote sasa najiuliza hizo pesa nje nje mlikuwa mnazipeleka wapi na mlikuwa mnazitoa wapi ambapo leo hii hamzipati tena?
Enzi ya mwinyi saa 4 asubuhi umeshajaa pesa mfukoni,biashara zilikua zinalipa balaa watu walikua na pesa balaa,starehe kwa kwenda mbele.Mzee mwinyi katufungua macho vyomba vya habari TV redio magazeti ruksa.Tegeta Tabata Sinza Mbezi Mikocheni pamejengwa enzi ya mwinyi.Barabara za lami zikajengwa.Mkapa kaja kaasisi ufisadi kuuza mali za umma
 
Hata kama kuna makosa JPM amefanya, lakini tuwe wakweli.

Wakati wa awamu ya Mwinyi uchumi ulikuwa mbaya kuliko kipindi chochote. Ni kipindi ambacho hatukuweza kujenga hata mradi mmoja mkubwa.

Inflation ilipanda hadi kufikia 30%. Pesa ikawa inakosa thamani kwa namna ya ajabu.

Alipoingia dola 1 ilikuwa sh 20, anaondoka dola 1 ikawa sawa na sh 800!

Tusiwadanganye vijana, uchumi ulikuwa mbaya sana kipindi hicho japo ndicho kipindi tulichoongoza kwa kupewa misaada mingi.
Nadhani ulikua mtoto bado enzi za mwinyi hata BOT ilikua inanunua dhahabu shilingi ikawa na nguvu kuja mkapa ikaanza kuporomoka
 
Hakuna rais ambaye alikuwa anagawa pesa kwa kila mtu kiasi kwamba kila mtu aseme awamu fulani maisha yalikuwa mazuri. kama wewe unaona kipindi cha mwinyi maisha yalikuwa mazuri basi kuna mwingine aliona mabaya na anaona mazuri sasa. wanadamu wanatofautiana mtazamo, radha, hisia na hamu.
 
Watanzania hawajui wanataka nini
Hakuna rais ambaye alikuwa anagawa pesa kwa kila mtu kiasi kwamba kila mtu aseme awamu fulani maisha yalikuwa mazuri. kama wewe unaona kipindi cha mwinyi maisha yalikuwa mazuri basi kuna mwingine aliona mabaya na anaona mazuri sasa. wanadamu wanatofautiana mtazamo, radha, hisia na hamu.
 
Ambae hakubahatika kupitia awamu hizi zoote, maandishi ya humu yanaweza kuwa yanampotosha
Uchumi kuporomoka ki vipi wakati kabla ya hapo ilikua foleni maduka ya kijiji na RTC kupata kilo 1 ya sukari???magari j2 hakuna kuendesha mpaka kibali maana petrol ilikua hakuna.Bia ni kwa mgao Sigara ni pafu moja unalipia
 
Back
Top Bottom