Enzi za Mwinyi – Best Days of My Life! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Enzi za Mwinyi – Best Days of My Life!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ngwanakilala, Aug 7, 2011.

 1. Ngwanakilala

  Ngwanakilala JF-Expert Member

  #1
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  When I look by at my life, sitasahau enzi za Mwinyi (naongelea hali ya maisha ya watu binafsi, furaha, amani na upendo – life standard & peace of mind).

  Nilikuwa niko sekondari, sina bili sina stress. Wazazi wangu wote wako hai, wanahela kama njugu. Karibu ndugu zangu wote wako hai, wana hela kama njugu. Nasafiri as I wish during holidays. Nna vigirlfriend vyangu. Wasichana wazuri wadogo, innocent with real love—life was Juicy. Nilikuwa na marafiki zangu wote wakutoka primary, sekondari na mtaanii. Life was stress free, wazazi walikuwa stress free, wanandugu walikuwa wanapendana sana na kuishi kwa upendo na amani. Kulikuwa hakuna maandamano ya wanavyuo kiivyo, hakuna machafuko ya kisisasa kiivyo, kazi zilikuwepo, madili yalikuwepo. Kulikuwa hakuna wizi wa ajabu ajabu serikali. Maisha yalikuwa mazuri yenye amani, utulivu na upendo sana.

  Punde akaja Mzee Ukapa. Najua huyu bwana alifanya makubwa statistically lakini that was the beginning of the end. Hela ikayeyuka kama maji yameanikwa juani. Kila mtu akawa hana hela, wengine wanapoteza kazi, stress everywhere, familia zikaanza kuparaganyika, amani na upendo vikaaanza kutoweka taratibu kama summer wakati wa spring. Wanandugu kibao wakaanza kufariki. Na mimi nikaanza kuwa mtu mzima na majukumu kibao. Marafiki wakaanza kusambaa vyuoni na wengine ulaya. Magirlfriend wakaanza kuwa materialistic-hapendwi mtu pochi tu.

  Baada ya hapo akaja Baba Riziwani. Hiki kipindi nakibatiza kipindi cha Things Fall Apart! Life ya watanzania as we know it ika-disappear na kubakiwa na commotions, confusions and frasturations. Kila mtu na kila kitu kiko confused, disorganized and dissapointed. Ukiangalia maisha ya watanzania na Tanzania yenyewe utawaonea huruma. Ni Kama Somalia in essence. Ni kama hakuna serikali na kila mtu anajifanyia vyake na wanaooumia ni wananchi wa kawaida. Sijawahi kuona kipindi ambacho nchi imevurugika na maisha kuharibikia nchi Tanzania kama wakati huu. Hali ya maisha kwakweli imeharibika sana na inavyoelekea itaendelea kuharibika zaidi siku hadi siku. Kila nnaemjua namuona to some extent yuko stressed and dissapointed. There is no light at the end of the tunnel. Bora ya sisi tuliosoma kidogo labda tuta weather the storm lakini ndugu zetu wengine – Duuh.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Aug 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  yaani hauko peke yako kwa hilo

  kuna watu machozi yanawatoka wakikumbuka enzi za ruksa
   
 3. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #3
  Aug 7, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 446
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Yaelekea nyie mlikuwa na kampuni za clearing na forwarding
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Aug 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  enzi za ruksa
  sinza iligeuka kutoka mashamba mpaka mji
  mbezi beach ni ugomvi wa viwanja tu lol
  dah,mwinyi amewapa wengi maisha na wengi wao wanamtukana leo hii
   
 5. Ngwanakilala

  Ngwanakilala JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Mkuu The Boss kama umeotea - tulikuwa tunakaa Sinza. Life was so sweet Mzee weekend kuogelea chuo kikuu, mpira abajalo, mitumba manzese na kariakoo, kwenda mwenge kwa miguu, weekend osterbay beach, la dolce vita, sleepway - you name it. Nilikuwa nikienda Keko au Temeke naona kama nchi za nje. hahahahah
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  ukizungumzia maisha bora kwa watanzania
  mwinyi was the best president so far
  watu walikuwa wanaacha kazi kufanya biashara
  sasa hivi hata kazi ya u messenger inagombaniwa
   
 7. Ngwanakilala

  Ngwanakilala JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Yaa nawakumbuka matajiri wa enzi zile akina Fordi wa Sinza, Job Mziwanda wa Bahama Mama, Bujugo, Mwanamboka, Super Star, Rwegasira wa Silent Inn, Sun Down ya Sinza, John Ngogwe, Achimwene (Mzee Wadi), Paulo Lyimo wa wa La Prima, Ayubu Kipipa, Macheni, Mzee Mahindi wa Chick King, akina Saba General, Mao Wambura, Joe wa Joes up date wear kindondoni

  Viwanja vya Best Bite, Joli Club, Kwa Mbise, Mwika, Karibu Hotel, Slip way, contena mbezi beach, bills, hoteli ya mawingu arusha

  Enzi za kukodi coaster za kwendea beach. Hahahahaha! Nchi nzima ilikuwa shambra shambra.
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mimi nakumbuka mchezo wa sikukuu ikiangukia weekend mnailipia siku za kazi lol
  enzi zile watu walikuwa starehe sana
  siku hizi watu wanafanya kazi wenyewe mpaka weekend
  maisha magumu mno lol
   
 9. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #9
  Aug 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu safi hiyo ilikuwa upande wako and glad you still remember those days, but here is the other side of the story!

  Mkuu unajua tuliograduate wakati huo huwa hatutaki kabisa kisikia hiyo era ya Mzee ruksa, kulikuwa hakuna kazi completely tena hasa kwenye uhandisi..., The place was fast and crazily becoming a lawlessness kinda of a country. Na mengi tunayoyaona leo chimbuko lake ni kipindi hicho. This was the era when honest and integrity vilizikwa na ujanja ujanja ikawa ndiyo the way. I know some guys walioamua kuweka kisomo pembeni na kuingia kwenye hivyo vi-clearing and forwarding. Made some few bucks got most of wht was regarded highlife in those days. Many pple lived in illusion and fantasy and some have never come back. Huu ndio wakati haswaa alternative ya ughaibuni in my case ilipoanza kutake charge.

  Wafanyabishara wakweli na walipaji kodi ndiyo walipopoteza kipindi hiki, rare proffesionals kama madaktari walionekana kama just some loosers!!!!!!!!!! Boy!! unajua daktari alikuwa nalipwa mshahara bei gani wakati huo???? Nyie acheni bwana haya mnayoyaona leo ufisadi, ujanja ujanja, kukosekana uwajibikaji, wizi, money is everything, lack of proffesinalism ndiyo the price tunayolipa kutokana na the shortlived fantassies watu walizoona ndiyo maisha wakati wa mzee ruksa!!!!!! Kifupi hakuna nchi duniani inaweza kuendeshwa kwa mfumo ule in a long term.

  Boy! unajua serikali wakati huo ilikuwa inakusanya kodi sh. ngapi kwa mwezi?????? Nyie acheni bana na tabu nyingine iliyoletwa na kipindi kile ilikuwa ni influx ya watu kukimbilia mijini, that's why Dar leo kuna watu kama 4m. To tell you the truth Tanzania kwa jinsi mambo yalivyo bado hatuna uwezo hata wa kuwa na jiji la kisasa lenye huduma zote muhimu la watu milioni mbili.

   
 10. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu, and you think that was the right way, how do you run a country na wachuuzi???? When aeverybody is mchuuzi, middle man???
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Aug 8, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  tunaweza kutofautiana mkuu
  kufanya biashara halali ni kitu kizuri
  hatuwezi woote kuajiriwa,tena serikalini
  nchi zote zenye uchumi mzuri watu hawagombanii kuajiriwa serikalini
  mwinyi alikuwa na makosa mengi pia,
  but umuhimu wa kuwepo industry nyingi zingine zinazotoa ajira uko pale pale
  ili mradi usimamizi na regulation uwepo,sizungumzii ujanja ujanja hapa
   
 12. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,302
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  <br />
  <br />
  Mkuu umenikumbusha mbali sana na mimi nilikua Sinza enzi hizo. Ayubu Kipipa yuko wapi siku hizi? Umemsahau Kadata Kadata, Mazola huyu bilboards zote za Sinza nzima alikua anachora yeye.!
   
 13. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #13
  Aug 8, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hii mnaikumbuka? "usipowajibika utakumbana na mfagio wa chuma". Sijui ilikopotelea na bdae kila kitu kikawa ruksa!
   
 14. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,045
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Mwinyi was the best president ever in Tanzania although ndo kipindi nilijikusanyia vijisent mapema na kulikimbia vumbi.long life mzee rukhsa.
   
 15. Ngwanakilala

  Ngwanakilala JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 396
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 60
  Mzee Nyambala sisi tunaongelea hali ya maisha ya watu wa kawaida, amani na utulivu (peace of mind). i bet wewe mwenyewe wazazi wako wote na ndugu zako kibao walikuwa hai mnafurahi pamoja kila mnapokutana. Ukoo ulikuwa umeshikama na watu wanasikilizana, kupendana na kuelewana. Wewe mwenyewe ulikuwa na washkaji kibao kutoka sekondari hadi chuo.

  Hela ilikuwa inapatikana, biashara zinalipa, kazi zinafanyika na starehe zinafanyika. Dalisalama panakalika. Sasa hivi kama huna hela au kazi Dar chungu hapakaliki. waandishi wa habari tatizo lilikuwa nchi nzima walikuwa wanasoma journalism na hotel magement forodhani that was the problem ila other than that life was sweet back then.


  Mzee Fabolous umenikumbusha mbali sana kadata kadata na Bar ya Linje na Hoteli ya Namnaani. hahahaha!
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  life was ****ing hell enzi ya mwinyi. mkapa era was the best!
   
 17. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  it is useless to cry over spilt milk and things have to change for life to move on. Mwinyi had his time, then Mkapa came over before handing it to Kikwete. Whereas you might undermine Kikwete's competence, some finds him strong and bright.
   
 18. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #18
  Aug 8, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu nimekuelewa sana nilichokielezea ni the other side of the story and especially kwa upande wangu. Hicho ndicho kipindi nilianza maisha ya kujitegemea. Man it was hell!!!! Muulize mtu yeyote aliyegraduate wakati huu!
   
 19. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #19
  Aug 8, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ifeel your pain bro lakini hii ya kusoma ili upate kazi haijakaa vizuri kuna masomo ambayo hata kabla hujamaliza unafahamu nisipopata kazi nitafanya hiki.
   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  Aug 8, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Boss sijakataa kwamba kufanya biashara ni kitu kizuri lakini aina za biashara zilizokuwepo wakati wa Mwinyi hata siku moja zisingetufikisha kokote, Mtu ananunua shati la mtumba (made in Taiwan) Tandika, anakuja kuliuza posta, posta linanunuliwa kwenda kuuzwa Sinza... wote hapo wameishi lakini ukiangalia fundamentally hakuna kodi iliyolipwa, shati ni la Taiwan... Unakumbuka "vitu vya kupointi"????

  Na the so called ajira serikalini mimi ni mmoja wa watu ambao siamini katika hilo na ndiyo maana so far sijawahi na wala sitaki kuajiriwa na serikali, sekta binafsi ndiyo haswaa inapaswa kuwa source kubwa ya ajira.

  Mkuu hakuna kitu kinanisikitisha kama kuona nguvu kazi iliyopo hapo Dar badala ya kujishughulisha na uzalishaji utakuta eti mtu katoka Kigoma anakuja mjini kuendesha baskeli. Ukienda pale Africana kuna baskeli mpka leo zinapiga ruti maeneo.
   
Loading...