Enzi Za Mwalimu

ibanezafrica

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,261
6,543
Kampuni ya mabasi taifa(Kamata)
Urafiki Textile
Mwatex
Sungura TeX
Kilitex
Musoma TeX
Tabora Spinning
Ubungo spinning
Ufi
Kibuku
Tipper
Bhesco
General tyre
N.M.C.
R.T.C
National Panasonic
Nasaco
Tacoshili
Tanzania Elimu Supply
National housing Corporation
Tanzania Dairies Ltd (Maziwa)
Tanzania Fishnet
Uda
TRC
Agip(T)Ltd
Esso
Shell Tanzania
Embassy Hotel
Motel Agip
Dodoma Hotel
Tabora Hotel
Tanganyika Packers Ltd
Tancut-Iringa
Morogoro Canvas
Swala bicycles
Nyumbu
Tamco Kibaha....nk

Nimekumbuka Enzi tuliokulia wakati huo hakuna ada ya kumwona daktari..!so ilikua hauhitajiki kubeba pochi kwenda kutibiwa!
Shule daftari ikiisha linachanwa unapewa jipya!
Dar es salaam magari ya taka yalipita kila mtaa kukusanya taka bure!
Walipita wapuliziaji dawa vyooni na makaroni bure!
Kulikua na street lights
Uda ilifika hadi Kongowe,Tandika kilakala,Mlandizi nk
Chai ya maziwa na mkate wa siha ilikua jambo kawaida kila asubuhi kila nyumba
Hata sie wanyongeTuliishi nyumba za Nhc!
Noli noli(ambulance)zilifika uswahilini kubeba wazazi
mia nyekundu ilikua na nguvu ajabu!
Ee mungu turudishe enzi zile! Enzi za Mzee majambo !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ibanezafrica umenikumbusha mbali sana enzi za Mzee Majambo. Alikuwa anauza karanga huku akiimba Majambo njeeenjeenjeee. Kuna mdogo wangu alikuwa anamuogopa sana yule Mzee. Mungu amlaze Mzee Majambo mahala pema peponi...Amina.

Enzi hizo kuna yale magari ya kuuza Koni yanapita mitaani. Baba wa Taifa aliwezaje kufanya yote hayo kwa weledi na ufanisi wa hali ya juu!? Huwa najiuliza nashindwa kupata majibu. Ni wapi Watanzania tulipokosea kama Taifa!?
 
So proud.

Mchana au alasiri ukisikiliza Radio Tanzania Dar Es Salaam ...

But nakumbuka enzi hizo kiwanda cha saruji wazo walikuwa na mabasi ya staff yakifika mpaka mtaani kuwachukua wafanyakazi akiwemo my late dady.
 
Hata Huyu Yuko Vizuri, Fly Over, Stg, Mwendokasi, Bombadia, Drimlaina, Air bus, Na Mengine Mengi Yanakuja Kwa Wakati Wake
 
Hata Huyu Yuko Vizuri, Fly Over, Stg, Mwendokasi, Bombadia, Drimlaina, Air bus, Na Mengine Mengi Yanakuja Kwa Wakati Wake
 
Sasa miaka Hiyo huduma hizi zilipatikana mjini zaidi huko vijijini watu walikuwa choka mbaya usafiri shida shule unaifuata kilometres 30 nenda rudi zinakuwa kilometres 60 zahanati za kulenga na manati usafiri siku 7 uko njiani
 
Umenikumbusha aise bwana na bibi afya wanapita nyumba kwa nyumba na balozi kuhakikisha dawa imepuliziwa kwenye mashimo yote.

Balozi anawatambua watu wake hadi mgeni anayeishi kwako anatambulika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio sababu haukushuhudia hayo aliyoandika mleta mada. Enzi za Baba wa Taifa huduma za Afya na Elimu zilikuwa bora sana. Gari za wagonjwa na huduma za afya zilikuwa bora. Kulikuwa kuna huduma za kumwaga na kupuliza Dawa kwa kila nyumba ili kuzuia na kutokomeza magonjwa kama Malaria na mengineyo. Madaftari tulipewa shule. Huduma za afya zilitolewa bure kabisa. Kulikuwa na Maduka ya Kaya na Maduka ya Ushirika. Kila nyumba ilikuwa na kadi ya ushirika...hii ilikuwa inakuwezesha kufanya manunuzi katika Maduka ya Kaya na ushirika kwa bei nafuu na ya kumudu.

Usafiri katika jiji la Dar es salaam ulikuwa wa kistaarabu sana enzi tukitumia mabasi ya UDA aina ya Ikarus 280 na Leyland.
Mitaa mingi ilikuwa na barabara za lami na mataa ya barabarani.
Tulikuwa tunaishi kwa Umoja na Upendo katika jamii zetu.
Ni hayo machache tu nimeorodhesha kwa sasa, wadau wengine watajazia.
Ila maisha yalikuwa matamu sana wallah.
 
ibanezafrica umenikumbusha mbali sana enzi za Mzee Majambo. Alikuwa anauza karanga huku akiimba Majambo njeeenjeenjeee. Kuna mdogo wangu alikuwa anamuogopa sana yule Mzee. Mungu amlaze Mzee Majambo mahala pema peponi...Amina.

Enzi hizo kuna yale magari ya kuuza Koni yanapita mitaani. Baba wa Taifa aliwezaje kufanya yote hayo kwa weledi na ufanisi wa hali ya juu!? Huwa najiuliza nashindwa kupata majibu. Ni wapi Watanzania tulipokosea kama Taifa!?
Duuuh! Mimi sikuwepo enzi za Mwl. Lakini kwa habari ambazo nazisikiaga huku mtaani kutoka kwa wahenga kuhusu mazuri aliyeyafanya Mwalimu halafu yakaja kuharibiwa huwa nahamu siku moja viongozi wetu watueleze ni nini kilitokea au wapi tulikosea kama taifa sababu haiwezekani Mwl. alifanya mambo makubwa kama hayo na alikuwa hachimbi madini halafu leo tunashindwa, angalau awamu hii wanajitahidi kiasi chake.
 
Ndio sababu haukushuhudia hayo aliyoandika mleta mada. Enzi za Baba wa Taifa huduma za Afya na Elimu zilikuwa bora sana. Gari za wagonjwa na huduma za afya zilikuwa bora. Kulikuwa kuna huduma za kumwaga na kupuliza Dawa kwa kila nyumba ili kuzuia na kutokomeza magonjwa kama Malaria na mengineyo. Madaftari tulipewa shule. Huduma za afya zilitolewa bure kabisa. Kulikuwa na Maduka ya Kaya na Maduka ya Ushirika. Kila nyumba ilikuwa na kadi ya ushirika...hii ilikuwa inakuwezesha kufanya manunuzi katika Maduka ya Kaya na ushirika kwa bei nafuu na ya kumudu.

Usafiri katika jiji la Dar es salaam ulikuwa wa kistaarabu sana enzi tukitumia mabasi ya UDA aina ya Ikarus 280 na Leyland.
Mitaa mingi ilikuwa na barabara za lami na mataa ya barabarani.
Tulikuwa tunaishi kwa Umoja na Upendo katika jamii zetu.
Ni hayo machache tu nimeorodhesha kwa sasa, wadau wengine watajazia.
Ila maisha yalikuwa matamu sana wallah.
Aiseee hizi shida zimetoka wapi sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom