Enzi za mwalimu Nyerere, Waziri wa Utalii, Dr. Kigwangalla angeeleza alikopeleka pikipiki 25

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,507
141,236
Najikumbusha tu namna viongozi wa umma walivyoishi kwa maadili yasiyotia shaka enzi za awamu ya kwanza ya JK Nyerere.

Waziri kununua pikipiki 25 kwa fedha taslimu wakati wa kuelekea uchaguzi lazima angeitwa na tume ya maadili pale jirani na Avalon cinema kujieleza.

Yote kwa yote namuunga mkono Dr Kigwangalla kwa kuzitetea sh bilioni 20 za Simba SC ambazo Mo Dewji anadaiwa.

Maendeleo hayana vyama!
 
Kigwangala anajua kila mmoja ametoa Rushwa ndani ya CCM ndio maana anajiamini.
 
Hiyo serikali na kiongozi wake anajua hizo pikipiki ni za nini, hivyo hawataweza kumuuliza.
 
Kwani hapa TZ, kuna tume ya maadili kweli? Ndio naisikia leo, kweli ingekuwepo BASHITE angeponea wapi? Licha ya malalamiko ya meya wa ubungo jacob?
 
Chama cha MAJIZI na MAFISADI PAPA,. CCM ya Magufuli wote ni MAJIZI yanashindana kuibia nche yetu.
BABA LAO linaongoza.
LIJIZI la 2,4 TRILLION zetu lipo IKULU.
 
Yote kwa yote namuunga mkono Dr Kigwangalla kwa kuzitetea sh bilioni 20 za Simba SC ambazo Mo Dewji anadaiwa.
wanaSimba tunamchukia Sana huyu Kigwa kwa ushakunaku anaousambaza dhidi ya muwekezaji wetu Mo. Akome tena akome kweli kweli (in jiwe's voice).
 
Pikipiki 20 ni wastani wa milioni 50 za kitanzania. Akiwa kama mtumishi wa umma ni fedha nyingi kuhonga jimboni. Ila alipata kiinua mgongo chake hivyo kama ana uhakika wa kurudi kutoa hapo milioni 50 siyo ishu!
 
Back
Top Bottom