Enzi za Mwalimu Nyerere mbunge wa Kigoma Mjini Zitto angewekwa kizuizini kwa matamshi yake

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,559
Ananieleza Mzee Mgaya kwamba Rais Magufuli ni mkali lakini ni muungwana na mvumilivu sana.

Enzi za Mwalimu Nyerere huyu Kabwe angekuwa kizuizini muda huu akichunguzwa juu ya kauli zake za mara kwa mara zilizojaa uchochezi, anaeleza MzeeMgaya.

Waziri katumbuliwa na kosa lake limeelezwa wazi lakini anaibuka Mbunge anadai Waziri kamzunguka Rais ndio maana katumbuliwa, Nyerere asingemvumilia huyu mchochezi vyombo vya dola lazima vingemuhoji, amemalizia mzee Mgaya.

Maendeleo hayana vyama!
 
Angalikuwapo Mwl. Nyerere hoja zingejibiwa kwa hoja, na mara kwa mara aki "fly abroad" ili kupanua maelewano ktk wigo wa kiplomasia za kimataifa. Wala asingekuwa na upendeleo kuliko maeneo mengine muhimu ya kiuchumi, kwa ajili ya Butiama tu, na hata kupeleka huko maendeleo ya vitu pasipo kuwa na aibu yoyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui Zitto ana ushahidi gani kuwa mh raisi kazungukwa,nadhani huu ndio wakati wa kumsweka ndani halafu ndio akalalamike kwa wajomba zake nchi za magharibi
 
Huyo jamaa ni kumpotezea tu nafikiri hata Serikali yenyewe wameshajua kwamba wanadili na mtu anayependa attention kama mtoto ndo maana analazimisha kukamatwa, hivyo wanampotezea tu.

Jamaa hana input yoyote hata kwenye Chama chake tu hakuna chochote anachoweza kuonyesha, binafsi huwa nashangaa hata huko kwa Muzungu wanakokimbilia si ni lazima uwe na cha kuonyesha? Sasa wewe una Mbunge 1 nani atakusikiliza? lkn bado makelele meengi urafikiri yeye ndio mpinzani Mkuu TZ, kumbe, ...
 
Huyo jamaa ni kumpotezea tu nafikiri hata Serikali yenyewe wameshajua kwamba wanadili na mtu anayependa attention kama mtoto ndo maana analazimisha kukamatwa.

Jamaa hana input yoyote hata kwenye Chama chake tu, lkn makelele meengi urafikiri yeye ndio mpinzani Mkuu TZ, kumbe wapi.
Lakini tukiachana na tabia za Zitto, jee anayoongea huoni mantiki yake? Mangapi yamefanyika bila kupitia bungeni kwa nini hili tuu ndio limtie hasira mzee baba?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakaza Mwalimu hakupenda watu wakucheka cheka, rejea hotuba ya Mwalimu 1995 akihutubia mkutano mkuu wa CCM Dodoma!

Mwalimu alihitaji watu kama Magufuli, akikuambia hiki kinyesi amemaliza, ata umuulize kesho kile ulisema nn? Atakujibu "Kinyesi." sasa kuna wengine leo anakuambia kinyesi kesho anakuambia mkate!
 
Zama zinabadilika... Na wewe ubadilikage...!
Ndo maana babu zako hawakuwahi kumiliki simu na maisha yao yalisonga bila wasi wasi!
Kwako wewe bila simu ya kupangusa maisha ni kama yana stuck stuck!
Zitto yupo very right... Hata ukimfufua Mwl. Nyerere atakubaliana nae!
 
johnthebaptist,
Huyo Mzee Mgaya angeeleza kama aliyoyasema Mh Kabwe ni uongo hapo ningemwona wa maana, lakini hajakanusha hayo badala yake karukia mengine.

Huyo Mzee kakueleza kwamba Mwalimu aliyafanya kama hayo aliyoyaeleza Mh Kabwe?

Ubaya ni kwamba wewe hapo ndio mpotoshaji na kumfanya mzee Mgaya awe mwongo; Hakukueleza habari za akina Lissu na wengine yaliyowapata? Hayo yalitokea wakati wa Mwalimu?

Njia zenu za kunyamazisha watu kwa vitisho; hivi hamchoki kuzitumia njia hizo hizo hata baada ya watu kuzitambua mbinu zenu hizi?
 
Huyo jamaa ni kumpotezea tu nafikiri hata Serikali yenyewe wameshajua kwamba wanadili na mtu anayependa attention kama mtoto ndo maana analazimisha kukamatwa, hivyo wanampotezea tu.

Jamaa hana input yoyote hata kwenye Chama chake tu hakuna chochote anachoweza kuonyesha, binafsi huwa nashangaa hata huko kwa Muzungu wanakokimbilia si ni lazima uwe na cha kuonyesha? Sasa wewe una Mbunge 1 nani atakusikiliza? lkn bado makelele meengi urafikiri yeye ndio mpinzani Mkuu TZ, kumbe, ...
Hana input, unaijua maana halisi ya input
 
Chakaza Mwalimu hakupenda watu wakucheka cheka, rejea hotuba ya Mwalimu 1995 akihutubia mkutano mkuu wa CCM Dodoma!

Mwalimu alihitaji watu kama Magufuli, akikuambia hiki kinyesi amemaliza, ata umuulize kesho kile ulisema nn? Atakujibu "Kinyesi." sasa kuna wengine leo anakuambia kinyesi kesho anakuambia mkate!

..Jpm ni mtu muongo, mzushi, mdhalilishaji, mropokaji, fisadi, na mkatili.

..Mwalimu alikuwa havumilii watu wa namna hiyo ktk safu yake ya uongozi.
 
Mzee mgaya fisadi tu anayelalamika kwa sababu ya njaa na kutafuta uteuzi.

ENZI ZA MWALIMU BUNGE LINGEHESHIMIKA.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom