Enzi za Mwalimu Nyerere mbunge wa Kigoma Mjini Zitto angewekwa kizuizini kwa matamshi yake

Zama zinabadilika... Na wewe ubadilikage...!
Ndo maana babu zako hawakuwahi kumiliki simu na maisha yao yalisonga bila wasi wasi!
Kwako wewe bila simu ya kupangusa maisha ni kama yana stuck stuck!
Zitto yupo very right... Hata ukimfufua Mwl. Nyerere atakubaliana nae!
Mbona Zitto kagonga penyewe.
 
Tusipigane michanga ya macho. Zitto anafanya yote hayo kwasababu Maalum.. Ni joka la kibisa ama mbwa mkali asiye na meno... Wanamfahamu vema na ni faida kwao... Ni lazima awepo mtu wa kupigapiga kelele ili ionekane serikali inavumilia na kukubali kukosolewa.

Itakapokaribia uchaguzi atalipwa chake kama ilivyokuwa 2015. Zitto ni mpinzani kwa hoja na takwimu lakini hana misimamo imara... Yu rahisi mno kugeuka na kuvaa ngozi ya kondoo. johnthebaptist,

Jr
 

Attachments

  • downloadfile-16.jpeg
    downloadfile-16.jpeg
    21.1 KB · Views: 1
johnthebaptist,
Nyerere alikuwa aweki ndani watu kwa kuongea😂😂 Nyerere alikuwa ni mtu wa debate mzuri sana hayawahi kukimbia mahojiano na mijadala hata siku mmoja. Hatujapata mtu kama yule kwenye debates
 
Sijui Zitto ana ushahidi gani kuwa mh raisi kazungukwa,nadhani huu ndio wakati wa kumsweka ndani halafu ndio akalalamike kwa wajomba zake nchi za magharibi
Mheshiwa Zitto Kabwe amekuja na vielelezo hata wewe hukuona au hujasoma alicho andika? Yaani mifano yote aliyo toa pale huelewi? Kuongoza taifa la wajinga ni kazi rahisi sana.


/
 
Tuanzie kwenye sheria zinasemaje kwenye suala la kusaini mikataba nje ya nchi,,na waziri anaposafiri kwenda nje huwa anapata ruhusa kwa nani miongoni mwa viongozi wa nchi,,,Waziri pamoja na timu yake wakati wanaondoka kwenda Romania walitoroka bila kuwajulisha wakubwa zao.

Je usalama wa taifa pamoja na uhamiaji kwenye kiwanja cha ndege walichokitumia kupanda ndege hao viongozi hawakushituka kumuona kiongozi tena mwenye dhamana ya usalama wa Raia na mali zao akiondoka bila ruhusa ya wakubwa zake,,Usalama wa taifa unafanya kazi gani hadi unashindwa kumsaidia Rais kwenye kadhia hii?IGP SIRRO hakujulishwa na kamanda Andengenye kwamba anaenda nje ya nchi?

SIRRO hakumuliza mdogo wa kicheo kuhusu safari husika?na kama analijulishwa hakuweza hata kumshauri jinsi taratibu zinavyotakiwa kufanywa?hivi wizara haina mwanasheria wa kuwashauri viongozi wa wizara?Tutafakari kwa kina ili tujue chanzo ni nini?ikiwezekana wandishi wa habari waende Romania kujua zaidi ya zaidi maana kuna kizungumkuti.TUIJENGE TANZANIA KWA MUSTAKABALI WA KIZAZI KIJACHO.
 
Nyerere wa sasa hivi ndio baba lao, ukimkosoa tu na kuweka hadharani mambo yake ya uvuguni, mara umepotezwa kwa kutekwa na watu wasiojulikana, ukipona katika hilo ujue kuwa pyuupyuu inakuhusu, kwa wale waliopona kama Zitto ni Mungu tu anawalinda.
 
Msifananishe pilau na makande!
Mwl kwanza alikuwa hawadharirishi mawaziri/viongozi hadharani hata kama anawaondoa ilikuwa unasikia tu "Amestaafishwa kwa manufaa ya umma".

Mwalimu hawezi kuwa kufanana utendaji na huyu anayejiita kichaa! johnthebaptist,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
We Na Huyo Mgaya Wote Kama Mume Wa Hamida tu Mnafikiria Kama Kambale

Mnabaki Kutapatapa Unajaribu Kuchochea Ili Awekwe Kizuizini Sahau Ukweli Hushinda Milele

Mwambie Kizee Wako Azeeke Kiustaarabu Sio zama Za Nyerere hizi..

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu johnthebaptist wala hajawahi kumconsult huyo Mzee Mgaya hata siku moja, anajiandikiaga tu kuchochea hadhira. Usije ukamkosea adabu mzee wa watu bure
 
johnthebaptist,
Nyerere alikuwa hafanyagi mambo ya kijinga kabisa kama ya awamu hii, ukweli utabaki kuwa ukweli bila kujali unamgusa nani. Kifupi ni kuwa awamu ya tano inongoza kwa ufisadi wa viongozi wa ngazi za juu
 
Back
Top Bottom