Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,952
- 4,326
Kwanza napenda ku declare interest kwamba mimi si mwanachama cha siasa cho chote. Mimi ni mwanasayansi tu!
Hili suala la kuahirisha mikutano ya hadhara ya kisiasa kwa sababu ya uhafifu wa vipaaza sauti linanipa taabu sana kulielewa.
Sayansi ya vipaaza sauti ni nyepesi sana, hata wahitimu wetu toka vyuo vyetu vya VETA ambao tunao wengi kila sehemu nchini ni magwiji sana wa tekinolojia hii. Hata kwenye sherehe za harusi, disko n.k. hili huwa haliwapi taabu. Hata Enzi za akina Nyerere na Kawawa haikuwahi kutokea eti mkutano unaahirishwa kwa kukosa kipaaza sauti. Walikuwa na nguvu na uwezo wa kuhutubia maelfu ya watu hata bila kuwa na vipaaza sauti na watu wakawasikia vizuri tuu.
Naomba mtujuze ni wapi pengine nchini au sehemu nyingine duniani ambapo mkutano mkubwa wa hadhara wa kisiasa ulishapata kuahirishwa kwa sababu ya vipaaza sauti?