The August
JF-Expert Member
- Oct 9, 2018
- 1,080
- 2,024
Habari wakuu!
Miaka ya nyuma kabla Runinga hazishamili na pia kabla mpira wa Ligi kuu ya Tanzania bara kuanza kuonyeshwa kwenye MaTV, basi tulikua tukisikiliza mapambano kupitia Radio Tanzania Dar es salaam (RTD). Kwa kweli enzi hizi tuliijua ladha ya mechi hizi kwa fikra za kichwani. Watangazaji kama kina Ahmed Jongo walizinogesha sana mechi hizi kwa simulizi murua.
Nakumbuka sana Jinsi Edibily Jonas Lunyamila alivyokuwa akipambwa na watangazaji hawa.
Yupo mwandinga Saidi Mwamba kizota huyu bwana nasikia alikoa anatokea kwenye kupiga pombe lakini anaingia uwanjani kusukuma gozi na shughuli yake si ya kitoto. Je, hili linaukweli?
Hebu tukumbushane kuhusu mpira nyakati za radioni tu pamoja na visa na mikasa ya wachezaji enzi hizo.