Enzi za Mpira RTD: Tukumbushane Visa na Mikasa ya wakati huo.

The August

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
1,080
2,024
Habari wakuu!

Miaka ya nyuma kabla Runinga hazishamili na pia kabla mpira wa Ligi kuu ya Tanzania bara kuanza kuonyeshwa kwenye MaTV, basi tulikua tukisikiliza mapambano kupitia Radio Tanzania Dar es salaam (RTD). Kwa kweli enzi hizi tuliijua ladha ya mechi hizi kwa fikra za kichwani. Watangazaji kama kina Ahmed Jongo walizinogesha sana mechi hizi kwa simulizi murua.


Nakumbuka sana Jinsi Edibily Jonas Lunyamila alivyokuwa akipambwa na watangazaji hawa.

Yupo mwandinga Saidi Mwamba kizota huyu bwana nasikia alikoa anatokea kwenye kupiga pombe lakini anaingia uwanjani kusukuma gozi na shughuli yake si ya kitoto. Je, hili linaukweli?


Hebu tukumbushane kuhusu mpira nyakati za radioni tu pamoja na visa na mikasa ya wachezaji enzi hizo.

Screenshot_20190513-182949.jpeg
Screenshot_20190513-182936.jpeg
Screenshot_20190513-182919.jpeg
Screenshot_20190513-182850.jpeg
Screenshot_20190513-182800.jpeg
Screenshot_20190513-182739.jpeg
 
Nakumbuka pia mara ya kwanza kumsikia Charles Hilary ilikua mechi ya Man U vs Blackburn Rovers. Sijui ilikua mwaka 2001!! Ila ilikua kwenye redio ya mbao ya babu yangu. Enzi hizo za sticker kwenye bublish Michael Owen anatamba sana Ulaya.

Alaisababisha nikawa mshabiki wa Liverpool mpaka leo.
 
''Wapenzi wasikilizaji tunajiunga moja kwa moja na watangazaji wetu walioko uwanja wa Taifa! Watangazaji wetu huko ni Charles Hilali na Ahmed Jongo''! Daah kitambo sana, ilikuwa burudani kuliko laivu ya Baraka Mpenja!
 
Ahamed Jongo
Moira unapigwa maguu 12 ya MTU mzima.
''Wapenzi wasikilizaji tunajiunga moja kwa moja na watangazaji wetu walioko uwanja wa Taifa! Watangazaji wetu huko ni Charles Hilali na Ahmed Jongo''! Daah kitambo sana, ilikuwa burudani kuliko laivu ya Baraka Mpenja!
 
.....Kiberiti bora cha KANGAROO kimethibishwa hapa Tanzania na makasha yake yamejaa kabisa .....
Hiyo ni mwaka ya 199
 
Back
Top Bottom