Enzi za Mpira RTD: Tukumbushane Visa na Mikasa ya wakati huo.

Baada ya taarifa ya habari ya saa kumi kamili jioni tutajiunga na watangazaji wetu waliopo uwanja wa Taifa kukuletea mpambano wa mpira wa Miguu kati ya Simba na Yanga uwanja wa Taifa.
Watangazi wetu huko ni Sued Mwinyi Ramadhani Mnyamwezi wa Tabora na Juma Suleiman Nkamia.
Wathamini wetu ni bia ya Safari larger ,
Nami studioni ni Christine Chokonigela
 
Hamna mtangazaji aliyekuwa mwongo kama Salum Mbonde si kwa uongo ule. Mpira hata upite mita 5 pembeni ya goli utasikia Mogela anakosa hapa sentimita chache.

Goooooooohhh, hapana ni kona
 
Sanif Lazaro
Thomas Kipese
Edward Chumila
Makumbi Juma
Hamis Gaga
Zamoyoni Mogela
Said Mwamba Kizota
Juma Pondamali
..............
 
Enzi hizo ukisikia Dua Dua Dua Dua! tayari ujue ni goli! Au utasikia Said Sued "Scuuuuud"! Hawa viumbe walikuwa ni hatari sana kwenye ufungaji. Siyo siku hizi washambuliaji wetu wanaruka ruka tu uwanjani.

Halafu wakati wa mapumziko utawasikia wadau waliolipia kadi zao za salamu zikisomwa mubashara RTD na mtangazaji ; utasikia " Tate Mkuu, muuzaji maarufu wa ngogwe na sunga akiwa pale sokoni Manundu Korogwe, anaitakia ushindi timu yake ya Yanga goli 2 kwa nunge dhidi ya mikia fc ili warudi huko porini kwenye makazi yao ya kudumu.
 
Baada ya taarifa ya habari ya saa kumi kamili jioni tutajiunga na watangazaji wetu waliopo uwanja wa Taifa kukuletea mpambano wa mpira wa Miguu kati ya Simba na Yanga uwanja wa Taifa.
Watangazi wetu huko ni Sued Mwinyi Ramadhani Mnyamwezi wa Tabora na Juma Suleiman Nkamia.
Wathamini wetu ni bia ya Safari larger ,
Nami studioni ni Christine Chokonigela
Wewe hupishani umri na mm
 
Back
Top Bottom