Enzi za Mkapa wananchi waliona bora magazeti yafungiwe, enzi za Kikwete wakabadili msimamo..

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
2,476
2,000
Wakati Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete anaingia madarakani, wananchi wengi walikuwa wanaona ni sawa serikali kuwa na mamlaka ya kufungia magazeti hasa pale yanapotoa taarifa zenye utata.. Hawakuwa na neno ilionekana kawaida tu..

Nadhani pengine ni athari ya hulka ya Mstaafu aliyemtangulia, Mzee wetu BW Mkapa, ambaye tofauti yake na Ngosha ni kidogo tu ila wote ni 'wakali'..

Nachotaka kusema, pamoja na mambo mengine, inawezekana uelewa wananchi umekuwa ndani ya kipindi cha JK.. Kwamba watu wameelewa zaidi thamani ya Uhuru wa Maoni.

Au ni athari za kisiasa? Kwamba wananchi wengi wamenufaika na upevukaji wa siasa zetu za ndani wakati wa JK? Sina uhakika..

Ninachoamini.. Hizi namba zimeongezeka sio kwa bahati mbaya. Ipo kazi ilifanywa na serikali iliyopita ambayo naamini serikali ya sasa itazidi kuiendeleza kazi hiyo ya kuacha uhuru wa maoni utamalaki kama wananchi wanavyotaka..

Nimechochea? Sidhani..

10.JPG
 
Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,213
2,000
Mzee Mwinyi hakufungia sana Magazeti. Au hayakuwepo? Nadhani shida ipo kwa viongozi, sio mfumo..
Usalama au hatari ya Uhuru wa Maoni inategemea na nani yupo kwenye madaraka, hatari sana hiyo!
 
Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,213
2,000
kule msikitini sheikh akikosea anaambiwa kakosea na hana kinyongo kulipokea hilo la kukosolewa..sijui nyumba zingine za ibada hali ikoje?!
Naamini kwenye kukosoana.. Watu wakosoane vizuri.. Wakosoaji hujipa mamlaka makubwa sana kwa sababu tu wapo sahihi.. Sidhani kama ni sawa.. Usikosoe kwa kutukana wala kuzodoa.. Uvumilivu haufanani baina ya watu!
 
inamankusweke

JF-Expert Member
Apr 24, 2014
6,307
2,000
Naamini kwenye kukosoana.. Watu wakosoane vizuri.. Wakosoaji hujipa mamlaka makubwa sana kwa sababu tu wapo sahihi.. Sidhani kama ni sawa.. Usikosoe kwa kutukana wala kuzodoa.. Uvumilivu haufanani baina ya watu!
ulimwengu alitukana!?hostel hazina nyufa?nchi haikumshinda mchonga!?
 
MISULI

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
7,359
2,000
ulimwengu alitukana!?hostel hazina nyufa?nchi haikumshinda mchonga!?
Mkuu elewa tu kuwa hatuna wakosoaji.tuna wanafki,wafitini,watukana matusi,wadhalilishaji,watafuta kiki za kijinga,wadhandiki na wambea na hawa wote wamejificha chini ya mwamvuli wa wakosoaji.
 
jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
32,581
2,000
Taifa haliwezi kuendeshwa kwa udaku wa media.
Ni hatari sana kuwaachia makanjanja wanaonunulika kirahisi na mafisadi ndio wawe wanatuchagulia ajenda za kujadili.

Piga picha ya Yule jamaa wa elimu ya hapa na pale alivyomtukana Fisadi halafu leo hii yuko kimyaa baada ya kumtetea kwa kishindo.
 
Travic

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
720
1,000
Taifa haliwezi kuendeshwa kwa udaku wa media.
Ni hatari sana kuwaachia makanjanja wanaonunulika kirahisi na mafisadi ndio wawe wanatuchagulia ajenda za kujadili.

Piga picha ya Yule jamaa wa elimu ya hapa na pale alivyomtukana Fisadi halafu leo hii yuko kimyaa baada ya kumtetea kwa kishindo.

Sawa.. Ila iwe kwa kiasi basi..
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom