Enzi za cheo ni dhamana zimeishia wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Enzi za cheo ni dhamana zimeishia wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bishop Hiluka, Aug 12, 2011.

 1. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Nchi hii imeingiwa na ugonjwa mbaya sana wa mmong'onyoko wa misingi ya utawala bora,
  umoja na mshikamano wa kitaifa; maadili na utu wema, jambo linalowatumbukiza walio wengi
  katika umasikini.
  Huko nyuma tulizoea kuambiwa kuwa ‘cheo ni dhamana’ na kwamba ‘uongozi ni utumishi’,
  lakini siku hizi kupata cheo ni kuula! Neno 'kuula' limeanza kama lugha ya mtaani ambayo ina
  tafsiri pana kidogo. Moja ya tafsiri ni 'mambo kuwa mazuri (kunyooka)'.
  Miaka ya hivi karibuni wazo la cheo ni dhamana limepotelea mbali na kusahauliwa kama
  lilivyosahauliwa Azimio la Arusha. Tunawezaje kupata viongozi wazuri kama kila mmoja
  anafikiri nafasi aliyonayo ni haki yake, ni mali yake, na ni stahili yake?

  Zama hizi mtu anaruhusiwa kuwa na kampuni na akajipa tenda ya kutoa huduma ofisini kwake,
  zama ambazo kufikishwa mahakamani kwa ubadhirifu inategemea umekwapua kiasi gani, kama
  ni kikubwa, dola yenyewe inatamka kuwa hukamatiki!  Ni zama ambazo ukiwa mtumishi wa umma mwenye cheo kikubwa unaweza kusomesha mwanao
  nchi yoyote uitakayo bila mawazo ya karo, si hivyo tu kutibiwa nje si kwa magonjwa ya moyo tu
  bali hata mafua, muhimu cheo kizuri cha kuhudumia umma.
   
 2. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Huo usemi uliishia kwa Hayati Nyerere,hauko tena,na sa hivi cheo si dhamana tena.
   
 3. eliakeem

  eliakeem JF-Expert Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 2,920
  Likes Received: 1,028
  Trophy Points: 280
  KWELI KABISA MKULU

  DHANA ZA Cheo ni dhamana iliondoka na JK Nyerere wa Ukweli......ikazikwa kule Zenj walipokuja na AZIMIO LA ZANZIBAR.....na DHANA MPYA IKAWA CHEO NI DILI (UTAJIRI).....NA NDIYO MAANA TANGU WAKATI HUO MTU AKIWA NA CHEO KATIKA NGAZI YEYOTE NCHINI LAZIMA AWE TAJIRI....
   
 4. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Cheo ni Ufisadi!
   
 5. c

  change we need Member

  #5
  Aug 13, 2011
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  cheo sasa ni utajiri! hasa ukiwa mtumishi wa umma na una cheo kikubwa "umeula" sio kama zamani, marehemu Mwalimu ni kama aliondoka na Maadili ya utumishi wa umma kwani fisadi ndio anatetemekewa na serikali na hata viongozi wa juu kabisa wenye dola wanasema hakamatiki! usipoiba nchi hii unachekwa unaonekana *****..na jamii nayo imebadilika ukiiba unasifiwa, mfano jamaa baada ya mradi kaporomosha bonge ya jumba na gari mbili kali..utasikia wananchi wakisema jamaa mjanja! hata kama huo mradi ukidumu kwa miaka 2 hakuna anayejali..
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Aug 13, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Toka enzi ya Mwinyi na Azimio la Zanzibar ambalo liliondoa miiko na maadili ya viongozi, ili kuacha miaya ya conflict of interest ktk uongozi kuwa sii makosa tena ktk nguzo za uongozi bora.
   
 7. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #7
  Aug 13, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Misemo katika jamii huashiria fikra za jamii hiyo. Kwa kutumia na kukubali neno la 'kaula', jamii imehalalisha kitendo cha ubadhirifu na kuwajibika kazini ili mradi tu yule aliyepewa jukumu lile afaidike kwa njia yeyote ile.
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Aug 13, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 180
  mimi nadhani hata kwenye masomo ya menejiment topic ya decision making process imefutwa, ndiyo maana maamuzi hakuna. bila maamuzi sahihi hata neno CHEO NI DHAMANA haina nafasi tena
   
 9. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #9
  Aug 13, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  mwalimu alipokufa amekwenda navyo vyote, yale mafundisho yake watu hawayafuati tena.
   
Loading...