Enzi za CCM ya Nyerere - Lowasa, Mramba,MAKAMBA,YONA WOTE BAKORA 12/12 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Enzi za CCM ya Nyerere - Lowasa, Mramba,MAKAMBA,YONA WOTE BAKORA 12/12

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 10, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,586
  Likes Received: 5,772
  Trophy Points: 280
  Enzi za CCM ya Nyerere Lowasa, Mramba na wenzao wangetimuliwa[​IMG]Salim Said na Hashim Gulana

  CHAMA Cha Mapinduzi kingekuwa na nidhamu yake ya zamani watuhumiwa wote wa ufisadi pamoja na wabunge wanaotoa lugha chafu kwa wenzao, wangekuwa nje ya Chama", ilielezwa jijini Dar es Salaam jana.

  Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Kitengo cha Sayansi ya Siasa na Utawala cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Benson Bana, alipozungumza na waandishi wa gazeti hili.

  Akizungumza ofisini kwake jana, Dk Bana alisema nidhamu ndani ya CCM imeporomoka na kusababisha baadhi ya wabunge kuanza kushambuliana kwa mambo ya faragha binafsi badala ya yale yenye maslahi ya umma.

  “Nidhamu ndani ya CCM imeporomoka; kinadharia na kivitendo, zamani kulikuwa na kuheshimiana ndani ya Chama, lakini sasa hakuna tena kuheshimiana wala kufichana,” alisema Dk Bana na kuongeza:

  “Kama hii ni CCM tuliyoielewa zamani, basi wakina Edward Lowassa, Nazir Karamagi, Ibrahim Msabaha, Andrew Chenge, Rostam Azizi, Daniel Yona na Basil Mramba, wangekuwa wamebaki kuwa wapiga kura tu”.

  Dk Bana alifafanua kuwa wabunge hao walioguswa na tuhuma mbalimbali za ufisadi na ambao pia walikuwa mawaziri serikalini, wangekwishavuliwa uwaziri, ubunge na hata ujumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec), bila ya kuwaonea huruma.

  “Wakina Karamagi, Lowassa, Msabaha na Rostam wana mkakati wa kujisafisha mbele ya umma wa Watanzania na hii ni kwa kuwa adhabu waliyopewa ni ndogo kwa sababu CCM haina dhamira ya kweli,” alisema Dk Bana.

  “Watu kama hawa si wa kutamba tena bungeni, lakini kwa sababu wana nguvu na ushawishi ndani ya Chama ndio maana unaona hata katika vikao vya NEC, mashambulizi huelekezwa kwa wale wanaopambana na ufisadi,” aliongeza.

  Alisema viongozi hawana maadili kwa kuwa wamekuwa wakizungumza maneno ambayo kimsingi hayapaswi kusemwa na kiongozi wa umma.

  “Kinachoonekana hapa ni ‘erosion of ethics’ mmomonyoko wa maadili, maneno kama yaliyosemwa na Waziri wa Utawala Bora Sophia Simba au Samuel Malecela katika malumbano yao hayapaswi kusemwa na viongozi,” alisema Dk Bana na kusisitiza:

  “Maneno yao machafu hayawakilishi CCM bali ni tabia ya mtu binafsi na kama ni enzi za Mwalimu Julius Nyerere wangekosa nyadhifa zao”.

  Lakini Dk Bana alisema kwamba, malumbano hayo yanampa fursa Rais Jakaya Kikwete kujifunza na kutafakari namna na aina ya viongozi aliowateua katika serikali yake.

  “Lakini pia wananchi wanapata kujua aina ya viongozi wanaowaongoza, pia kwa sababu nchi yetu haina mkakati wa elimu ya uraia, basi malumbano haya yanawapa fursa ya kufanya maamuzi katika uchaguzi ujao”.

  Kuhusu sakata la wabunge kuchukua posho mbili, Dk Bana alisema suala hilo ni zito na kwamba anawashangaa Spika Sitta na Mbunge wa Kyela (CCM) Dk Harrison Mwakyembe, kwa kujibu maswali kuhusu sakata hilo kama watu ambao hawana elimu ya sheria wakati ni wanasheria.

  Alisema cha kusikitisha zaidi ni kwamba, wabunge hao wamekuwa wakichukua posho mbili kwa muda mrefu tena bila ya kuzilipia kodi, ilihali mishahara midogo ya watumishi wa umma inakatwa kodi.

  “Kama ingekuwa wanalipia kodi ingekuwa afadhali lakini hata kodi hawalipi, wanapaswa kupewa deni la kulipia kodi tangu walipoanza kuchukua posho mbili. Unafikiria ni kiasi gani cha fedha ambacho kimepotea kama utaratibu wa posho mbili ulikuwapo tangu 1970s,” alihoji Dk Bana.

  Alisema kuna makundi mawili ya wabunge wa CCM; la kwanza likiwa lile linalotuhumiwa kwa kufanya ufisadi na la pili ni linalotuhumu na kupambana na ufisadi huo.

  “Katika kundi la pili kuna watu kweli wamejitolea kupambana na ufisadi, lakini kuna baadhi yao wanapiga kelele kwa sababu wao hawakupata fursa ya kufanya ufisadi.

  Hivyo lazima tuwatambue ili wasitupelekeshe, Mwakyembe anadaiwa kumiliki kampuni ya kufua umeme kwa njia ya upepo,” alisema Dk Bana.

  Kuhusu tuhuma na madongo waliorushiwa wabunge wanaojiita vinara wa kuapambana na ufisadi, Dk Bana alisema, “Sisi tunaona hizo ni hisia tu, lakini ‘tunaamini kuwa hisia hizo ni za kweli hadi hapo wahusika watakapokanusha kwa kutoa ushahidi na sio kutuhumu zaidi”.

  “Kama waziri Simba anasema ndoa ya Anne Kilango na Malecela ilifadhiliwa na Jetuu Patel na kwa kuwa ndoa hiyo ipo kweli, wahusika sasa waje watuambie kwamba walitumia kiasi gani cha fedha, walipozitoa, waliochangia na kama Patel yumo au hayumo katika orodha, kwa sababu ndoa za siku hizi tunazijua ni za ‘fund rising’ yanani michango, aliongeza. Hivi karibuni kumekuwa na malumbano makali baina ya wabunge wa CCM, ambapo mashambulizi ya moja kwa moja kutoka kwa mbunge kwenda kwa mbunge mwengine yamekuwa yakitumika, kufuatia Kamati ya Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi kuanza kukusanya maoni kuhusu tofauti za ndani ya Chama hicho.
   
 2. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Hili lingeanza na JK ndo wafuate wa chini yake.
   
 3. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Posho mbili ndio utaratibu uliopo kwenye ofisi zote za Serikali hasa kwa wakubwa wanaposafiri hupewa per diem na ofisi zao na wanapofika kwenye mikutano wanapokea pia fedha kutoka kwa waandaaji mikutano. Kwa hiyo kuwasakama Wabunge kwa jambo hilo ni kuwaonea tu. Ni mfumo mzima uliooza!
   
 4. f

  friendsofjeykey Senior Member

  #4
  Sep 1, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i hate to agree with you
   
Loading...