Enzi za Augustino Lyatonga Mrema kusaidia NCHI, yuko wapi??? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Enzi za Augustino Lyatonga Mrema kusaidia NCHI, yuko wapi???

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fikirikwanza, Jul 12, 2012.

 1. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nakumbuka enzi za Mrema kusaidia nchi kusafisha wezi, majambazi, wazembe kazini, boss akichelewa kazini anakuta kiti kimechukuliwa, enzi za kutoa siku saba, alitusaidia kiasi kuwa rais mwinyi akajichanganya akampa unaibu waziri mkuu; enzi za wizara ya mambo ya ndani ni kila kitu, ndo mambo ya ndani hayo; wenzake walilalamika kuwa anaingilia wizara zao, mwinyi akatafuta jibu, japo alivunja katiba.

  Huyu Mrema, ambaye alikuwa mtetezi wa wanyonge, shujaa ktk kupinga wizi wa mali ya umma, aliyekamata dhahabu dar airport, aliyewapeleka puta wanyanyasaji wa kijinsia, huyu mrema tuliyemuona tegemeo la watanzania ambaye ndo mpinzani aliyeweka record ya kupata kura nyingi za urais over 35%, huyu mpambanaji yuko wapi??? anafanya nini??? nondo zake kapeleka wapi???? tumsaidieje arudi kutumikia taifa kama hapo mwanzo??? alitusaidia kipindi fulani labda sasa anahitaji tumsadie.

  Mbona nchi iko ktk kipindi kigumu yeye akiwa kimya, CCM imenyamazisha??? Sio mtu wenye maono tena na uwezo wa kupambana, amechoka kiakili na mwili? mbona hajaaga watanzania?

  Nawasilisha
   
Loading...