Enzi hizo: Radio ya Kiswahili ya SA dhidi ya Radio za Ukombozi

Bandiwe

JF-Expert Member
Oct 19, 2013
9,530
3,556
Nakumbuka miaka ya 70's wakati Frelimo inapigana na Mreno zile nyimbo za ukombozi zikivuma !
Nakumbuka enzi ya miaka ya 80's wakati ANC na PAC kupitia Redio Tanzania External Service, wakipeperusha matangazo yao ya propaganda kuhusu ukombozi wa South Africa. Kipindi huanza kwa bundiki ya rasha rasha ya Kalashnikov ikirindima huko mtangazaji akirepu maneno makali ya hamasa.
Hii iliwalazimisha serikali ya Makaburu kuanzisha Radio SA kwa ajili ya kurudisha propaganda za ANC na PAC.
Ilikuwa ni Redio ya Burudani na kutumiana salaam. Mtuma salamu maarufu wa Babati Zakaria Ndenfoo akipaishwa hewani wakati wote.
Je redio hii bado ipo kweli ? Kuna redio yeyote ya Kiswahili SA !?
 
Hakuna radio ya kiswahili SA na wamesahau kabisa kwamba watanzania waliwasaidia no baadhi Sana wanaokumbuka
 
Hawa jamaa wa SA hawana shukrani. Walikuwa wanawafukuza hata kuwaua watanzania kule kwao,kisa ajira.
 
Huyu mtuma salamu bado namsikia redio za huku kaskazini,ila hiyo idhaa hasikiki huku,sijui wanarusha matangazo yao kwenye masafa gani.
 
Hakuna radio ya kiswahili SA na wamesahau kabisa kwamba watanzania waliwasaidia no baadhi Sana wanaokumbuka
Hiyo Redio ilikuwa ya Serikali ya South Africa ikijaribu kuwafutia watu wa Afrika Mashariki. Najiuliza tu ile hamu yao ya kutumia Kiswahili huku wakiamini kina nguvu imeenda wapi !?
 
Nimeupenda huu uzi kwani umenikumbusha hawa watangazaji wa RSA akina Duncan Kandawire, Francis Chandiona, William Jeranje na Boston Calleja Kaunda. Kama sikosei hawa wote hawakuwa watanzania lakini walikuwa wakitiririka kiswahili utadhani wazaramo.

Nilikuwa mmoja wa wanachama wa idhaa ya kiswahili ya radio hiyo na kila mara walikuwa wakinitumia barua ndani yake kukiwa na picha za hao watangazaji na habari mbalimbali zilizohusu hiyo idhaa yao.
 
Mbali na habari na vipindi vya salaam, Radio SA pia ilikuwa na kipindi cha maswali na majibu. Wasikilizaji walikuwa wanatuma maswali kwa barua ambayo yalikuwa yanajibiwa studio. Siku moja miaka ya 70 kuna msikilizaji aliuliza, "Kwa nini kuna ubaguzi wa rangi SA?" Jibu: "Hakuna ubaguzi wa rangi SA isipokuwa kuna sera ya kutenganisha mababila ambayo imekuwa na mafanikio makubwa kwa kuleta maendeleo ya haraka."(!!)
 
Back
Top Bottom