Enyi wazazi kuoza binti yako na mahali kubwa mnafikiriaje?

Me too

JF-Expert Member
Feb 9, 2015
7,377
9,297
habarini humu ndani?
moja kwa moja kwenye mada tafadhari!
Ewe baba / mama ulikimbia majukumu ya kulea mpaka binti yako kapata kazi ndio unakuja kujitambulisha ili akupe walau robo ya mshahara wake unajisikiaje ufanyapo ivo?
binti amepata mchumba anataka afunge ndoa unaweka kizingiti ndoa isifungwe mpaka mahali ilipwe mil 5 wakati huohuo amuoae amemlea kwa kumsomesha chuo hadi kazi kampatia bado unakuja juu kudai mahali kubwa na wakati ulikimbiamajukumu yako na kijana wa watu akayabeba.
leo hii unajitokeza kwenye mahali kubwaaaaa.

msiwape wakati mgumu vijana wenu.
mtafakari mngekuwa ni nyie ndio waoaji /waolewaji mngejisikiaje?


***ni wazo tu***
 
Kashamueka binti yake kitega uchumi huyo!!!

Kuna sababu nyingi zinachangia wazazi kufanya hivyo...

1. Wana ule utamaduni ya kua mtotowa kikeananunuliwa... Yaani wanamfanya kitega uchumi, njia ya kuondoka umasikini.

2. Hawamtaki huyo mwanaume kwa sababu moja au nyingine, kwahiyo wanafanya komoa.

3. Kuna wale wazazi hawataki mtoto wao aolewe... Hii ipo sana kwa wanaoishi na wazazi wa kambo au walezi. Wivu tu kua mdada anaolewa...

4. Pride/majivuno. Unaona binti yako ni bora sana au umemgharamia sana ko unataka kuweka kiwango cha juu kuoneaha kua binti yako ni wa hadhi ya juu.

Sijui kwanini wazazi wanafanya hivi kwa kweli!!! Sio haki kabisa. Mahali iwe kiwango kidogo cha kuonesha shukrani kwa wazazi... Isiwe ishu kumfanya mkaka ajhtie maamuzi.
 
Gharama walizotumia kumlea ni kubwa
hujaelewa nimezungumzia mzazi aliekimbia majukumu ya kulea bint akapata mpenzi na mpenzi huyo akamuahidi atamsomesha chuo hadi kumtafutia ajira amesha mtafutia yote hayo ni jasho la mpenziwe.

inapokuja swala la kuonesha wazazi mzazi alie kataa kukusomesha ndio anakazania uolewe kwa mahali mil 6±±
je huoni ni ukandamizaji?ء
 
Dah mleta mada umenikumbusha juzi tu mkasa huo umempata jamaa yangu, story iko hivi;

Jamaa yangu alikuwa ana mpenzi wake sasa dada huyo akamwambia jamaa akajitambulishe kwao, jamaa akaona hamna shida akaenda kujitambulisha

Sasa cha kushangaza mama mtoto akawa na furaha binti yake kuleta mchumba ajitambulishe cha ajabu baba mtoto akawa mkali wakati wa utambulisho.

Maswali yakawa mengi mara unafanya kazi gani kwa ukali mara ninavyokuona huna sifa ya kuoa binti yangu bac kukawa na tafrani kiaina

Binti akaanza kulia anamwambia baba yake akikataa aolewe na jamaa bac atakunywa sumu. Mama akawa anapoza mambo

Sasa mzee mwenyewe anayeongea upupu wote huo kwanza hajaenda shule, ni mlevi hatari, maeneo yake yote kayauza yaani dah!

Bac jamaa akaniambia tuondoke maana hawezi kuvumilia kudhalilishwa na mzee kama yule

Kesho yake mama yake binti akampigia cm jamaa na kumwambia atulie awe mpole mke atapata shida ni mzee maana kumbe alishachukua hela kama kianzio kwa mshkaji mmoja 300,000 bila mama kujua wala binti, pia binti hamfahamu hata huyo mchumba baba yake anayemtaka kwa kuwa ameshakula hela yake

Sasa jamaa ndio akaniambia mzee kama shida yake ilikuwa hilo deni angetuambia , tungempa hiyo hela ya deni then atupangie mahari.

Sasa binti kakosa mchumba kisa ulafi wa baba yake. Sasa tumeamua kuhamishia majeshi kwa mwingine, hatupendagi ujinga na usumbufu usio wa lazima
 
Ukisema gharama zilizotumika kumlea ni kubwa kwani kijana wa kiume huwa halelewi kwa gharama?, huo ni ulimbukeni wa wazazi na mila potofu
Nw kuona ni biashara huria ukiona bei tafuta mwingine wa bei nafuu
 
Nw kuona ni biashara huria ukiona bei tafuta mwingine wa bei nafuu
Siku hizi wanaume wengi wala hawapati shida wazazi wa mke wakikomaa na mahari kubwa unampiga chini binti yao akae nao, Mara binti anaanza kulia na wengine wanachangia na wao mahari ili wafanikishe kuolewa. Chezewa kuolewa usawa huu.
 
Back
Top Bottom