Congo
JF-Expert Member
- Mar 13, 2008
- 2,064
- 2,301
Nimekuwa nikisikiliza mambo mengi yahusuyo madai ya Wazanzibari kudai nchi yao. Wakitaka muungano ujadiliwe na ikiwezekana zaidi uvunjike. Mimi nawashauri jambo moja la ziada, daini pia ushiriki wa nchi yenu (Zanzibar) kama nchi kamili ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Sababu yangu ni kuwa, kulingana na mchakato wa Shirikisho la Afrika Mashariki kuna uwezekano wa mambo yaleyale ambayo Tanganyika na Zanzibar imeungana nayo yakawa ndio hayohayo yatakayokuwa mambo ya muungano wakati wa shirikisho. Mambo kama ulinzi, mambo ya ndani, fedha, forodha, mambo ya nje n.k. yanaweza kuwa ndio yatakayokuwa mambo ya muungano wa Shirikisho la Afrika Mashariki. Ikiwa hivyo umuhimu wa muungano wetu wetu hautakuwepo utakuwa ni ujirani kwa kuwa Waziri wa ulinzi atakuwa wa Shirikisho na sio wa muungano hivyo mambo tuliyoungana nayo yatakuwa yanaongozwa na Shirikisho. Nawashauri Wazanzibari watafakari wadai kiti chao ndani ya Jumuia ya Afrika Mashariki kama nchi kamili.