Enyi watawala wetu,hili la watoto wetu kufeli halafu walimu wanashangilia mnalichukuliaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Enyi watawala wetu,hili la watoto wetu kufeli halafu walimu wanashangilia mnalichukuliaje?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Chatumkali, Jan 10, 2012.

 1. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #1
  Jan 10, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ilikuwa piga nikupige kati ya mwanasiasa John Komba na walimu wa Mbinga.Mh aliwajia juu walimu kwa kushangilia watoto wetu kufeli mtihani wa drs la saba.Walimu nao wakajaribu kutunisha misuli wakanywea!Hivi serikali imejaribu kujiuliza kwanini watoto wanafeli halafu walimu wao wanaangusha shangwe kama ya harusi?Hapa tatizo ni nini?Ni kwanini tumefikia mahala sasa watanzania wanashangilia pindi wanapopata matokeo HASI?

  Majuzi tulishuhudia mashabiki wa soka wanashangilia Kilimanjaro stars kufungwa!Sasa walimu wanashangilia vijana kufeli!Nachelea tusifike mahali madaktari nao wakashangilia wagonjwa wakifa,askari wa usalama barabarani nao wakashangilia ajali zikitokea,polisi wakashangilia wakitorokwa na mwizi,JWTZ wacheze sebene nchi ikivamiwa na ikitokea wakulima nao wakasherehekea kwa mvua kutokunyesha basi tujue kiama cha nchi kimefika.Watawala mtafakari na mchukue hatua maana ni dhahiri kuna kitu hakipo sawa.KAZI KWENU!
   
 2. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #2
  Jan 10, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  ...mbona nmechangia kwenye hii post laki mchango wangu umepote ktk mazingira ya kutatanisha.Mods vp umeanza utaratibu gani tena?,au unaogopa kutwa mchochezi?.Nasubiri jibu lako,kama ni vp tupe naomba mwongozo...
   
 3. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #3
  Jan 10, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,184
  Trophy Points: 280
  Inawezekana walimu wanatuma ujumbe kwamba "Mnatunyanyasa na kutulipa vibaya, mnatucheleweshea hata hiyo mishahara midogo, hamtupi zana za kufundishia, huku mnapandishiana mishahara wenyewe, haya ndiyo matokeo yake"
   
Loading...