Omela Odongo
Member
- Mar 26, 2021
- 47
- 66
Nawasalimia Wana jf wote nikitumai mu wazima na weekend hii tulivu. Mimi ni member mpya katika jukwaa hili kwa kuandika na kuchangia maada lakini nimeanza kuichungulia Jamii forum tangu mwaka 2010.
Niende kwenye maada moja kwa moja, nimekuwa nikisoma maada humu kwenye jukwaa za kuwakejeli hawa wanaoitwa "Single mother" na kadiri siku zinavyozidi maada hizi zinaongezeka kuna uwezekano hata wao wanaongezeka kila kukicha. Sasa swali la kujiuliza ni nani anayesababisha hali hii kuongezeka kwa kasi namba hii?Je wanazaa peke yao? Kwa nini wanaume muwazalishe wanawake(mabinti)halafu muwatelekeze na kisha muanze kuwasimanga kwa kiwango hiki tunachokishuhudia nyakati hizi.
Wanaume kama mumeamua kuwaita single mothers basi na wanaume mliowazalisha mnatakiwa kuitwa single fathers kama wasivyoaminika kama wakiolewa hata ninyi pia humuamiki kwenye ndoa na huu ni ubaguzi wa hali ya juu na roho mbaya kutoka kwa wanaume unaofanana na kisa hiki:.
John 8:3-11 Waandishi na Mafarisayo wakamleta mwanamke aliyefumaniwa katika uzinzi,wakamweka katikati.Wakamwambia mwalimu, mwanamke huyu amefunaniwa alipokuwa akizini.Basi kwa torati,Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake namna hii, nawe wasemaje?.............
Mwanaume aliyekuwa akizini naye aliachiwa huru Ila mwanamke alitakiwa kupigwa mawe.Sasa tujiulize mwanamke alikuwa anazini peke yake? Kwanini kwa mwanamke ni kosa lakini so kwa mwanaume?Enyi wanaume acheni kuwapiga mawe wanawake wakati ninyi ndio mnaowazalisha.