Enyi Wake Watiini Waume Zenu Ebo!

capuchino

Member
Jun 27, 2008
47
0
Ndugu Zanguni Tunarudi Tena Na Somo Kwa Wale Mabinti Wanaoolewa Au Waliioolewa,,jamani Hakuna Starehe Kama Mme Kujua Mkewe Anamtii Na Kumheshimu......kumekuwa Na Wanawake Wengi Ambao Hivi Sasa Wanajua Ndoa Ni Kazi Na Pesa Na Si Mapenzi Tena Na Hili Nimeona Limehangaisha Wengi Sana Na Ndoa Zao Kuaribika,,,
Ewe Mwanamke Ukiolewa Ujue Mumei Ni Kichwa Si Boyfriend Huyo
Unakuta Mmeoana Mwanamke Anakuuliza Kama Umeshindwa Achia Ngoma Wenzio Wahangaike Nayo/1111jamani Kama Ulikuwa Unajuwa We Parking Ya Tbs Pale Posta Ukifika Saa Moja Sh 300/=.....kwa Nini Ulikimbilia Kanisani Au Msikitini..embu Jaribuni Kuacha Kucheza Na Maisha Waume Kwa Wake!!!!nimekuja Na Wanawake Leo Maana Wamekuwa Wakichangia Sana Hivi Karibuni Kuaribu Kama Si Kuvunja Ndoa...na Kuacha Watoto Wakiangaika!!!!!!

Ewe Mwanamke Kama Auko Tayari Kuolewa Acha Nasema Acha..ashura Kaamua Usilazimishe Ili Uonekane Sauri Yako!!!!!

Capuch-wakunesa
 
na wanaume jifunzeni destruri za kuishi na wanawake ... mwanamke ni binaadamu pia si kifaa au mali ya kumiliki ukaichezea unavyotaka ... kuweni nanyii wastaarabu pia na kuweni karibu na wake au familia zenu ili muweze kugundua na kutatua matatizo kwa pamoja ... wengi wenu mnakimbilia nyumba ndogo badala ya kutatua matatizo yenu ya ndani kwanza.

Wanaume ndiyo hukimbia watoto si wanawake ... ukiona mwanamke kamwacha mtoto ujue mwanaume kamemgangania sana na kutamba kwamba anaweza kumtunza... ila kitendo cha kumtenganisha mama na mtoto sisi wanawake hujisikia kama mtu kakuchoma kisu rohoni kwani huwa tunaamini hamna anaeweza kuwa mama mbadala isopokuwa in cases za kifo tu
 
Ndugu Zanguni Tunarudi Tena Na Somo Kwa Wale Mabinti Wanaoolewa Au Waliioolewa,,jamani Hakuna Starehe Kama Mme Kujua Mkewe Anamtii Na Kumheshimu......kumekuwa Na Wanawake Wengi Ambao Hivi Sasa Wanajua Ndoa Ni Kazi Na Pesa Na Si Mapenzi Tena Na Hili Nimeona Limehangaisha Wengi Sana Na Ndoa Zao Kuaribika,,,
Ewe Mwanamke Ukiolewa Ujue Mumei Ni Kichwa Si Boyfriend Huyo
Unakuta Mmeoana Mwanamke Anakuuliza Kama Umeshindwa Achia Ngoma Wenzio Wahangaike Nayo/1111jamani Kama Ulikuwa Unajuwa We Parking Ya Tbs Pale Posta Ukifika Saa Moja Sh 300/=.....kwa Nini Ulikimbilia Kanisani Au Msikitini..embu Jaribuni Kuacha Kucheza Na Maisha Waume Kwa Wake!!!!nimekuja Na Wanawake Leo Maana Wamekuwa Wakichangia Sana Hivi Karibuni Kuaribu Kama Si Kuvunja Ndoa...na Kuacha Watoto Wakiangaika!!!!!!

Ewe Mwanamke Kama Auko Tayari Kuolewa Acha Nasema Acha..ashura Kaamua Usilazimishe Ili Uonekane Sauri Yako!!!!!

Capuch-wakunesa

...dah, mkuu leo kweli umeamka mkali sana :D

...Unajua Hasira Za Asbh,,
Ukiangalia Nimenymwa Unyumba Asb Kisa Kushelewa Usiku'
Jf Wakanikumbusha Machungu Nikaamua Kupombeka Nao

Jf Wastaarabu...

...wikiendi njema!.
 
Sawa mume kichwa,
Kama je mume mwenyewe kichwa cha mwendawazimu?
 
Kweli kabisa..mimi naona vyanzo vingi vya ugomvi maranyingi husababishwa na heshima kupotea.... mimi binafsi naona Heshima ndio mchawi mkubwa kwa ndoa zetu.....na hata bibilia ilisema enyi wanawake watiini na muwaheshimu waume zenu..lakini wanafanya kinyume na hapo ndipo sir god anapotoa adhabu ya kukiuka maandiko yake........ugomvi kila siku'' hata uende kwa mganga..dawa ni moja tu....tii na muheshimu mumeo hata kama ni kichwa cha nini sijui we muheshimu tu..afurahi nyumba iwe na amani
 
Mimi ni mwanamume ila story ya kwamba mwanamke amuheshimu na mumewe ni old time.Na wewe mwanamume muheshimu mkewe na kila mmoja atimize wajibu wake kwenye familia tuache 'upapa' wa kijinga hizi ni enzi mpya mambo ya kwamba baba's word ndio final word its crap wanawake need say as well.
 
Heshima kwa mungu kwanza, kisha kila mtu atajua wajibu wake ktk ndoa. Hamna uadilifu na heshia ya upande mmoja!!!!!
 
Wake wawatii waume zao tu hata kama wanataka kwenda kinyume?????!!!!!
Inabidi WAKE NA WAUME WAHESHIMIANE, wakishamaliza WAPENDANE, wakishamaliza WASAIDIANE na KUSHIRIKIANA na mwisho wa siku WAJENGE FAMILIA IMARA
 
Siri ni kutafuta mwenzi unayeweza kumuheshimu na kuheshimu maamuzi au mapendekezo yake.
Kama unatabia ya kutokupenda waendao disco, wapendao vipodozi, au wanya pombe, au masikini, au wasiosoma, au dini fulani, basi ukiwa nae nyumbani ni balaa tupu, usitegemee kumbadilisha.
Jinadae kumsikilza na kumuacomodate kwa h eshima na taadhima.
kama hauko tayari jiandae kuitwa mwenye gubu, wivu, mkosaji wa heshima, mwenye dharau etc.
 
Wake wawatii waume zao tu hata kama wanataka kwenda kinyume?????!!!!!
Inabidi WAKE NA WAUME WAHESHIMIANE, wakishamaliza WAPENDANE, wakishamaliza WASAIDIANE na KUSHIRIKIANA na mwisho wa siku WAJENGE FAMILIA IMARA

Well Mama hebu tutafakari wote. Hivi hii sentensi kwenye biblia na hata Koran ina maana gani. Kwa nini ilisemwa hivyo, au nini kilitokea hadi ikapelekea hii.
Inawezekana zamani hizo wanawake walianza tabia ya kutowaheshimu waume zao. MY TAKE.....

Wanawake wana tabia ya kupenda viwango vya juu ,na ndio natural characteristics yao kwa upande huo. Mwananume asipoweza kuvifika anaoneakana weak , na ndio maana hawachi kuwasengenya waume zao wakiwa masalooni wakisuka nywele hadi leo. Girlfriend wa zamani anakutana na wewe leo baada ya kuolewa na mtu ambaye ana kiwango pungufu kuliko chako.Na atanza kuuliza hivi ni kwa nini sikuolewa na wewe tena ? Anaonyesha kujuta. Ukiendeleza topic atakupa failure side ya mumewe na at that point utagundua anamdharau kwa hilo. Hapa wanaume toeni facts ,kama niko wrong say it openly.

Hili ndilo Mungu hataki wanawake wafanye. Wale wanaopinga hili ndio wanaleta balaa, na ndio hao wanaokimbizana na wanaodhani wanaviwango kumbe ni mafisadi tu na viwango vyao ni vya muda mfupi. Baadae wanaachika na kumsukumia mwanume sababu tele za kuachika kwake ,kumbe sababu ni hiyo tu. Heshima.

Na ole wao wabadilishao maneno ya Mungu kwa akili na sababu za kidunia.
 
Kweli kabisa..mimi naona vyanzo vingi vya ugomvi maranyingi husababishwa na heshima kupotea.... mimi binafsi naona Heshima ndio mchawi mkubwa kwa ndoa zetu.....na hata bibilia ilisema enyi wanawake watiini na muwaheshimu waume zenu..lakini wanafanya kinyume na hapo ndipo sir god anapotoa adhabu ya kukiuka maandiko yake........ugomvi kila siku'' hata uende kwa mganga..dawa ni moja tu....tii na muheshimu mumeo hata kama ni kichwa cha nini sijui we muheshimu tu..afurahi nyumba iwe na amani

Ungemalizia pia agizo... walipoambiwa enyi wake watiini waume zenu..wanaume nao waliagizwa..muwapende wake zenu!!...Heshima si ya upande mmoja.....wanaume nao wangewapenda wake zao..obviously wake nao wangewatii vilivyo... na hii ipo dhahiri.Wanawake wanaopendwa huwaona waume kuwa ni more than waume..huwaheshima na kuwaenzi kwa kila namna!..Tatizo ni kwamba ndoa nyingi zimejaa dharau ( nyumba ndogo, mahawara, watoto wa nje kila kona, vipigo,na mateso ya kila namna) hakuna upendo, kilichotawala ni karaha, gubu, lawama,matusi..... the list is long.Wanawake nao wamejifunza kukomaa nao. Ndio maana with every action from men/husbands women react..Hapo utashangaa kuwa heshima imepungua?
Jamani wanaume wapendeni wake zenu muoje pepo hapahapa duniani.Vinginevyo itaendelea kuwa hell..na hell ya kweli bado yangoja kuwameza.
 
Hii heshima inayoongelewa hapa nafikiri ni ya kuhakikisha kila mmoja hamkwazi mwenzake kwa maneno au matendo. Kama mwanamke anatakiwa awe na heshima kwa mumewe then mwanaume vilevile anastahili kurudishia heshima aliyopewa kwa kumheshimu mkewe!!!

Katika maisha ya ndoa dharau nyingi hutokana na
> Yeyote katika ndoa kutokuwa muaminifu ni dhahiri atakuwa anamdharau mwenzi wake
> Kama maamuzi katika ndoa yatafanywa na mtu mmoja bila kushauriana na mwenzake basi hapa pia itakuwa ni dharau
> Kuficha matukio au habari zingine ili mwenzi wako asizijue pia ni dharau

Ni bora wote tuamininiane na kupeana heshima inayostahili kama wanadamu, na pili kama watu wenye mahusiano ya kimapenzi (ndoa)!

Heshima mbele
 
Wake zetu tunawapenda sana ila hawajui. tatizo wanawake huwa wakisha pata watoto hupunguza upendo kwa waume zao, pia huanza kuwanyika TENDO LA NDOA ambalo nidyo msingi wa ndoa. Mume akishoka kuomba na kubembeleza hutafuta sehemu ya kujihifadhi ili kupunguza matatizo ya nyumba-kama atapewa tendo la ndoa sawa asipopewa hakuna matata. Mke akijua ndiyo huanza mara oh mume hajatulia.
Watu wengine nao wakijua na kwa vile hawajui chanjo basi mume ataonekana mbaya PENGINE mke ndo atakuwa anatoa mara mmoja kwa miezi mitatu.

Jamani chanzo nini hapo??? kwanini watu wanapenda kuangalia "manifestation" badala ya kuangalia na kumlaumi 'source' ya tatizo????

Kina mama kama mnaona TENDO LA NDOA SILA MSINGI UMEOLEWA KUFANYANINI? KWANINI UTOKE KWENU KWENDA KWA MUME?? NINI MAANA YA MUME? KWANINI MUMEO ASIWE KAKA YAKO AU BABA YAKO?
 
Last edited:
Mimi ni mwanamume ila story ya kwamba mwanamke amuheshimu na mumewe ni old time.Na wewe mwanamume muheshimu mkewe na kila mmoja atimize wajibu wake kwenye familia tuache 'upapa' wa kijinga hizi ni enzi mpya mambo ya kwamba baba's word ndio final word its **** wanawake need say as well.

Hata ujifanye una busara kiasi gani kamwe huwezi kuibadili kauli ya Mungu juu ya mwanadamu. Labda pengine hatujui nini Mungu alimaanisha aliposema 'Enyi wake watiini waume zenu'. Hakuna agizo la Mungu kwa mwanaume kumtii mke wake. Naomba nikubandikia waraka kutoka 1Petro 3:1-7

"Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu, ili kama wako wasioamini lile Neno, wapate kuvutwa na mwenendo wa wake zao pasipo neno, 2kwa kuuona utakatifu na uchaji wa Mungu katika maisha yenu.

3Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi.

4Badala yake kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa ndani, kwa uzuri usioharibika, wa roho ya upole na utulivu, ambako ni kwa thamani sana machoni pa Mungu.

5Kwa kuwa hivi ndivyo walivyokuwa wakijipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu. Wao walikuwa ni watiifu kwa waume zao,

6kama Sara alivyomtii mumewe Abrahamu, akamwita ‘bwana.' Ninyi ni watoto wa Sara kama mkitenda yaliyo mema na bila kuogopa jambo lo lote.

7Vivyo hivyo ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili, nanyi wapeni heshima mkitambua ya kuwa wao ni wenzi walio dhaifu na kama warithi pamoja nanyi wa kipawa cha thamani cha uzima, ili kusiwepo na cho chote cha kuzuia maombi yenu.
"

Huo mstari wa saba unamuelezea mwanamke kama kiumbe mdhaifu. Lakini unataka pia AHESHIMIWE. Lakini ni nini basi maana ya UTII.

Pamoja na heshima utakayopata toka kwa mumeo, bado wewe mwanamke una wajibu wa kumtii mume wako. UTII ni rejeo la kauli ya Mungu bustanini. Tazama Mwanzo 3:16 'Akamwambia mwanamke, "Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala"'

Utaona kuwa UTII upo katika mamlaka zaidi. Na neno UTII mara nyingi kwenye Biblia limeambatanishwa katika mazungumzo yanayohusu Mamlaka.

Kinachotusumbua leo ni HARAKATI ZA MWANAMKE KUWA SAWA NA MWANAUME. Heshima ya ndoa imepotelea hapa na wanawake waamekengeuka kiasi wanashindwa kuelewa nini wanataka. Kauli ya Mungu haikuwa peke yake. Upo ushahidi wa Kibaiolojia kuwa uwezo wa mwanamke wa kufikiri ni mdogo kulinganisha na mwanaume.

Mimi huamini kitu kimoja. Amri waliopewa wanaume ni ngumu kuliko agizo walilopewa wanawake. Hebu itafakaraki hii kauli 'nanyi waume, wapendeni wake zenu'.
1. Ukimpenda mkeo, utajitoa kwake
2. Ukimpenda mkeo, utamuheshimu
3. Ukimpenda mkeo, utamthamini
4. Ukimpenda mkeo, utamuongoza katika njia iliyo njema
5. Ukimpenda mkeo...........n.k, n.k

Lakini utatoka wapi upendo wa kumpa mwanamke anayeshindana na kutaka kuwa sawa nawe hata akasahau nafasi yake katika ndoa. Wapo wanawake wanaodhani kuwa kushindana na mwanaume ndio ushindi katika ndoa. Si haiba ya mwanamke kuwa mshindani kwa mwenzi wake wa ndoa ambaye ana jukumu la kumtunza na kumlinda. Ndoa yenye heshima ni zao la wanandoa wenye kujua wajibu na mipaka yao. Hata hivyo, yahitaji mwanamke awe na busara na unyenyekevu kujua namna ya kumbadili mwanaume akili na tabia.

Ushauri kwa wanaume:
Heshima ya ndoa haitafutwi kwa mabavu. Kama ulishaoa kirukanjia kilichokosa maadili ya dini basi tambua kuwa ni neema ya Mungu tu inahitajika. Na maisha yako yasiwe ya kushindana naye. Mungu aliposema mke wako akutii na umtawale basi ni kutokana na yale aliyoyaonesha mwanamke bustanini. Ni dhahiri Mungu alijua kuwa mwanamke akikuongoza basi ytajirudia yale ya kupewa tunda bustanini. Lakini hii haimaanishi kuwa hana akili na hawezi kukushauri. Ikiwa ushauri wake utaonekana si mwema, muoneshe penye hitilafu na si kumwambia 'hamna kitu kama hicho, mimi ndio nimeshasema'

Ushauri kwa wanawake:
Unyenyekevu ni silaha namba moja ya mwanamke. Ukweli ni kwamba, mwanaume ana makosa mengi zaidi ya mwanamke linapokuja suala la uhusiano. Lkn si vyema kukabili mwanaume on the spot na kujaribu kuwa juu yake. Unapjaribu kufanya hivyo ndio unamuweka mbali zaidi na kuelewa kwani muda wote atakuwa anaandaa namna ya ku- exercise power badala ya kuelewa unachosema. Jaribu kuwa kimya na tafuta wakati ufaao kubadili matokeo na si kwa ubishi. Take it from me, Hakuna mwanaume mwenye uwezo wa kumbishia mwanamke mwenye busara.

Wandugu haya ni maoni na mtazamo wangu tu. Ndoa yahitaji busara. Niwaachie mfano mmoja wa uzoefu wa ndoa yangu: Mke wangu alikuwa na tabia chafu ya kupenda kutunishiana misuli na mimi na hilo lilinikera sana hata nikashindwa kumjali (binafsi nilipenda mwanamke aliye mhitaji wa ulinzi na uangalizi na adeke haswa). Nikaamua kumuweka ktk nafasi anayotaka. Fainali ilikuwa siku moja usiku tukiwa tumelala. Nyuma ya nyumba yetu kuna banda ambalo tulifuga kuku wa kienyeji kwa ajili ya kitoweo. Wife aliniamsha usingizini na kuniambia 'Noremi, hebu amka kuna kitu kitakuwa kimeingia bandani mwa kuku wanapiga kelele sana' mimi sikuamka, nilimjibu tu kwa upole 'huna haja ya kuomba ruhusa kwangu d, jisikie huru tu kwenda bandani, tumeoana na tupo sawa huna haja ya kujidhalilisha kuniomba ruhusa' Sikuamka na kuku wote waliuawa na nyoka vikabaki vifaranga. Asubuhi niliamka nikafukia wale kuku waliokufa na wakati tunakunywa chai nikajisemesha 'nyumba yetu ingekuwa na mwanaume, kuku wetu wasingeuliwa na nyoka' . Mke wangu akaacha kunywa chai akaenda chumbani, nilipomfuata nikamkuta analia. Hicho ndio nilichokuwa nataka akione, hapo nilimbembeleza na ukawa mwisho wa ushindani wetu japo ilimchukua muda kubadilika kabisa
 
Hata ujifanye una busara kiasi gani kamwe huwezi kuibadili kauli ya Mungu juu ya mwanadamu. Labda pengine hatujui nini Mungu alimaanisha aliposema 'Enyi wake watiini waume zenu'. Hakuna agizo la Mungu kwa mwanaume kumtii mke wake. Naomba nikubandikia waraka kutoka 1Petro 3:1-7

"Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu, ili kama wako wasioamini lile Neno, wapate kuvutwa na mwenendo wa wake zao pasipo neno, 2kwa kuuona utakatifu na uchaji wa Mungu katika maisha yenu.

3Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi.

4Badala yake kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa ndani, kwa uzuri usioharibika, wa roho ya upole na utulivu, ambako ni kwa thamani sana machoni pa Mungu.

5Kwa kuwa hivi ndivyo walivyokuwa wakijipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu. Wao walikuwa ni watiifu kwa waume zao,

6kama Sara alivyomtii mumewe Abrahamu, akamwita ‘bwana.' Ninyi ni watoto wa Sara kama mkitenda yaliyo mema na bila kuogopa jambo lo lote.

7Vivyo hivyo ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili, nanyi wapeni heshima mkitambua ya kuwa wao ni wenzi walio dhaifu na kama warithi pamoja nanyi wa kipawa cha thamani cha uzima, ili kusiwepo na cho chote cha kuzuia maombi yenu.
"

Huo mstari wa saba unamuelezea mwanamke kama kiumbe mdhaifu. Lakini unataka pia AHESHIMIWE. Lakini ni nini basi maana ya UTII.

Pamoja na heshima utakayopata toka kwa mumeo, bado wewe mwanamke una wajibu wa kumtii mume wako. UTII ni rejeo la kauli ya Mungu bustanini. Tazama Mwanzo 3:16 'Akamwambia mwanamke, "Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa utungu utazaa watoto; na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala"'

Utaona kuwa UTII upo katika mamlaka zaidi. Na neno UTII mara nyingi kwenye Biblia limeambatanishwa katika mazungumzo yanayohusu Mamlaka.

Kinachotusumbua leo ni HARAKATI ZA MWANAMKE KUWA SAWA NA MWANAUME. Heshima ya ndoa imepotelea hapa na wanawake waamekengeuka kiasi wanashindwa kuelewa nini wanataka. Kauli ya Mungu haikuwa peke yake. Upo ushahidi wa Kibaiolojia kuwa uwezo wa mwanamke wa kufikiri ni mdogo kulinganisha na mwanaume.

Mimi huamini kitu kimoja. Amri waliopewa wanaume ni ngumu kuliko agizo walilopewa wanawake. Hebu itafakaraki hii kauli 'nanyi waume, wapendeni wake zenu'.
1. Ukimpenda mkeo, utajitoa kwake
2. Ukimpenda mkeo, utamuheshimu
3. Ukimpenda mkeo, utamthamini
4. Ukimpenda mkeo, utamuongoza katika njia iliyo njema
5. Ukimpenda mkeo...........n.k, n.k

Lakini utatoka wapi upendo wa kumpa mwanamke anayeshindana na kutaka kuwa sawa nawe hata akasahau nafasi yake katika ndoa. Wapo wanawake wanaodhani kuwa kushindana na mwanaume ndio ushindi katika ndoa. Si haiba ya mwanamke kuwa mshindani kwa mwenzi wake wa ndoa ambaye ana jukumu la kumtunza na kumlinda. Ndoa yenye heshima ni zao la wanandoa wenye kujua wajibu na mipaka yao. Hata hivyo, yahitaji mwanamke awe na busara na unyenyekevu kujua namna ya kumbadili mwanaume akili na tabia.
Ushauri kwa wanaume: Heshima ya ndoa haitafutwi kwa mabavu. Kama ulishaoa kirukanjia kilichokosa maadili ya dini basi tambua kuwa ni neema ya Mungu tu inahitajika. Na maisha yako yasiwe ya kushindana naye. Mungu aliposema mke wako akutii na umtawale basi ni kutokana na yale aliyoyaonesha mwanamke bustanini. Ni dhahiri Mungu alijua kuwa mwanamke akikuongoza basi ytajirudia yale ya kupewa tunda bustanini. Lakini hii haimaanishi kuwa hana akili na hawezi kukushauri. Ikiwa ushauri wake utaonekana si mwema, muoneshe penye hitilafu na si kumwambia 'hamna kitu kama hicho, mimi ndio nimeshasema'

Ushauri kwa wanawake: Unyenyekevu ni silaha namba moja ya mwanamke. Ukweli ni kwamba, mwanaume ana makosa mengi zaidi ya mwanamke linapokuja suala la uhusiano. Lkn si vyema kukabili mwanaume on the spot na kujaribu kuwa juu yake. Unapjaribu kufanya hivyo ndio unamuweka mbali zaidi na kuelewa kwani muda wote atakuwa anaandaa namna ya ku- exercise power badala ya kuelewa unachosema. Jaribu kuwa kimya na tafuta wakati ufaao kubadili matokeo na si kwa ubishi. Take it from me, Hakuna mwanaume mwenye uwezo wa kumbishia mwanamke mwenye busara.

Wandugu haya ni maoni na mtazamo wangu tu. Ndoa yahitaji busara. Niwaachie mfano mmoja wa uzoefu wa ndoa yangu: Mke wangu alikuwa na tabia chafu ya kupenda kutunishiana misuli na mimi na hilo lilinikera sana hata nikashindwa kumjali (binafsi nilipenda mwanamke aliye mhitaji wa ulinzi na uangalizi na adeke haswa). Nikaamua kumuweka ktk nafasi anayotaka. Fainali ilikuwa siku moja usiku tukiwa tumelala. Nyuma ya nyumba yetu kuna banda ambalo tulifuga kuku wa kienyeji kwa ajili ya kitoweo. Wife aliniamsha usingizini na kuniambia 'Noremi, hebu amka kuna kitu kitakuwa kimeingia bandani mwa kuku wanapiga kelele sana' mimi sikuamka, nilimjibu tu kwa upole 'huna haja ya kuomba ruhusa kwangu d, jisikie huru tu kwenda bandani, tumeoana na tupo sawa huna haja ya kujidhalilisha kuniomba ruhusa' Sikuamka na kuku wote waliuawa na nyoka vikabaki vifaranga. Asubuhi niliamka nikafukia wale kuku waliokufa na wakati tunakunywa chai nikajisemesha 'nyumba yetu ingekuwa na mwanaume, kuku wetu wasingeuliwa na nyoka' . Mke wangu akaacha kunywa chai akaenda chumbani, nilipomfuata nikamkuta analia. Hicho ndio nilichokuwa nataka akione, hapo nilimbembeleza na ukawa mwisho wa ushindani wetu japo ilimchukua muda kubadilika kabisa

nimependa sana hapo kwenye red!ahsante MTOKA pabaya kumbe kuna wakati huwa unatunyima maskills haya enh!uwe unatumegea bana si unajua kila siku tunajifunza kutokana na vyanzo mbali mbali vya watu!mimi like this sana!
 
Last edited by a moderator:
mwanaume unapotaka mkeo AKUTII je wewe UNAMUHESHIMU mkeo?

Ni kweli mwanaume ni kichwa ila jiulize wewe mwanaume kichwani una ubongo au *****?
 
hahahahaha nimeikuta hii mahali nikaipenda, wanaume kazi kwenu:-

usimuonee wivu mke umpendaye;
utakuwa umemfundisha namna ya kukudhuru.
Usimwachie mwanamke ukuu wako,
la sivyo atakutawala kabisa (sira 9: 1-2)

nyingine hii (dedikesheni kwa wanaume wapenda kulelewa):-

usinaswe na uzuri wa mwanamke,
wala usimtamani mwanamke kwa mali yake
ni ghadhabu, aibu na fedheha mume kulishwa na mkewe. (SIRA 25: 21-22)

na kwa mabachela ujumbe wenu ni huu:-

mwanamume akipata mke amepata ubora mkubwa mno,
amejipatia msaidizi bora na nguzo ya msaada.
Mali isiyolindwa kwa ukuta itaporwa;
ni pasipo mke, mwanamume atatangatanga na kusononeka.
Nani atakayemwamini jambazi azururae mji hata mji?
Hivyo hakuna atakayemwamini mwanamume asiye na kwake, ambaye ana malazi popote usiku unapomkuta (SIRA 36:29-31)

ASANTE MTOA MADA KUMBE BIBLIA IMEANDIKA HII, NISINGEIONA KAMA NISINGEKUTA POSTI YAKO

'......na ubaya wa mwanamke hutoka kwa mwanamke' sira 42:13

by the way samahani kwa kukuchakachulia loh.....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom