Enyi Wafungwa/ mahabusu watarajiwa jiwekeeni hazina

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Wanasiasa wetu ndani na nje ya chama NI mahabusu watarajiwa.

Viongozi wa umma wakiwemo makatibu wakuu pia ni mahabusu/Wafungwa watarajiwa.

Ninaposema mahabusu na Wafungwa simaanishi lazima wawe mafisadi Bali zipo njia nyingi zinakufanya uwe mahabusu au mfungwa.

Pius Luhende na Ditopile hawakuwahi kuwaza kwenda mahabusu ila wameingia.

Mwanyika, malinzi, mbowe, Lema, no yamkini hawakupaswa kwenda mahabusu lakini wapo huko.

Mzee wa NIDA na wengine kwenye utumishi wa uma waliosave wakati wa jk hawakuwaza kuishia mahabusu lakini walienda.

Lau Masha hakuwahi kwenda mahabusu lakini alienda

Wazee wa majengo pacha hawakuwaza kuwa one day watapelekwa rumande lakini walienda.

Mifano hii na kwakuzingatia wanaotutuma tuvunje Sheria wamewekewa Kinga Basi ni Jambo la kawaida kabisa watawala waliopo Sasa ikafika zamu yao kwenda kuishi jela au mahabusu.

Kwa kuwa mahabusu hapaepukiki Basi tupatengeneze Sasa ili siku tukienda tupakute panafaa kuishi watu na si wanyama.

Nilimsikiliza Palamagamba alivyoshupaza shingo kuhusu haki ya kujamiiana nikajiuliza huyu amesau mkataba wa kuuza korosho alioshuhudia wiki kadhaa na kuusifia umebainika wamesaini na watu wasionamtaji? Kesho akipelekwa mahabusu akashindwa kuwasiliana faragha na mkewe atamlaumu Nani?

Mahabusu/magereza yetu tunayokila sababu ya kuyaboresha na kuyafanya ya kisasa Sasa tukiwa tunaweza kutoa maamuzi ili ikitokea kesho tukawa huko tupakute panafaa na hata tusipokwenda huko Basi ndugu zetu waishi Kama binadamu na si Kama wanyama.

Siyo kila aliyepo gerezani ni mualifu, wengine wamepelekwa kwa sababu tu yupp mtu mwenye mamlaka ya kuagiza uwekwe ndani na ambaye Leo ni rafiki yako Ila kesho ni adui yako.Leo yupo chini yako Ila kesho atakuwa Juu yako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Awamu ijayo makaburi yatakapofukuliwa wengi watafungwa wallahi sababu kuu ni matumizi ya Madaraka, kutumia vyeti feki,matumizi mabaya ya kodi zetu, upotevu wa watu,uuzaji wa nyumba na Mali za serikali.nk,kila MTU ni mfungwa mtarajiwa kama sio ndani nje the Hague, Ishu ya kinga ni busara za ajae katiba si msahafu isibadilishwe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom