singidadodoma
JF-Expert Member
- Nov 11, 2013
- 4,394
- 1,536
Kwa muda mrefu Cuf imejitambulisha kwa watanzania kama chama cha wananchi na kinachopigania haki sawa kwa wote, ikiwa na itikadi ya utajirisho ikilenga kumkomboa mwananchi wa kawaida kutoka katika lindi la umasikini kwa kutumia rasilimali za nchi.
Lakini sasa baada ya kuachana na misingi yake ya awali haielweki inachokipigania wala haitabiriki, baada ya kupita uchaguzi wa marudio huko Zanzibar hakuna ajuaye Cuf inafanya shughuli gani chanya ya kisiasa itakayonufaisha mwananchi.
Hapa ilipojifikisha Cuf haieleweki inapigania haki sawa kwa wote ama baada ya kupindisha malengo yake ya awali sasa inapigania maslahi binafsi ya kiongozi wake mkuu Seif Sharif Hamadi
Cuf ya sasa imekosa washauri makini baada ya Seif Sharif Hamad, kuwafukuza viongozi wenzake ndani ya Cuf ama kusababisha wajiondoe watu waliokuwa na uwezo wa kumwambia Seif HAPANA.
Ni hasara kwa kiongozi mkuu kuzunguukwa na watu wasioweza kukwambia hili na hili HAPANA, AU KUMWAMBIA HAPA UNAKOSEA MKUU, hakuna mwenye uthubutu huo jambo ambalo limeisababisha Cuf kutoka nje ya mfumo wa uongozi wa Zanzibar lakini viongozi hao wanataka kuendelea kuwepo ndani ya mfumo wa kuendesha siasa za Zanzibar.
Wengi walishauri Cuf isijitoe wala kususia uchaguzi wa marudio kwa kuwa kufanya hivyo kuna madhara makubwa kuliko faida moja ya hasara ni hili la kuendesha siasa nje ya utaratibu ‘’to operate in illegality’’ na kuendesha siasa nje ya utaratibu siku zote huwa hauwezi kumnufaisha mwananchi anayetawaliwa baada ya uchaguzi kupita kwa kuwa hatakuwa na namna yeyote kuiepuka serikali itakayoundwa na huyo mshindi wa uchaguzi uliosusiwa.
Hivi Cuf wanaposema kuwa Dr. Shein kachaguliwa na wachache baada ya wao kususia uchaguzi wanadahani atashindwa kuwatawala wengi waliohamasishwa kususia uchaguzi?
Jibu la swali hilo ni kwamba lipo peupe wamkubali au wamkatae bado Dr. Shein ndiye mtawala wao hawana namna kumuweka mtawala mwingine wanayemtaka wao.
Shein ameshakula kiapo hivyo basi wapende wasipende wataishi chini ya huyo huyo waliomsusa na kutokana na kususa kwao wamemsababishia kushinda kiurahisi kutokana na kususia kwao, Na katika suala la ulinzi na usalama pamoja na kususa kwao bado wanahisaji kulindwa na serikali hiyo hiyo walioisusa ya Dr. Shein, kwani hawawezi kujilinda wenyewe na wala kuepukana na ulinzi wa serikali inayotambuliwa kikatiba na kisheria.
Seif Sharifu Hamadi anatambua kuwa pamoja na kuhamasisha wananchi kususa lakini hana uwezo wa kuwalinda wananchi hao kwa lolote lile na hawezi kuunda serikali yake yenye uwezo wa kuwalinda raia na mali zao pamoja na kusimamia shughuli zao za kila siku.
Kwa kifupi Serikali ya Dr. Shein haiepukiki wala haizuiliki kutekeleza mipango yake ya kila siku ya kuwahudumia wananchi wote waliomchagua pamoja na waliohamasishwa kusuasa.
Viongozi wa Cuf wanajua gharama za watu kuishi chini yaserikali iliyoundwa na kiongozi wanayemkataa na kukiri wazi kutomtambua, kwani walishajionea uzoefu chini ya serikali ya Dr. Salmin Armour mara baada ya uchaguzi wa mwaka 1995.
Swali la msingi je Cuf wanapoamua kuendesha siasa za mwelekekeo hasi wa chuki, kununa, kususa, kukataa,kuhamasisha wazanzibar kutoshirikiana na serikali wanakusudia kumuadhibu nani? Sharif Hamad na wenzake kuhamasisha wananchi wanaoikubali Cuf wawe kinyume na serikali isiyoepukika hawaoni kuwa wanawatwisha wananchi hao mzigo mzito wasioweza kuubeba? Na kwanini mzigo huo wasiobebe wenyewe?
Hadi sasa viongozi wa Cuf bado wanaendelea kuwadanganya wananchi wanaowasikiliza haswa pale Sharif Hamadi aliposema hamtambui Shein kama Rais, watu makini wanamuona kama anafanya maigizo au mwanasiasa mfa maji amabaye haachi kutapatapa kwa tabia yake ya kuendesha siasa zisizo na uhalisia.
Haiwezekani hata kidogo kwa raia anayetawaliwa na Rais wa nchi yake akadai hamtambui Rais wakati tayari Rais huyo ni mkuu wa nchi anayesimamia shughuli zote za serikali inayotawala raia wote wanaoishi ndani ya nchi hiyo.
Seif anaposema Dk. Shein hatomaliza miaka 5 pamoja na kuwa kauli hiyo keshawahi kusema kwa Dr. Salmin Amour na akamaliza kipindi chake hadi uchaguzi mwingine wa mwaka 2000 uliomuingiza Karume mtoto ikulu ya Zanzibar. Pamoja na kauli hiyo lakini Seif hasemi atafanya nini kitakachomuondosha Dr. Shein ikulu ilia toke mapema kabla ya kipindi chake kwisha.
Hivi ikitokea mwanafunzi wa chekechea akamuuliza kiongozi wa Cuf kuwa Rais wa Zanzibar nani watamjibu kuwa Zanzibar haina Rais wala serikali?
Hili linadhihirisha kuwa Cuf inakoelekea siko baada ya kukuosa watu makini ndani ya chama wenye nguvu ya kumkosoa Seif kwa kumwambia ukweli peupe.
Tumesikia tamko la baraza kuu la Cuf linapofurahishwa na vikwazo vya Marekani vya PAMOJA NA KUITAKA JUMUIYA YA KIMATAIFA KUIADHIBU Zanzibar na Tanzania bar kwa ujumla hivi wanajua wanaloomba katika jumuiya hizo za kimataifa?
Cuf wanashindwa kutambua kuwa katika dunia ya sasa ya watu waliostaarabika wanapiga vita adhabu ya vikwazo, iwe vya uchumi au usafiri wa anga ama vikwazo vya biashara, kwa sababu imedhihirika pasipo shaka kwamba adhabu hizo hazilengi kumwadhibu mkosaji mojakwamoja zaidi ya wananchi tena wenye hali ya chini kabisa.
Hivi ikitokea jumuiya ya kimataifa ikaiwekea vikwazo vya uchumi Zanzibar, kitakachofuata ni kwamba hali za wananchi zitakuwa ngumu aliyekuwa anakula mlo mmoja huenda asipate kabisa, cha ajabu ni kuwa hali hiyo hatamuumiza Jecha wala Shein wasiomtaka wao isipokuwa wale wale wananchi waliowahimiza kususa ndio watakaokumbana na hali ngumu na ukali wa maisha kutokana na vikwazo hivyo.
Wananchi wa kawaida amabao Cuf inajitia kuwapigania ndio hao watakaopata msoto mkali wa maisha, hapa ndipo kunapokuja swali je Cuf inaamini kwenye itikadi yake ya wali ya haki sawa kwa wote na utajirisho? Au imekengeuka inapigania maslahi ya binafsi ya Seif Sharif Hamaf kama mwana siasa mwenye kiu ya madaraka anayeendesha siasa zisizo na uhalisia.