Enyi CCM mtoto akiomba mkate hupewa jiwe? Makala na Uchambuzi (MTANZANIA) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Enyi CCM mtoto akiomba mkate hupewa jiwe? Makala na Uchambuzi (MTANZANIA)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 1, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  WIMBO wa sasa kila kona nasikijia ni kujivua gamba tu, uliyoasisiwa na Chama Cha Mapindizi (CCM) wiki kadhaa zilizopita.

  CCM yenyewe inasema imejivua gamba eti kwa sababu inataka kujtakasa mbele ya wanachama wake na taifa zima kutokana na kushamiri kwa vitendo vya ufisadi.
  Inadai vitendo hivyo, vilisababisha chama kuchukiwa mno na wananchi hasa walalahoi wa ngazi za nchini.

  Wote tunakumbuka kwamba, CCM iliasisiwa kama chama cha wakulima na wafanyakazi na ndiyo maana hata nembo iliyoko kwenye bendera yake, inaonyesha nyundo na jembe.

  Kwa misingi hiyo, CCM iliweza kuwa karibu sana na wananchi tangu tangu kuzaliwa kwake na hata baada ya kuzaliwa.

  Lakini kadri miaka ilivyosonga mbele, CCM imekuwa ikibadilika kama rangi ya kinyonga, kutokana na matendo yake.

  Matendo yamekuwa ni mengi na ya kuudhi mno, rushwa, watu kujilimbikizia mali na kuacha wengine wakishindia mlo mmoja kwa siku.

  CCM imekuwa mbalimbali kushughulikia kero lukuki zinazoelekezwa kwake na wananchi hasa katika miaka ya karibuni.

  Wiki kadhaa zilizopita tumeshuhudia mabadiliko yaliyosababisha vigogo kadhaa kutupwa nje, huku safu mpya zikiingia na nguvu mpya.

  Lakini katika safu hizo, viongozi wanaokana kubebeshwa msalaba wa chama hicho ni Katibu Mkuu, Wilson Mukama na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa, Nape Mnauye.
  Katika salamu zake za kutambulisha Sekretarieti mpya, Nape amekuwa akisisitiza kuwa watu waliotuhumiwa kwa ufisadi lazima waondoke ndani ya siku 90.
  Amekuwa akitumia maneno hayo kila anakokwenda kutambulisha timu yake ambayo anaiita ya mapambano.

  Lakini tangu Nape waanze kazi hii, wanaonekana wazi kuwalenga watatu katika kijuvua gamba.

  Watu hao ni wabunge Edward Lowassa (Monduli), Andre Chenge (Bariadi Magharibi) na Rostam Aziz (Igunga). Hawa wanaonekana kuwa ndiyo wenye matatizo zaidi.
  Nasema tabia ya kuwahukumu kabla ya kuwapatia nafasi ya wao kujileza ki kitu mbayo ambacho kamwe hakikubariki.

  Ndani ya CCM kuna watu wengi mno ambao leo hii kama tukisema wajivue gamba ni wazi kwamba watapukutika kama upupu.

  Ufisadi wa CCM hakuuanzia juu tu, hebu jiulizeni namna ambavyo ngazi za chini kulichafua wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

  Huko ndiko tumeona namna ambavyo wanyonge walivyonyimwa haki zao za msingi, wenye pesa ndiyo waliopenya kupata nafasi mbalimbali za uongozi.

  Leo hii Nape anapotoa siku 90, hizi ni vichekesho kwa sababu naamini asilimia 100 siku hizo zikifika hakuna mtu atakayepewa barua ya kuondoka.

  Tukubari tusikubari, kama ikiwe hivyo basi hata mkuu wa kaya naye itabidi ajivue gamba kwa sababu amekuwa kionyeshewa kidole kuhusiana na masuala ya ufisadi.
  Nape anapaswa kuelewa wazi haya anayoyasema yanaanzia kwenye ofisi yake hadi kwa bosi wa chama.Hapa tusishangae CCM siku zijazo inageuka kuwa chama cha upinzani.

  Kundoka kwa watu wanaodaiwa mafisadi ina maana ni mwanzo wa kutaka hata serikali iliyopo iondoke, kwa vile hakuna msafi kiasi kinachotakiwa.

  Kwa mfano, wiki mbili zilizopita Tume ya Maadili ya Viongozi, imeendesha vikao vyake hapa Dar es Salaam, kwa kuwaita viongozi kadhaa kwenda kujieleza baada ya kushindwa kujaza fomu za mali wanazomiliki.

  Hebu fikilia kwa nini wamekwepa, hawa wamekwisha vuna vya kutosha, sasa wanakosa majibu ya msingi ya kukwepa fomu ambayo kisheria wanapaswa kuijaza.

  Mbali na mafisadi hao, hebu tujiulize kuna viongozi wangapi wanaotokea CCM, wamehakikiwa mali zao? Kama si kutaka kudanganya tu.

  Nape na Mukama nawaonea huruma sana kutokana na vita walioanzisha, kwani siku zijazo inaweza ikawageukia kama moto wa kifuu.

  Nasema hivyo, kwa sababu viongozi ambao wanaonekana kuja na moto mkali, lazima watashikwa na kigugumizi cha nani awe wa kwanza kuandika barua kwenda kwa watuhumiwa.

  Ni ukweli usiopingika kwamba CCM ya leo si ile ya miaka 15 iliyopita, haikubariki kwa vijana hata wazee ambao waliiasisi wenyewe.

  Nasikitika kuona hata leo ukiitishwa uchaguzi hapa,CCM watalazimika kutumia akili nyingine. Kama wakitaka "fair pray" hawatoki.

  Namwambia Nape na Mukama kuwa enzi za kuwahadaa Watanzania kwa kofia fulani wakati wanaendelea kupigika kwa maisha magumu, zimepitwa na wakati.

  CCM imefika wakati wa kukaa chini na kutafakari kwa kina, wapi imejikwaa na wapi itaangukia.

  Kama kuna kero za wananchi, zikiwemo za kunyang'anywa viwanja,mfuko wa bei na gharama zingine za maisha zinapanda, lakini hazishughulikiwi kwa nini wasiichukie kwa gharama yoyote?

  Hapo ndipo CCM, wanapaswa kufikilia hayo, kama kero hizi zinapatiwa ufumbuzi mwananchi gani ataipinga?

  Lakini hayo yanapopewa kisigo matokeo yake yameonekana mwaka jana, watabaki wanaandama watu fulani kwamba ni mafisadi, huu ni ujinga.

  Kwa Wakristo ukisoma kitabu za Mathaya 7:7-11 panasema Je, kuna yeyote miongoni mwenu ambaye mtoto wake akimwomba mkate atampa jiwe? Au, akimwomba samaki atampa nyoka? Kama, basi nyinyi, ingawaje ni waovu, mwajua kuwapa watoto wenu vitu vizuri, hakika Baba yenu wa mbinguni atafanya zaidi: atawapa mema yote wale wanaomwomba.

  Nape na Mukama nina uhakika mkitafakari maneno haya mtapa majibu. Napenda kuwaambia watoto wenu ni wananchi ambao wanataka mkate ninyi mnawapa mawe ndiyo maana wanawakimbia.kwa nini keki ya taifa iliwe na na kundi la watu wachache?

  Kama watoto hawa wanapoomba mkate mnawapa, basi hata siku moja tungeshuhia misamiati ya kujivua magamba, lakini mmekuwa mabingwa wa kuwapa mawe ambayo si chakula na kuwaacha wakinung'unika kila kukicha.

  CCM wanapaswa kutambua maneno haya " kila mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala

  Ndiyo maana nasema kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. Hizi ni zama za CCM kuokoa jahazi kabla ya halijazama.

  Siku za CCM kuendelea kutamba kwamba wao ni nambari wani zimekwisha, kama maandiko matakatifu yanavyosema "Si kila aniambiaye, `Bwana, Bwana,` ataingia katika Ufalme wa mbinguni; ila ni yule tu anayetimiza mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.

  Kwa vile CCM inashindwa kutimiza mapenzi kwa Watanzania, sasa ni wazi wataendelea kukalia kuti kavu. Tunasema hivyo kwa sababu walitakiwa kufanya uchaguzi mwaka 2012, lakini kutokana na hali kuwa tata wamelazimika

  Namalizia kwa kusema enyi CCM mtoto akiomba mkate mtapa jiwe? Moto wa Nape na Mukama naona bado wana kazi ngumu mbele yao,kwa jinsi hali ilivyo hatuamini kama watu wataondoka ndani ya siku 90, hii ni ‘porojo tu'

  0712 207 553,karedia2005@yahoo.co.uk
   
 2. H

  Haki sawa JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2011
  Joined: Oct 3, 2007
  Messages: 4,701
  Likes Received: 559
  Trophy Points: 280
  Lengo sio kuwavua watu magamba ila ni mfumo kristo uliotawala kuwa Sisi waislamu hatuwezi kuongoza ndio maana yafuatayo yanafanyika;
  1. kuwa JK chama kitamfia kwani hana uwezo wa kuongoza.
  2. Makamba , kwa sababu alikuwa muislamu aliondolewa na kuwekwa mkristo tena mkatoliki ili CCM iwaridhishe wakatoliki na kuweza kuchukua wale waioenda CHADEMA kana kwamba bila wakatoliki ccm itakufa.
  3. Tazama secretyariat mpya ni mfumo kristu mtupu majina haya hapa ,
  • wilson Mukama
  • John Chiligati
  • Nape Nnauye
  • aliyeiba jina mbunge wa kule iramba
  • January makamba -huyu ni muislam lakini ni "Tarikh swalaa"
  hata huu mkakati wa kuvua gamba ni ili kumwondoa muislamu Rostam na hawa lowassa na Chenge ni chambo tuu, lakini lengo ni kuwangoa waislamu ambao wamekuwa na nguvu kwenye mifumo ya kisiasa nchini na hata kushawishi maamuzi makubwa
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Wewe kweli ni Mzushi haujui kuwa Nape Nnauye ni MUSLAMU? Shame on you !!!
   
 4. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Wewe haki sawa unatapatapa tu, mimi nilitegemea a good analysis with the numbers instead umetaja watu watano. ACHENI UNAFIKI
   
 5. t

  tarita Senior Member

  #5
  May 1, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 156
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hufai hata kutemewa mate. Udini mpaka kaburini.Mdini kuliko dini yako. CRAP.
   
 6. maulaga

  maulaga JF-Expert Member

  #6
  May 1, 2011
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 472
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mawazo na mtazamo huu ni hatari sana. Unaikosea jamii nzima ya wapenda amani na utulivu duniani kote kwa sumu mbaya kama ya udini unaopandikiza kwetu. Naamini watu wenye nia njema watakudharau na kukupuuza mtu hatari kama wewe. Hata uislamu wenyewe huutendei haki hata kidogo.
   
Loading...