Enyi CCM masilahi nisikilizeni

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Nchi hii, Tanzania, ni yetu wote bila kujali rangi, dini, kabila, itikadi, jinsia wala nini sijui.
wote tunahaki ya kula, kufaudu na kufurahia mema yote aliyotukirimia Mwenye
Mungu katika Mipaka yetu.

Ni jukumu letu la kitaifa katika umoja wetu mkubwa sana tulio nao kuhakikisha kwamba
kila mmoja wetu anaishi maisha ya raha na starehe katika namna na viwango vinavyompendeza
Mwenyezi Mungu na sisi wenyewe katika umoja wetu.

Katika kutimiza hili, ni wajibu wetu kuhakikisha kwamba tunakuwa na serikali imara
inayoweza kusimamia mahitaji haya bila shaka wala mawaa, serikaili inayoweza kusimamia
usalama wa mali,sisi wenyewe, shibe na furaha zetu dhidi ya maadui wowote kutoka nje
na ndani ya mipaka yetu.

CCM, ambacho ndio chama kinachounda serikali tunayotegemea isimamie mahitaji haya
imeshindwa kutupatia mahitaji haya. miaka 50 baada ya uhuru ni watanzania wachache
sana ambao hawafikii hata asilimia mbili ya kizazi chetu kilichopo hai leo ndio maisha
yao yamefikia viwango hivi.

Natambua kwamba binadamu wanakawaida ya kusahau matatizo yao yooote pale
wanapopata shibe ya siku moja, ambacho ndio nachokiona kwenu wana CCM masilahi,
ambao bila shaka, kama mmoja wenu alivyesema jana na mbunge wa mtela alivyosema
uko Igunga, mko tayari kufa kuliko kuona CCM ikitoka Madarakani.

Lakini naomba mfumbue macho yenu na kuangali matatizo yanayotukabili kama taifa,
well, angalieni jinsi binamu zenu na bibi zenu huko vijijini wanavyoteseka, Mwita 25, angali
jinsi ndugu zako nyamongo wanavyoteseka na kufa kwa njaa na maradhi ama yanayotibika
ama yanayosambazwa kwa makusudi huku wakiwa wanazungukwa na madini yenye
thamani kubwa hapa duniani. chonde chonde Jamani.

Niko tayari kuungana na nyie katika kuhakikisha kwamba CHADEMA aichukui uongozi wa
serikali mwaka 2015 lakini na nyie nawaomba tuungane kuhakikisha CCM inaondoka madarakani
2015.
 
Umejielewa wewe mwenyewe. Kumbe wewe ukishapewa ulaji tu hatutakuona kwenye harakati. Mchumia tumbo!
 
Mimi naomba nchi hii iuzwe na kila mtu apate chake. Halafu kila mtu atajua mahali pa kuishi. Maana dharau imezidi sana!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom