English Grammar: Benki ya Posta Tanzania ni TPB Bank au TPBank? Ni sahihi kwa neno "bank" kutumika mara mbili?

wehoodie

JF-Expert Member
Nov 20, 2011
979
1,000
Soma hiyo picha hapo chini nilipo fanya highlight
View attachment 1171516
Hayo ni makosa ya kiuandishi tu...sidhani kama tuna haja ya kubishana kitu ambacho kiko obvious hivyo. kama unafahamu mtu yeyote katika Industry ya Advertising Agency, branding nk mcheki anaweza kukufafanulia.

Sio lazima kuwa sahihi kila wakati - pia zingatia haya ni makampuni makubwa mpaka logo au jina linapitishwa linapitia mchakato mrefu ndani na nje ya kampuni. watu wote wa huo mlolongo hawawezi kufanya kosa la kuita 'barabara ya morogoro road'....good day.
 

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
9,480
2,000
TPB kirefu chake ni "Tanzania Postal Bank" kama sikosei. Sasa TPB Bank maana yake ni Tanzania Postal Bank Bank? Ni sawa na mtu anayesema "daraja la Selander bridge" anakuwa ametamka "daraja na bridge" kwa wakati mmoja wakati maneno yote mawili yana maana sawa???
Hayo ni mambo ya kawaida tu. Kumbuka shule ya sekondari ya wasichana ya Songea Girls, au Green vest ya kijani, gazeti la serikali la Government Gazette, au mtaa wa Msimbazi Street
 

ISO M.CodD

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
4,907
2,000
Ulichokizingumzia nakifananisha na chaneli ya ESPN Marekani.

Mwanzoni, ESPN ilikuwa ni kifupi cha Entertainment and Sports Programming Network.

Lakini baadaye nikaja kusikia kwamba waliamua kuji rebrand na kujiita tu ESPN kwa sababu tayari walikuwa wameshakuwa brand name kwenye mambo ya habari za michezo na burudani.

Kwa hiyo, ESPN ya sasa hai stand for anything tena.
Asante mkuu. Asante sana.

Kiranga sisi wananchi wa kawaida hatumuwezi kwa kweli. Tusaidid mkuu.
 

ISO M.CodD

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
4,907
2,000
Benki kama hii haikawii kukutungia accounting principles mpya zitakazofanya kila shilingi yako uliyoweka kwao baada ya mwaka iwe senti hamsini.

Wanaweza kukuambia "tume i rebrand one shilling iwe fifty cents"!
Mkuu you are hitting imagination levels that were previously unprecedented....
 

ISO M.CodD

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
4,907
2,000
Tukimaliza hilo tuhamie kwenye BancABC
Banc ndio bank au? Ngoja tuendelee na TPB kwanza.
Acha roho mbaya mkuu unataka huu uzi uende mpaka 2025?

Nyie ndio mkikuta ugomvi mahali mnauchochea afu mnaagiza bia.
 

ISO M.CodD

JF-Expert Member
Feb 17, 2013
4,907
2,000
Citibank wame rebrand kutoka Citibank kwenda Citi. I was there. Mpaka email addresses wakabadilisha kutoka @citibank.com kwenda @citi.com.

Sijaona Citibank Bank!
If they rebranded from Citibank to Citi doesn't that mean they used to be Citibank bank?

By the ways theirs is not a case of redundant acronym syndrome kwahiyo just as you refused the ESPN network example, this one is non admissible as well in our context
 

Likwidi

Member
Mar 25, 2019
68
125
Sio lazima inategemea na scope unapo operate,mfano ukisema Nmb kwa Tz kuna mtu hataelewa unamaanisha bank? Yaani kuitaja Yanga hadi uweke na fc ndio mtu aelewe unamaanisha timu ya mpira?
Sasa yanga inakujaje hapa tena
 

Thebroker

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
881
1,000
Sie wabongo ni wabishi kweli kweli. Pamoja na maelezo mazuri ya baadhi ya wachangiaji bado watu wanataka kurefusha hivyo vifupisho...)
Correct; Watanzania ni wavivu wa kufanya research....kuna bank ilikua inaitwa:
Kenya Commercial Bank Limited(KCB) siku hizi haipo tena, sasa kuna KCB Limited, haina kirefu japo ipo affiliated na Kenya Commercial Bank Limited ya kenya....simply ni kwamba walibadilisha jina la usajili wao kwa msajili wa makampuni.

Na hio ndo imetokea kwa Iliyokua Tanzania Postal Bank ambayo kwa sasa haipo tena kuna TPB Bank Plc na ndo imemchanganya mleta mada!
 

Bakyaitaki

Member
Apr 6, 2012
65
125
Neno Bank linaongezwa kibiashara. Ukisema Crdb au Tpb bila kuwa kuweka neno Bank inaathiri kimatangazo.
Siyo kibiashara mkuu, ni kisheria. Banking law inazitaka taasisi zinazoitwa benki kuweka neno Bank katika majina yao. Mtoa mada hajiu kwamba jina la tasisi hiyo lilishabadilishwa kutoka Tanzania Postal Bank na sasa ni tpb Bank.

Yaahi lilibadilishwa kisheria kwa hiyo kwa sasa hakuna kitu Tanzania Postal Bank. Ni sawa na CRDB ambayo wengine humu mnaweza mkawa hata mmeshasahau ilikuwa na kirefu chake lakini kwa sasa jina ni CRDB Bank.
 

Tattoo

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
2,816
2,000
Usichojua ni kwamba bank hizo zoye zimefanya kubadili majina yao BRELA. Hawaitwi tena Tanzania Postal Bank, wala Cooperative and Rural wala National Microfinance Bank. Kama ambavyo walijifupisha PPF Pension Fund.

Walishatoa matangazo wote kwa nyakayi tofauti, TPB walitaka watambulike TPB Bank. Yaani hizo herufi ndio jina lao. Hicho kirefu chao cha zamani hawakitaki tena.

Afu google na wikipedia usizitegemee sana. Kasome historia ya Tanzania wikipedia uone ujinga uliopo.
 

Emery Paper

JF-Expert Member
Jun 1, 2019
1,414
2,000
Nadhani ukitumia kifupi cha hayo maneno yanakuwa hayatoi taarifa inayojitosheleza, ndio maana huwa inabidi kuongeza neno Bank mwishoni ili kuwa maalumu. Mfano neno TPB lingeweza kuwa na virefu vingi kama Tanzania Private Businesses, Tanzania Postal Bank, Telecommunication Professional Board. n.k. Ila ukisema TPB Bank moja kwa moja unaelewa kinachozungumziwa hapa.
 

Bakyaitaki

Member
Apr 6, 2012
65
125
Nadhani ukitumia kifupi cha hayo maneno yanakuwa hayatoi taarifa inayojitosheleza, ndio maana huwa inabidi kuongeza neno Bank mwishoni ili kuwa maalumu. Mfano neno TPB lingeweza kuwa na virefu vingi kama Tanzania Private Businesses, Tanzania Postal Bank, Telecommunication Professional Board. n.k. Ila ukisema TPB Bank moja kwa moja unaelewa kinachozungumziwa hapa.
Neno Bank ni lazima liwekwe kwenye jina la Bank kisheria (Banking Law) na ndiyo maana haiitwi Ltd au Inc. au chochota, kama ni Bank, dunia nzima lazima neno Bank liwekwe.
 

Mr Easy

JF-Expert Member
Jan 16, 2016
1,529
2,000
Tulienda watu wawili nmb wiki iliyopita kuomba bank statement YETU. Tulipompa tu kadi akawa anamwambia mwenzake kuwa kadi yetu ni ya zamani! kipindi cha National Microfinance Bank! (kadi ina hayo maneno).

Nikamwuliza kwani kirefu cha NMB ni nini! akajibu herufi NMB hazina kirefu chake, ni jina la bank inayoitwa NMB. Sasa mbona kwenye kadi hapo imeandikwa National Microfinance Bank! Sisi ni wateja wa bank ipi! Akasema wa NMB.

Mpaka hapa nipo njia panda kwa majibu yake.
 

Nyaru-sare

JF-Expert Member
Aug 2, 2019
2,276
2,000
Hii ni Double Noun. it's Grammatically correct, ktk Lugha ya kiingereza ipo ivo. tatizo waswahili tunataka kiingereza kiwe kama kiswahili.

Pilipili ili ijulikane kwa kiswahili ni lazima utamke hivo, siyo ''pili'' lkn kiingereza huwezi sema ''second second'' au pepper pepper. hii TPB Bank unaitohoa kwa mantiki ya kiswahili zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom