England vs Darnmark: Kawaida ya Euro 2020, timu bora lazima iage mashindano leo!

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Feb 17, 2015
13,663
18,037
Kuna mapinduzi makubwa kwenye soka la kileo kama ilivyodhihirika kwenye mashindano ya Euro 2020 mwaka huu. Timu bora si lazima ishinde na mara nyingi timu bora imekuwa ikizidiwa mbinu na kutupwa nje ya mashindano.

Jana timu bora sana ya Spain ilizidiwa mbinu na Italia na kutupwa nje!! Hali kadhalika timu bora za Ufaransa, Ujerumani, Ureno, Uholanzi zote zimetupwa nje! Inavyoelekea benchi la ufundi ndilo huamua matokeo zaidi kwa kuja "antidote plan" ya kuua makali yote ya timu pinzani na kutumia udhaifu uliopo kipata matokeo.

Enzi za kutegemea super stars zinaelekea ukingoni! Kwa hiyo lek tutegemee Uingereza kuaga mashindano!
 
Si tayari kamoja huko au bado!!?

Watoto ya bibi laazma watoke🤑🤑🤑🤑
 
Si tayari kamoja huko au bado!!?

Watoto ya bibi laazma watoke🤑🤑🤑🤑
Mpaka mapumziko ni sare lakini mwelekeo unaonesha watoto wa malkia watasepeshwa, siyo kwa kuwa siyo timu nzuri lakini kwa mbinu za kocha wa Danmark. Naona counter attack za Danmark zitakuwa na matokeo mazuri!
 
Back
Top Bottom