Engine overhaul

Nenda pale ilala uliziya msaada gereji utakutana na fundi ISSA atakufanyia na kukupa ushauri mujarabu kabisa ni karibu na Bungoni
 
ndugu yangu gharama za overhaul kit (full) hazijaachana mbali na bei ya engine ya 1JZ used ...

ushauri nenda kanunue engine nyingine used funga kwenye gari maisha yaendelee
kweli, bei ni mule mule, nimeamua kununua engine used
 
Kuelezwa kote huko bado unataka uendelee na utafiti ? inaelekea wee ni mbishi kama Muhidin Ndolanga na mie nasisitiza nenda na fundi wako pale Ilala mchague Engine safi muifanyie test then ukaifunge ianze kula mzigo na hiyo uliyoitoa unaweza kuikarabati taratibu au ukaifanya spare kijana, tatizo lako watu tulishapitia na wengi wanaokupa ushauri hapa tayari wana experience e.g Chilubi #8 hapo juu kakuelezea kitaalamu sana fata ushauri wake bro hutaumia
Hamna nimekaa na kuzunguka huku na kule na nimeona kweli, ni bora engine used bei ni mule mule, tofauti kidogo na uhakika wa overhaul mdogo,
 
Habari wakuu, nahitaji kufanya engine overhaul kama nilivyoshauriwa na mmoja wa mafundi,hii inatokana na kuwa gari niliyonunua ilikaa muda mrefu na iligundulika wakati wa service kuwa oil pump haifanyi kazi, water pump nayo haiko sawa, pia baadhi ya pipes zinazoonekana zinahitaji kubadilishwa, aina ya engine ni 1JZX.

Pia fundi aliniambia anahisi kuna moja ya piston huenda ikawa na tatizo. Naombeni ushauri pia kama kuna mtu anamfahamu fundi mzuri wa overhaul hapa Dar anitupia namba. Lkn pia ushauri kutoka kwa wataalam

Kama siyo bahili sana nashauri ununue injini mpya. Siyo mtaalamu wa magari lakini common sense tu imenionyesha hivyo kutokana na ulinyowasilisha issue yako. Hicho unachotaka kufanya kuna uwezekano mkubwa kikaja kukugharimu zaidi ya injini mpya, pamoja na usumbufu juu! Pia kuna uwezekano mkubwa ukaja ukakosana na hao mafundi wako. You would better order a new engine right from Japan. Nahisi gari yako ni LandCruiser LX or similar, 4000cc possibly
 
Kama siyo bahili sana nashauri ununue injini mpya. Siyo mtaalamu wa magari lakini common sense tu imenionyesha hivyo kutokana na ulinyowasilisha issue yako. Hicho unachotaka kufanya kuna uwezekano mkubwa kikaja kukugharimu zaidi ya injini mpya, pamoja na usumbufu juu! Pia kuna uwezekano mkubwa ukaja ukakosana na hao mafundi wako. You would better order a new engine right from Japan. Nahisi gari yako ni LandCruiser LX or similar, 4000cc possibly
Land Cruiser haitumii JZX engines mkuu, JZX ni cc2500-3000 utaipata aidha kwenye Mark 2 ama Chaser GX90/100/110 ama currently kwenye Altezza, Brevis, Progress, Aristo ama Supra.

Kwenye Land Cruiser LX anaishi mnyama aitwaye 1Hz ama 1HD-T na sasa 1VD-FTV ambaye ni v8!
 
Land Cruiser haitumii JZX engines mkuu, JZX ni cc2500-3000 utaipata aidha kwenye Mark 2 ama Chaser GX90/100/110 ama currently kwenye Altezza, Brevis, Progress, Aristo ama Supra.

Kwenye Land Cruiser LX anaishi mnyama aitwaye 1Hz ama 1HD-T na sasa 1VD-FTV ambaye ni v8!
Uko sahihi. ila nadhani kitu kama Landcruiser LX zina injini inaitwa ZX!
 
Uko sahihi. ila nadhani kitu kama Landcruiser LX zina injini inaitwa ZX!

ZX sio engine ni trimming code tu za Land cruiser. Kuna EX,GX,GXL,LX,SX,TX,TXL,LX,VX,VX-R,ZX ambapo EX na SX ni trim za LC Prado series 1. Series 2 zikaongezeka TX,GX na VX kwenye trimming ya prado.

LX ni trim ya Land Cruiser 70 series ambazo wengi tunaziita cruiser LX ila kuna trim yake nyengine ambayo ni ZX,TXL GXL ambapo TXL nyingi zinauziwa Australia other than Japan.

VX,VX-R ni trim za high end land cruiser kuanzia 80 series mpaka 200 series zipo pia GX na GXL landcruiser ambazo ndio ngumu ama gari za kazi!


Ila kifupi trimming code inayoanziwa na G ama T maanake ni gari ngumu ya kazi. Hutaikuta ina accessories ama Luxury kama Trim zinazoanziwa na L ama V. Halikadhalika inayoanziwa na Z ama S basi ujue ni semi luxury. Iko kati ya hizo mbili!
 
Asanteni wakuu, Naona hapa katika kusoma ushauri wenu, kununua engine nyingine ni bora kuliko overhauling, sababu ya mafundi wetu, ingawa overhauling inasaidia kupata new components ndani ya engine ila pia chochote kikikosewa katika process nzima ya overhaul basi unaweza kujikuta kweli umepoteza.

Naona niendelee kuliweka kwenye utafiti na mawazo niamue je ni overhaul ama ni replace...
usijaribu kufanya overhaul bongo kwa injini za vigari vidogo labda malori/mabasi. Naungana na waliokushauri kuwa nunua used usithubutu kabsaaa kuoverhaul utapoteza pesa zako. Issue ni kuwa kwanza spare nyingi za overhauling lazima utapata ambayo kuna fake, kingine mafundi wenye weledi na vifaa vya kutosha kwa kazi hiyo bongo hamna. Kuoverhaul engine kunahitaji fundi kuwa na vifaa vingi sana na vya kisasa kwa ajili ya kazi hiyo, na fundi atalazimika kufanya vipimo kadha wa kadha na calibration kibao, plus setting za kufa mtu.Kumbuka overhauling ya engine siyo kufunga funga tu machuma ya engine ili gari liwake big no! kuna performanca ambayo lazima gari liwe nayo at certain conditions sasa bongo fundi gani ana hayo mavifaa yoooote kwa ajili ya kazi hii??? hata wachina wenyewe hawana.
 
Siamini sana overhauling ya mafundi wa kibongo,walinifanyia ya gearbox nikaingia gharama kibao na bado ikaendelea kunisumbua mwishoe nikaishia kununua used gearbox ndio ikawa ponya yangu,kwahiyo hata mimi ningekushauri kama alivyoshauri mtu hapo juu,ujichange kununua engine kama hiyo used...
Ushauri kwa wengine, Gearbox usijaribu kurepair, nunu nyengine tu ustarehe.
 
Back
Top Bottom