Engine Oil Seal kupasuka

Sizinga

Platinum Member
Oct 30, 2007
9,101
6,027
Nina gari ya Toyota Corolla 111 INA tabia ya kupasua hizo oil seal,hii ni Mara ya 3 inapasuka na kuvuja oil yote sema uzuri naistukia maana taa ya check engine inawaka nyekundu nikipaki nakufungua boneti ni balaa. Pia imeanza kutoa moshi mweupe mwingi kidogo.

Sasa hivi kuipa route za mbali naogopa nisije kulala porini na naogopa kuikaanga,kuna funding mmoja kaniambia kuna rings za kubadilisha sijui,hapa nafikiria kununua engine nyingine tu used za Dubai ingawa sijui being yake.

Ushauri wenu wataalam wa magari please.
 
Kununua engine nyingine sio solution,

Kama hautagundua tabia inayofanya hizoseal kupasuka ni kazi bure maana nayo itarejea kule kule.

Mimi nashauri anza kutafuta ufumbuzi kwanza wa hii engine kabla haujanunua nyingine.

Pili kama unatumia oil ya kupima au za bei chee nalo huwa tatizo maana oil nyepesi huua bearing pamoja na oil seal.

Mwenye kujazia nyama pia karibu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom