Eng. Rwenge, Deo Sanga, Asharose Migiro,Nnauye Nape na Kinana wafunzwa adabu

Rose Mayemba

JF-Expert Member
May 7, 2012
721
1,017
Leo katika jimbo la Spika wa Bunge la Tanzania Anna Makinda imetokea sintofahamu kubwa sana hasa katika kipindi hiki ambacho tume ya taifa imetanzaza chaguzi za nafasi zilizoachwa wazi taifa zima ambao utafanyika 9- feb mwakani.


Eng Rwenge, Jar People, Asha- Rose Migiro, Nape Mnauye pamoja na mzee wa Tembo walilundikana jimboni hapa ikiwa ni maandalizi ya kupima upepo juu nani ni nani katika uchaguzi ujao wa kiti cha udiwani katika kata ya njombe mjini.


Mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya kanisa katoliki( pale ilipotua helkopta wakati wa ujio wa mh mbowe na tundu lisu) ulianza saa tisa na kuisha saa 11 kasoro hivi umekuwa wa kihistoria mkoani njombe ukizingatia ndiko anakotoka mh spika na ni katikati ya mji wa njombe.

Pamoja na juhudi za kusomba watu maeneo mbalimbali vijijini lakini hali ilikuwa tete tangu wanaanza mpaka wanamaliza.


NAPE MNAUYE AKURUPUA MATUSI KWA CHADEMA

Sijui kama ni kuchanganyikiwa ama vipi lakini katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi ameshindwa kuzungumza hoja kwa wananchi zaidi ya matusi na kejeli kwa Chadema, hii imepelekea hata wachache waliokuwepo kuanza kuondoka kwenye eneo la tukio kwa madai hakuna cha maana wanachokipata.

WATENDAJI NAO WANENA.

katika pitapita zangu hapa na pale nikakutana na watendaji wanaofahamu kuwa mimi ni Chadema, hawakusita kuniambia mipango iliyo ndani ya chama cha mapinduzi baada ya kunihakikishia kuwa waliitwa kwenye kikao na viongozi wa ccm wakisisitiziwa kukiunga mkono chama chao ili kuzilinda ajira zao jambo ambalo lilipingwa vikali na baadhi ya watendaji hao hivyo kuhatarisha vibarua vyao.

MAONI YA WANANCHI

sehemu kubwa ya wananchi inawashangaa viongozi wa CCM kwa kuendeleza propaganda bila ya kutatua matatizo yanayowakabili mda mrefu hususani upatikanaji wa maji. hii imewapelekea kuwa bize na shughuli zao bila kujali nani alikuwepo kwenye ardhi yao kwa muda huo, katika maongezi yao wameahidi kuwaumbua ccm kwenye uchaguzi mdogo wa udiwani

.Baadhi ya picha za mkutano huo




MZEE KINANA AKISEMA YA MOYONI

SAFU YA UONGOZI YA CHAMA CHA MAPINDUZI NA WAANDISHI WA HABARI




WACHEZA SHOO KATIKATI WAKIMCHEZEA KINANA

SEHEMU YA WANANCHI WAKIMSIKILIZA KINANA

WENGINE WAKIONDOKA BAADA YA NAPE KUANZA MATUSI

SOURCE
THE MAYEMBA BLOG
 
jar ndio jah, eng rwenge ndio lwenge, na mnauye ndio nnauye...alafu mwandishi ni mwanafunzi wa chuo kikuu...

naona umeanza kucheza na spelling huku ukiukubali ukweli.....hahahaaaaaaaa....kutaja jina la mtu yataka moyo hasa linapofanana na miti shamba
 
maccm ni mafisadi
Hiki chama tunatakiwa tukiue kabisa
Haiwezekani mafisadi ndo wanafaidi rasilimali za nchi hii watu hawana hata maji
Nakasirishwa mno na hiki chama RIP ccm
 
CCM wana Laana mbaya.Kila siku wanatuma Watu kutukana Wakristu halafu wanafanyia Mkutano katika Viwanja vya Kanisa Katoliki?.Lazima Mungu awaumbue.
 
maccm ni mafisadi
Hiki chama tunatakiwa tukiue kabisa
Haiwezekani mafisadi ndo wanafaidi rasilimali za nchi hii watu hawana hata maji
Nakasirishwa mno na hiki chama RIP ccm

Kufa kisife kibaki ili kiwe chachu ya watu kuwa na akili za kutambua mema na maovu ya upande wa pili. Though kimejaa maovu mengi....
 
Back
Top Bottom