Eng.Nsiande na Majibu ya Tatizo la Nishati ya Umeme - Must Read

NAFURAHIA SANA MICHANGO YA KILA MMOJA WENU KWENYE HII THREAD JAMANI!

Sikujua kama tuna wataalam wote hawa wanaoweza kukidhi kiu yetu ya kutaka kujua undani wa hili tatizo sugu la umeme!

Nadhani tumejifunza kwamba kama tutawatambua wataalam wetu humu JF na kuwalenga moja kwa moja kwa heshima kama ilivyofanyika kwenye thread hii basi tutafaidika sana!

Hatutafaidi kama tutarusha "makombora" bila mwelekeo, ndio mwanzo wa kukaribisha yale mazungumzo ya utani befitting jukwaa la Chit Chat.Hili halijajitokeza kwenye hii mada huenda ni kwa vile hakuna asiyeguswa na hili tatizo.

Hongereni nyote wasomaji na wachangiaji... tuendeleeni tafadhali!

Nawe hongera kwa kuleta hii mada maana wengi wetu tumejua tatizo ni nini.
 
Dush sorry... I was away for so long such that someone asked me to log in...

Apart from what is posted on the web, reality sucks..reality is...we as a country has gas shortages so even if we get 300MW now we won't be able to run the gas plants...

Mtera is @ 691m.a.s so literally it has to be shut @ 690m.a.s which will be achieved in August...unfortunately it didn't rain there!!

Grid control center is currently asking to shed further 30MW ( that explains last night outage...)

Kimsingi sina maelezo zaidi ya yaliyotolewa, ila for a state owned utility kazi ya generation bado ni mpango wa serikali.....

Pole mzalendo na watanzania wenzangu...I didn't think that I would advice this...but anyways...pls if u can go solar..it will be severe in November kama mvua za vuli ( ambazo hydrologically si. Nyingi zikiacha kunyesha Mtera )

I can advice on solar option based on ur load..yani umeme unaotumia majumbani

I was a human being before reading this sentence but I must say this is absolutely ridiculous. What if I cannot afford solar panel into my house therefore shall I say that my government failed to provide me with a reliable electricity?? Further, for 50 years since independence what have you guys been doing instead of realying on small hydro electrical power dam in Mtera. You have abandoned the plan of construction of a dam in Rufiji which would have been a much reliable source.

I think the entire Tanesco company need to be dismantled
 
Am I getting you well engn?

Kuna siku nilikuwa nimekaa mbele ya TV yangu natazama mahojiano na mainjinia fulani toka TANESCO (sidhani kama ulikuwepo), na mmoja wao akasema kwa kujiamini na kwa bold language kuwa umeme wa solar hauwezi uakatumika kwa scale kubwa kwa sababu solar zinazalisha umeme kidogo sana na unapoweka panels nyingi unaongeza resistance, hivyo haisaidii. Nilibaki nimeduwaa nikidhani ndoto zangu kuwa Tanzania na nchi nyingine huku tropical tutakuja kukombolewa kwa umeme wa jua zimakwisha.

Say it again engn... Is it possible to use solar energy for big scale power generation?

Unaweza kuzalisha big scale power generation kwa kutumia njia mbili kwa kutumia solar

Moja ni kwa kutumia panels hizo na kuzalisha umeme direct Kama unavyozalishwa majumbani. Hii si cost effective mara nyingi ukilinganisha na eneo litalohitajika na performance ya solar panels zenyewe, na haipendelewi kutumika kwenye uzalishaji mkubwa

Njia ya pili ni solar thermal power generation, ambapo nguvu za jua zinakusanywa kufanya maji kuwa steam ambayo huzungusha mashine na kuzalisha umeme. Mara nyingi hii ndio njia inayotumika kwenye uzalishaji mkubwa.
 
Twende tena kwenye historia na jiografia. Ukianza na historia na ukaenda kwenye makabati ya wizara ya nishati na giza, pamoja na TANESCO, utakuta mpango wa zamani mzuri kabisa uliotengenezwa kwa nia ya kumudu ukuaji wa umeme nchini. Kiufupi ulieleza ni wakati gani tutakuwa na umeme wa gesi, ni wakati gani tutakuwa na umeme wa mkaa wa mawe na ni wakati gani wa kuwa na umeme wa maji. Hivyo utaikuta songosongo, kiwira na mchuchuma na Steigler's gorge. Lakini tangu miaka ya 90's tumekuwa na mgao wa umeme, kisingizio ni mvua na nyingi bla bla.....

Twende kwenye jiografia. Bwawa la Mtera lipo kwenye mto Ruaha Mkuu (Great Ruaha), na kuna kituo cha Mtera cha 80MW. karibu 160km " downstream" kuna bwawa la kidatu na kituo cha kidatu cha 204MW. Hapo maji huenda kupitia mashamba ya Kilombero na kisha kuingia mto Rufiji. Kabla ya kuingia Rufiji, mto Ruaha Mkuu huungana na Mto Kilombero. Mto huu ni mkubwa hukusanya maji ya mito mingi ikiwemo Lumemo, Luipa, Mngeta, Kihansi, Mpanga na mito mingine midogo. Ni kwenye mto kihansi ambako kuna kituo cha kihansi cha 180MW, kina uwezo wa kwenda hadi 300MW, iwapo bwawa la pili litajengwa (Upper Kihansi).

Maji haya yote huingia mto Rufiji na kuingia Bahari kuu ya Hindi (Indian Ocean). Vingozi wetu wamekuwa wakituaminisha kuwa mgao ni kwa sababu ya ukame katika mito hii. Mimi nakataa kwa kuwa sijawahi kusikia mto Rufiji umekauka. Mwaka huu kulikuwa na mafuriko bonde la kilombero ilipo mito ya lumemo, Luipa, mngeta na kihansi. Maji haya yote yameingia Indian ocean, na sasa kuna mgao. Kama mipango iliyotajwa kwenye hitoria hapo juu ingetekelezwa ina maana tungekuwa na mw 2100 za steigler's gorge, 300mw kihansi, pamoja na mchuchuma 400mw (coal fired). Sharti tukubali kuwa mipango mibovu ya serikali ndio chanzo cha matatizo haya. Siitetei TANESCO lakini wao kama wakala wa serikali, hawana la kufanya iwapo serikali inakuwa na mipango ya hovyo.

Mito ya Ruhuji na Lumakali ina uwezo wa kuzalisha mw 580 kwa pamoja. Mito hiyo ilikuwa kwenye mpango huo lakini hakuna kilichofanyika na sasa kuna mgao. Mito hiyo haijawahi kuwa na ukame. Mto Kagera haujawahi kukauka, maji yake huingia ziwa Victoria. Asitudanganye mtu ukame sio chanzo cha mgao. HAPANA.

Tukubaliane kabisa kuwa wizi na kukosa uzalendo ndio chanzo cha matatizo ya umeme. Vyanzo vya maji vina uwezo mkubwa wa kukabiliana na upungufu wa umeme kwa sehemu kubwa, na vyanzo vingine vinaweza kuwa kama nyongeza. Inaaminika kuwa karibu 10% ya vyanzo vya maji ndio imetumika. Kumbe ukame sio tatizo. Na wala nyuklia kwa wakati huu sio muafaka. Let's heavilly invest in Hydro Power instead of the expensive IPP's. Let's fight corruption in the energy sector, here gas, petroleum, coal and hydro inclusive.
 
I was a human being before reading this sentence but I must say this is absolutely ridiculous. What if I cannot afford solar panel into my house therefore shall I say that my government failed to provide me with a reliable electricity?? Further, for 50 years since independence what have you guys been doing instead of realying on small hydro electrical power dam in Mtera. You have abandoned the plan of construction of a dam in Rufiji which would have been a much reliable source.

I think the entire Tanesco company need to be dismantled

Hebu Acha kumlaumu Eng. yeye amekupa chaguo la solar kutusaidia. Ki uhalisia huwez kuwalaumu Tanesco,wa kulaumiwa na CCM yenu mnyoipa kura miaka yote.
Sio kama nawatetea Tanesco hapana bt serikali ndio inastahili kubeba lawama kwa kuleta siasa kwenye mambo ya kitaalamu. Matokeo yake ni wizi na ufisadi.
 
Unaweza kuzalisha big scale power generation kwa kutumia njia mbili kwa kutumia solar

Moja ni kwa kutumia panels hizo na kuzalisha umeme direct Kama unavyozalishwa majumbani. Hii si cost effective mara nyingi ukilinganisha na eneo litalohitajika na performance ya solar panels zenyewe, na haipendelewi kutumika kwenye uzalishaji mkubwa

Njia ya pili ni solar thermal power generation, ambapo nguvu za jua zinakusanywa kufanya maji kuwa steam ambayo huzungusha mashine na kuzalisha umeme. Mara nyingi hii ndio njia inayotumika kwenye uzalishaji mkubwa.
Mwl. Sikujua kua wakati unatufundusha kiswahili ulikua unasoma Uinjinia kisirisi.lol
Leo tumepata darasa murua
Big up all
 
I think Eng Nsiande na yeye anatoa opinion kama mtanzania sio decision maker. Kama ni mapendekezo mesema kuna mmipango mingi tatizo ni haifanywi kazi .Watu wanafanya kazi kwa style ya zima moto.

Tuna haki ya kuwa na hasira na TANESCO lakini tusifanye hizi hasira ziwe personal. Binafsi kuna baadhi ya malezo ya engineer nimeyaelewa kuliko zile press release zao za kireja reja.

Hope kama anaweza atafkiishia kwa hao wahusika hisia na maoni yeetu kwa wahusika wa TANESCO.

Labda mimi nimuulize Nsinde kwa maoni yake

  • Kwa mipango iliyopo where will TANESCO + other sources be in five years.? Kiutendaji, kifedha na kuzalishaji wa umeme kulingana na mahitaji
  • Watanzania wafaanye nini kuisadia TANESCO ili iwe katika position inayotaka iwepo ?
  • Serikali inatakiwa ifanye nini.
  • Bunge lifanye nini? Je ile sheria ya kuigawa TANESCO ina manufaa na hasara gani ?
 
Hii ni mojawapo ya mada ambazo wanasiasa wanatakiwa kusoma; maana wanataaluma wetu wengi wamekuwa wakisoma mambo ya wanasiasa hadi wanakatisha tamaa.. shukrani kwa kutufungua macho zaidi na zaidi.
 
Shukrani sana kwa wachangajiaji na maengineer wote.najifunza mengi sana hapa. Mpaka imebidi niandike kitu ili kesho umeme ukirudi niweze soma vizuri kwenye PC kwa undani zaidi na kuelewa..
 
Unatujibu kitaalam zaidi, kiasi hata Badra tunadhani kama angetuyeyusha tu.

Tunaelewa kwa jiji kama la dar es salaam yapo maeneo maalum ambayo ni kwa ajili ya viwanda, mashirika, maofisi na yapo mengine ambayo ni kwa ajili ya makazi, ingawa yanaweza kuingiliana but ni kwa kiasi kidogo.

Huu mgao unazingatia hili jambo? Yaani muda gani, umeme uwepo mahali gani.
 
hii ni thread muhimu sana. For sure baadhi wa majamaa watakuwa wanaquote yaliyoandikwa hapa 'mjengoni' kesho!
 
Hii ni mojawapo ya mada ambazo wanasiasa wanatakiwa kusoma; maana wanataaluma wetu wengi wamekuwa wakisoma mambo ya wanasiasa hadi wanakatisha tamaa.. shukrani kwa kutufungua macho zaidi na zaidi.

heshima kwako mkuu wangu mwanakijiji, naomba niulize swali moja inapokuja suala la utaalamu na si-hasa za Tanzania.....hivi jamani watu mnaelewa hasa jinsi wanasiasa uchwara wa ccm wanavyowachukulia wasomi("walioelemika") ndani ya serikali ya hiyo ccm?? Kama wewe ni msomi "uliyeelimika" ndani ya serikali hii basi wewe si kitu bali kimbelembele, adui mkubwa na kakijana kenye uchu wa kutaka sifa na madaraka kutaka kuchukua nafasi (sema cheo) ya "bana kubwa". Wasomi wanaopendwa na hawa wanasi-hasa uchwara ni wale "waliosoma" (wenye mavyeti mengi ya PHDs, masters nk) na siyo walioelimika kwa kiwango cha PHDs Masters nk. Unatakiwa uwe bwana "ndiyo mzee" ndo utakubalika...wenyewe wana misemo yao uchwara kuhalalisha u-kihiyo wao, mfano eti, "mkubwa hakosei"!!!!!!!!

baada ya hicho kibwagizo naomba mkuu wangu mwanakijiji nitabiri kitu....unless some drastiic measures are taken to rescue TANESCO, the Enterprise, just like many other Tanzania State Owned Enterprises (SOEs), is going to rest in peace soon.....and do you know why??? teh!! i know you know it but i will reiterate........

(samahanini nitamkoti Nkya kwa lugha aliyotumia japo siipendi sana lugha hii kwani imechangia sana kutufanya wadanganyika wengi kuwa wajinga zaidi kwa kufifisha uwezo wetu wa kufikiri, kuelewa na kuhoji)

Estomih J Nkya in his handbook on Public - Private Sector Relationship in Economic Development says it all, that........

one: SOEs (Tanzanian in particular or ccm's - if you would like to be more presice) are marred with performance and efficiency constraints. The constraints include the Kornai's "soft budget constraints" in which the public enterprises are assured of a bail-out if their financial situation deteriorates; failure is more likely to bring a fund infusion by the government than is success. According to Raiser (1996 cited in Bangura, 2000:17) the Kornai's soft budget constraints entails unlimited access to subsidies and grants, soft credit systems and preferential treatment in tax rates. It reduces the incentive to minimize costs.

Two: SOEs are often used by governements to pursue non commercial objectives which are inconsistent with efficient and financially viable performance(Adam, Cavendish and Mistry, 1992 cited in Nkya, 1995). These objectives include employment maximization, non commercial price setting aimed at inter-sectoral cross subsidization (keeping prices low for other sectors), equity (distributional-------umeme kila makao makuu ya wilaya hata kama kuna watumiaji 10tu) and political patronage(position in SOEs offered to political supporters.........ukitaka mambo yakunyokee njoo ccm...hata kama wewe ni kilaza mradi vaa shati la kijani unalambishwa u-CEO.) In most cases the the objectives are multiple and contradictory (such as surplus creation against equity or balancing regional development) and the situation is made worse by bureaucratic meddling by government officers (si-hasa za ccm kwenye mambo ya utaalamu ndani ya mashirika ya uma ndo zimetumaliza, kinachotakiwa na ccm si uwezo ki-utaalamu bali uwezo wa kupiga perepende mingi kama anavyofanya ngeleja sasa) and perverse regulatory prices(World Bank, 1983)

Sasa wazee wangu njia pekee hapa ni moja tu....ni ile aliyopendekeza mwanamuziki nguli Bob Marley nayo ni Total Destruction...Ondoa system yote "zee" ya ccm weka system ingine "kijana" of whatever other party although CHADEMA saves best at the time
 
Hapa cha msingi ndugu engineer ni ku explore other avenues kama wanavyoshauri wana jf tuna rufiji, kagera, rusaunga, malagarasi nk Hii mito yote kama mnataka kuendelea ku dwell kwenye hydro power jenga turbines huko muweze kupata umeme wa kutosha.

Issue ya kuona mgao ni solution kwa umeme ni aibu kwa taifa, hamuoni soni kwa wageni wanaotembelea nchi hii kutoka na majibu ya kutuona wajinga kwa kukalia vyanzo lukuki vinavyoweza kuzalisha umeme huku tukitoa visingizio mbalimbali?!

Nchi gani mnayotembelea namaanisha study tours mnazofanya kwa kutumia pesa ya shirika, mmekuta haina umeme kama ya kwetu? kwa nini msijifunze huko wanafanyaje kufanikisha kuwa na umeme wa kutosha?
 
  • Kwa mipango iliyopo where will TANESCO + other sources be in five years.? Kiutendaji, kifedha na kuzalishaji wa umeme kulingana na mahitaji
  • Watanzania wafaanye nini kuisadia TANESCO ili iwe katika position inayotaka iwepo ?
  • Serikali inatakiwa ifanye nini.
  • Bunge lifanye nini? Je ile sheria ya kuigawa TANESCO ina manufaa na hasara gani ?

Nitakubaliana na Mhandisi Nsiande kuwa kwenye makaratasi TANESCO inapaa na tatizo la umeme halipo kabisa, lakini kwenye utekelezaji au kuchukua hizo hatua za kutufikisha huko kwenye neema ndio kwenye tatizo.

Ukipitia Power System Master Plan ya serikali ya end of 2008, kuna miradi kadhaa imependekezwa kuchukuliwa baada ya kufanyiwa analysis kuhusu mazingira na masuala ya kijamii, lakini serikali inaleta siasa na haifanyi uwekezaji kwenye uzalishaji wala usambazaji.

Bei wanazotoza Tanesco kwa nishati pia ni ndogo ukilinganisha na gharama wanazoingia japokuwa ukibalance na kuwa wanaingia gharama kubwa kwa sababu ya mikataba ya kizembe na kutowekeza kwenye njia endelevu za uzalishaji umeme, ni ngumu kukubali mwananchi wa kawaida kulipia gharama zaidi ili kuongeza mapato ya TANESCO.


Binafsi nafikiri TANESCO inatakiwa kuacha kufikiri ndani ya box tu wakati wote. Kuna option ya umeme wa nguvu za upepo (tuliambiwa kuna waKorea watakuja kuwekeza sijui wameishia wapi). Kama walivyofanya Morocco tunaweza kupata ushirikiano mzuri na nchi za zilizoendelea kwa vile wao wanachotafuta ni carbon credits hivyo kutupa usaidizi wa kitaalamu na mkopo.

Pia wanaweza kuwa pioneers wa some solutions wasisubiri hadi solutions ziwe zimetumiwa nchi nyengine ndo na sisi tuige.

Ingelikuwa ni juu yangu ningewalazimisha clients wote wenye buildings with over a certain total floor area kuweka solar panels kwa kiwango fulani. Na umeme watakaozalisha kuingiza kwenye grid ya taifa. And maybe if I were bold enough ningewalazimisha kuingiza umeme huo wakati wa-peak ili kuondokana na ku deal na peak demand.
(ningewalazimisha kwa sababu hawa ni watumiaji wakubwa wa umeme na sasa umeme unachezewa sana kwa vile gharama yake ni ndogo)
 
...................................
failure is more likely to bring a fund infusion by the government than is success. According to Raiser (1996 cited in Bangura, 2000:17) the Kornai's soft budget constraints entails unlimited access to subsidies and grants, soft credit systems and preferential treatment in tax rates. It reduces the incentive to minimize costs. .......................................................

Mkuuu nakubaliana na wwa . sasa tunajiuliza hizi Pesa wanazolipwa IPTL kama wangeweeza TANESCO bofore.

Yaani wati hata mtoto wa darasa la ne anajua methali ya KINGA ni bora kuliko TIBA inawezekana Serikali kwa suala la TANESCO imeamua vice.
versa kuwa TIBA ni bora kulko kinga.

Yaani hivi sasa ni hasara mara mbili waati Tanesco iko hoi Mapesa yote yanaishia kwa hao tunaowaita wawekezaji kwenye sekta ya NISHATI.
 
Mtasema yoooooooooooooooote! Lakini ukweli ni huu:
Tatizo la umeme nchi hii ni la kujitengenezea. Linatengenezwa na wanasiasa na wanaitumbukiza Tanesco kwenye mchezo huu na wao wanaendesha game.
Kwa nini? Pesaaaaaaaaaa. ile asilimia ngapi sijui ndio tatizo kubwa.
Asante mainjinia. Mmekuja na maelezo mazuri ya kuvutia. Kwa kweli mmejitahidi sana kukoga akili zetu. Jambo moja tu hamkulisema na hili ndilo ukweli, tatizo la umeme nchini ni la kujitengenezea kwa sababu maalum.
Kwa nini hamkulijumuisha kwenye moja ya matatizo yenu ya umeme Tanesco enyii mainjinia? God forbid.
Nimewahi kujiuliza saaaaana kwamba kabla ya chaguzi zote huwa hatuna shida ya umeme hata kidogo, na mambo uenda swafiiiiii. Lakini kila tukimaliza chaguzi tu!, hapo ndipo tuanzapo kusikia shida za umeme. Mara ukame mara gesi sijui imekuwaje, mara mashine za IPTL sijui zimekosa mafuta. Mara umeme umekosea njia ukaingia njia ya Pugu road badala ya Mandela, Yaani shida baada ya shida.
Na kwa hilo mainjinia Tanesco mbona hawajawahi kutuambia kuwa shida ya kujitengenezea kuwa ni moja ya sababu? Leo tunaambiwa tatizo litakwisha 2013. Alafu bila shaka litaanza 2016 na kisha liishe 2018 na lijirudie 2021!. Ili mradi pesa ipatikane kwa wanasiasa. Siku watu wakigundua janja yenu mmekwisha.
Nawashukuruni na endeleeni kujadili. Hamtapata jibu nje ya jibu.
Kaa la moto.
 
Back
Top Bottom