Eng.Nsiande na Majibu ya Tatizo la Nishati ya Umeme - Must Read

Engineeer
Nadhani unakosea ukisema mgao hauimpact sana viwanda.. Mgao unaimpact sana viwanda kunaw watu wanakosa ujira na kazi sabbau ya umeme. Ile kasumbua kutoa umeme viwandani asubuhi na kuzuima usiku ni siasa. Kuna vinwada vingi operation zake ni 24 hrs. Kuna jamaa uswazi niko nao hawaendi kwenye ujira wao wa siku zao wananiambia sababu ya umeme.

Alafu niliwai kusikia maleezo tarrif za umeme wa viwandani ni nafuu zaidi kuliko umeme wa majumbani. Je hili ni kweli. ?

Still haimake sense kuwa ati Tanzania inategemea viwanda kisha ukaambiwa Japani inategemea domestic, na ndo maana Tanzania viwanda havikatiwi umeme!

Kwanza dhana nzima haipo sahihi, ukiangalia energy use profile ya Tanzania utaona kuwa peak demand is from 1800hrs-2300hrs (From Tanesco report to EWURA). Na hiyo profile haibadiliki ama siku za kazi ama weekend. Ikimaanisha kuwa wateja wa domestic ndio wanaosababisha peak wanapowasha taa wakati wa usiku (because there is no peak in early morning before work). Pia hakuna peak wakati wa mchana ikimaanisha kuwa viwanda sio vyenye demand kubwa.

Labda tungedhani dhana hiyo inatokana na mapato, lakini bado makusanyo ya revenue kutoka kwa D1 na T1 ni makubwa

* Wateja wa viwandani wanatozwa bei ndogo kwa consumption-kWh ya umeme kuliko wateja wa majumbani, lakini wao wanatozwa na bei ya demand-kVA pia
 
Kwako Nsiande...

Kuna ukweli wowote kuwa wakati wa Mkapa for 10 yrs Tanesco iliwekwa kuwa ni kampuni inayohitaji kubinafsishwa hence serikali haikuwa na mkakati wowote wa kufanya big investment for power generation?
 
Still haimake sense kuwa ati Tanzania inategemea viwanda kisha ukaambiwa Japani inategemea domestic, na ndo maana Tanzania viwanda havikatiwi umeme!

Kwanza dhana nzima haipo sahihi, ukiangalia energy use profile ya Tanzania utaona kuwa peak demand is from 1800hrs-2300hrs (From Tanesco report to EWURA). Na hiyo profile haibadiliki ama siku za kazi ama weekend. Ikimaanisha kuwa wateja wa domestic ndio wanaosababisha peak wanapowasha taa wakati wa usiku (because there is no peak in early morning before work). Pia hakuna peak wakati wa mchana ikimaanisha kuwa viwanda sio vyenye demand kubwa.

Labda tungedhani dhana hiyo inatokana na mapato, lakini bado makusanyo ya revenue kutoka kwa D1 na T1 ni makubwa

* Wateja wa viwandani wanatozwa bei ndogo kwa consumption-kWh ya umeme kuliko wateja wa majumbani, lakini wao wanatozwa na bei ya demand-kVA pia
Correction sijasema wanategemea domestic bali revenue yao ni kubwa, to prove that google 'load shedding in Japan' utaona jinsi viwanda vilivyoathirika lakini hii ni kutokana na ile natural disaster so viwanda vimeelewa na kushusha loadNchi nyingi na si Tanzania peak ni saa moja kamili usiku mpaka atleast saa 3 ukiwa RSA utaona kwenye TV wakiwarn kuwa sasa hivi ni peak punguzeni matumizi zimeni taa etc etc ili mzigo usiwe mkubwa, si tu kuwa kuna upungufu wa umeme ila technically kuoperate kwenye peak si ideal maana upotevu unakuwa mwingi na si TZ ni nchi zote tu.

Hapo kwenye nyota naomba ufafanuzi maana si sahihi ulichokiandika
 
Engineeer Nadhani unakosea ukisema mgao hauimpact sana viwanda.. Mgao unaimpact sana viwanda kunaw watu wanakosa ujira na kazi sabbau ya umeme. Ile kasumbua kutoa umeme viwandani asubuhi na kuzuima usiku ni siasa. Kuna vinwada vingi operation zake ni 24 hrs. Kuna jamaa uswazi niko nao hawaendi kwenye ujira wao wa siku zao wananiambia sababu ya umeme.Alafu niliwai kusikia maleezo tarrif za umeme wa viwandani ni nafuu zaidi kuliko umeme wa majumbani. Je hili ni kweli. ?
Mtazamaji hauathiri sana viwanda,kwamfano kama uko line 2 ya Wazo nadhani hujakumbwa na mgao..unaathiri ila si sana maana revenue zinawategemea hao 70% inatokana na large power users sema consumptionm yao ni kubwa
 
Kwako Nsiande...Kuna ukweli wowote kuwa wakati wa Mkapa for 10 yrs Tanesco iliwekwa kuwa ni kampuni inayohitaji kubinafsishwa hence serikali haikuwa na mkakati wowote wa kufanya big investment for power generation?
Mikakati ndugu yangu ipo imejaa vitabu hata mia...ImPLEMENTATiON tu! Ndio tatizo...nitawashangaa wabunge wakipitisha budget leo..but again I won't be much suprised as majority ....
 
Hapo kwenye nyota naomba ufafanuzi maana si sahihi ulichokiandika

Wateja wa General Use wanatozwa 125 Tshs per kWh na Wateja wa T2 wanatozwa 85 Tsh per kWh wakati wale wa T3 ni 79 Tsh per kWh

Wateja wa General Use hawatozozwi demand charges wakati wa T2 wanatozwa 9,347 Tsh per kVA na wa T3 wanatozwa 8,669 Tsh per kVA

Bill ya mteja ni majumuisho ya cost of maximum demand kwa mwezi (or 75% ya maximum ya miezi mitatu iliyopita?) na total consumption-kWh




* kisha nasikia wafanyakazi wa Tanesco mna bei zenu maalum za umeme sio kama za watu wa nje?
 
Mtazamaji hauathiri sana viwanda,kwamfano kama uko line 2 ya Wazo nadhani hujakumbwa na mgao..unaathiri ila si sana maana revenue zinawategemea hao 70% inatokana na large power users sema consumptionm yao ni kubwa

Tanesco itakuwa na matatizo sana, manake katika reports and data zinazowasilisha kwa consultant agencies and Ewura zinasema kuwa revenue ya Tanesco 43% ni D1& T1 (hawa ni domestic na biashara ndogo ndogo) wakati T2& T3 wanachangia 52% ya revenue na Zanzibar ni 5%. Sasa kama kumbe hao large consumers wanatumia 70% ndio maana hata solutions wanazopewa na hizo agency haziwezi kuwasaidia.
 
Kimsingi solar ni competitor..ni kama uende TBL wakushauri unywe serengeti my dear Mtazamaji..
Forget about competition and look at it as an opportunity. Ni kwamba Tanesco wangekuwa proactive wangeweza kuinvest ktk eneo la solar energy. Market ni kubwa tu finacing ndio shida hapo Tanesco wengeweza ku-capitalize easily. Lakini shida ni kwamba kama Tanesco hawana contingency plans its inconceivable kwamba wanaweza kufikiria hizi opportunity zingine. Tatizo kubwa kupita zote ni JK administration haiko serious hata kidogo ktk swala la umeme. Wangekuwa serious hakuna Waziri au Raisi angesimama mbele ya watu na kusema kina cha maji kimeshuka..umeme ni security good lakini unavyokuwa treated na hii administration ya JK ni kama vile mkate tu...you hear this Minister for energy repeating these words tuko ktk mchakato..., upembuzi yakinifu umekamilika...sijui megawati...SHAME
 
Nimefuatilia mjadala huu nimeona niweke mawazo yangu.

Wizara ya Nishati kwa kupitia TANESCO imekuwa ikianda Mpango Kabambe wa Sekta ya Nishati (Umeme). Mpango wa kwanza uliandaliwa mwaka 1985. Utekelezaji wake ulisuasua hadi ukapelekea kujengwa kwa Pangani falls kabla ya Kihansi ingawa mpango uliaininsha Kihansi kwanza, Hii ilitokana na gharama za mradi wa Pangani kuwa ndogo, IPTL ikajitokeza BILA KUWEPO KWENYE MPANGO HUU na ikapelekea kuchelewa kutekelezwa kwa mradi wa Songosongo.

Sekta ya Umeme ikabadilika na ikabidi kuandaa Mpango mwingine mwaka 1998. Mpango huu ulianisha kujengwa kwa Mradi wa Ruhudji ulioko Njombe uanze uzalishaji 2006. Mpaka leo hii mradi huu haujajengwa. Badala yake tumeshuhudia RICHMOND, DOWANS na hatimaye SYMBION ambayo haikuwepo kwenye Mpango huo. Hatimaye mwaka 2007 ukaandaliwa Mpango mwingine na ukarekebishwa (Update) 2009 ambao ndio upo sasa hivi. Tusubiri kuona utekelezaji wake.

Ninachokisema hapa ni kwamba MIPANGO imekuwepo tena mizuri lakini utekelezaji wake umeingiliwa na SIASA (ULAFI) badala ya UTALAAMU
 
dush sorry... I was away for so long such that someone asked me to log in...

Apart from what is posted on the web, reality sucks..reality is...we as a country has gas shortages so even if we get 300mw now we won't be able to run the gas plants...

Mtera is @ 691m.a.s so literally it has to be shut @ 690m.a.s which will be achieved in august...unfortunately it didn't rain there!!

Grid control center is currently asking to shed further 30mw ( that explains last night outage...)

kimsingi sina maelezo zaidi ya yaliyotolewa, ila for a state owned utility kazi ya generation bado ni mpango wa serikali.....

pole mzalendo na watanzania wenzangu...i didn't think that i would advice this...but anyways...pls if u can go solar..it will be severe in november kama mvua za vuli ( ambazo hydrologically si. Nyingi zikiacha kunyesha mtera )

i can advice on solar option based on ur load..yani umeme unaotumia majumbani
Mhandisi hapo kwenye nyekundu ndio key issue siku zote mi nasema long run investment kwenye umeme ndio infinite solution mtaendelea kuilaumu tanesco weee wakati our government inapenda sana hizi emergency power backup mimi mpaka huwa sina imani kabisa na nchi yangu lipakuja suala la ukame maana huwa na sense kuwa kuna watu wanafurahi utajiri unaongezeka.

Inatuuma sana hasa sisi wengine ambao umeme its our profession cha msingi wakuu tujaribu kwenye hizi alternative energy source kama solar, biogas nk tunaweza wapa hata ushauri wakitaalamu wa jinsi ya kutumia hio nishati mbadala ila tukiendelea kulalamika na hii seriakli ni sikio la kufa haaaaaaaaaaa
 
Thank God at last watu wanakumbuka wataalamu!

Sijui laana hii imetoka wapi, kusomesha wataalamu na kutowatumia kabisa kwa sababu ya ajenda za siri. Niliwahi kumtania mhandisi mmoja kuwa kwenye sekta ya umeme hatukutakiwa kuwa na tatizo.Kwani vipanga wote wa ilboru, mzumbe, kibaha na tabora boys wengi wao wanaishia kwenye fani hii! Hali ni kinyume na kwenye fani ambazo sisi vilaza huwa tunakimbilia kama ujenzi, migodi, n.k!! you can imagine

I personally nimefanya feasibility study, EIA,na infrustructural designs za miradi mingi ya umeme. Miradi mingi imeishia kufa na kutokukubaliwa kutokana na aidha urasimu wa TANESCO, au miundombinu mibovu.

Kwa mfano mradi wa kampuni ya TANCOAL (NDC ina asilimia 30) ambao uko Ngaka songea, mwekezaji na fedha vipo, mgodi (coal mine) umeishaanza, tatizo hakuna connection kutoka kwenye power plant (planned) kwenda kwenye gridi ya taifa. wana mpango wa kuzalisha umeme 400mw, INAHITAJIKA 400KV high voltage transmssion kutoka Ngaka mpaka kwenye gridi ya TAIFA. Ktuoka kwenye power plany mpaka songea mjini ni kama km 90 hivi ambapo kama serikali wangeamua kuchukua hii portion na kutomwachia mwekezaji ingekuwa bora. Kibaya ni kuwa mwekezaji ana uwezo mpaka wa kujenga hiyo line kutoka Ngaka mpaka songea mjini, lakini hata akifikisha hakuna gridi ya taifa tena ya 400KV!..Narudia fedha ipo...

If I were TANESCO ningefuta yote mengine na ku-encourage mradi huu, MRADI HUU UNEGEWEZA KUSOMBA UMEME TARAJIWA WA LIGANGA, MCHUCHUMA n.k!!!

Kama nilivyosema fedha ipo,mwekezaji yupo, mgodi umeishaanza, kwa sababu ya plan mbaya ya taifa, huyu mwekezaji anaanza kuuza mkaa kwenye viwanda vya cement vya ndani na kuuza malawi!!! mpo hapo??

Hivi umeme wa 400MW si ngau ungemaliza tatizo la kuomba mvua inyeshe!

 
thank god at last watu wanakumbuka wataalamu!

Sijui laana hii imetoka wapi, kusomesha wataalamu na kutowatumia kabisa kwa sababu ya ajenda za siri. Niliwahi kumtania mhandisi mmoja kuwa kwenye sekta ya umeme hatukutakiwa kuwa na tatizo.kwani vipanga wote wa ilboru, mzumbe, kibaha na tabora boys wengi wao wanaishia kwenye fani hii! Hali ni kinyume na kwenye fani ambazo sisi vilaza huwa tunakimbilia kama ujenzi, migodi, n.k!! You can imagine

i personally nimefanya feasibility study, eia,na infrustructural designs za miradi mingi ya umeme. Miradi mingi imeishia kufa na kutokukubaliwa kutokana na aidha urasimu wa tanesco, au miundombinu mibovu.


kwa mfano mradi wa kampuni ya tancoal (ndc ina asilimia 30) ambao uko ngaka songea, mwekezaji na fedha vipo, mgodi (coal mine) umeishaanza, tatizo hakuna connection kutoka kwenye power plant (planned) kwenda kwenye gridi ya taifa. Wana mpango wa kuzalisha umeme 400mw, inahitajika 400kv high voltage transmssion kutoka ngaka mpaka kwenye gridi ya taifa. Ktuoka kwenye power plany mpaka songea mjini ni kama km 90 hivi ambapo kama serikali wangeamua kuchukua hii portion na kutomwachia mwekezaji ingekuwa bora. Kibaya ni kuwa mwekezaji ana uwezo mpaka wa kujenga hiyo line kutoka ngaka mpaka songea mjini, lakini hata akifikisha hakuna gridi ya taifa tena ya 400kv!..narudia fedha ipo...

If i were tanesco ningefuta yote mengine na ku-encourage mradi huu, mradi huu unegeweza kusomba umeme tarajiwa wa liganga, mchuchuma n.k!!!

Kama nilivyosema fedha ipo,mwekezaji yupo, mgodi umeishaanza, kwa sababu ya plan mbaya ya taifa, huyu mwekezaji anaanza kuuza mkaa kwenye viwanda vya cement vya ndani na kuuza malawi!!! Mpo hapo??

Hivi umeme wa 400mw si ngau ungemaliza tatizo la kuomba mvua inyeshe!

mhandisi inaumiza sana nasikitika sana hii nchi inavyotuignore tunasota sana foe/coet, dit na huko mist lakini wala cha ajabu tu wanatupiga benchi(unemployed) hasikilizi ushauri wakitaalamu .wito kwa wahandisi hasa umeme nafikiri tuweza kujaribu kuinvestment kwenye vi miradi vidogo vya power generation ili tuokoe hii nchi najua technical we can manage kufanya haya mambo. Tungekuwa na serikali sikivu zile project za umeme zingefanyiwa kazi na mgao ungekuwa history
 
Moja ya suluhisho la tatizo la umeme Tanzania ni kwa Tanesco kuganywa katika sehemu tatu; Uzalishaji, Usafirishaji na Ugawaji. Kila moja ya hivi vipengele ni shughuli inayojitosheleza ilivyo. Napataga shida kuyumkini jinsi vikao vya utawala wa ngazi ya juu Tanesco vinakuwaje pale unapokuwa na watu kutoka sehemu hizi wanapresent ripoti zao;

Hebu fikiri, kwa mfano; Mtu wa usafirishaji anaelezea hitajio la Dollar Million kadhaa kununua speya ili kurudisha umeme Zanzibar, huku mtu wa Ugawaji anajaribu kuripoti tatizo la virus kwenye server za Luku, na yule wa Uzalishaji naye analia kuwa Nyumba ya Mungu wanahitaji gari jipya, Ubungo generator limepasua gasket na kwa ujumla umeme hautoshi Tanzania! Utaweza endesha kampuni kama hilo kwa ufanisi kweli, au utabakia kuwa mtu wa ku-react.

Nakumbuka wakati fulani kulikuwa na kampuni ya Posta na Simu, ambayo ilikuwa ni Postal Bank + Posta + TTCL + TCRA. Hivi ndivo ilivyo Tanesco leo.
 
mhandisi inaumiza sana nasikitika sana hii nchi inavyotuignore tunasota sana foe/coet, dit na huko mist lakini wala cha ajabu tu wanatupiga benchi(unemployed) hasikilizi ushauri wakitaalamu .wito kwa wahandisi hasa umeme nafikiri tuweza kujaribu kuinvestment kwenye vi miradi vidogo vya power generation ili tuokoe hii nchi najua technical we can manage kufanya haya mambo. Tungekuwa na serikali sikivu zile project za umeme zingefanyiwa kazi na mgao ungekuwa history

Mkuu hivyo vimradi vidogo vinahitaji capital mbazo bado ni tatizo nchini kwetu.

Trust me, nchi inavyoendeshwa hii, uzalendo umeishwashinda wengi, watu wana 'zipiga' kama hawana kili, low standard barabara ni kitu cha kawaida, who cares anyway? after 5 years zitatafutwa fedha za maintenance.

wanasiasa na CCM yao wameinajisi nchi hii
 
Japan kuna mgao wa umeme after the natural disaster and it will be there for 2 years, they urged other companies to sell the solar and other renewable energy to its citizens, they can't fix the natural calamities without loadshedding for 2yrs and they were bold enough to say they won't get rentals and themal to do it bcoz its just so expensive.

So, local companies do the solar thing there, actually their electricity sector had been regulated since the 80'sIn other parts Solar is operated for distribution by other companies and not the core utility and as for here solar can be used in generation. There are companies already doing the solar business and common mwananchi can get it from them, not from the state owned utility, u may give reference on state owned utilities that run parralel(sp) with solar for distribution

...u will find solar is there for generation only and thts what the utility is doing right now. So yes though inashangaza to say it but literally tht is a competitor and its done already by other companies locally and this helps to build the local capacity but it won't do for utility now to go solar for this loadshedding of 6months alone

Am I getting you well engn?

Kuna siku nilikuwa nimekaa mbele ya TV yangu natazama mahojiano na mainjinia fulani toka TANESCO (sidhani kama ulikuwepo), na mmoja wao akasema kwa kujiamini na kwa bold language kuwa umeme wa solar hauwezi uakatumika kwa scale kubwa kwa sababu solar zinazalisha umeme kidogo sana na unapoweka panels nyingi unaongeza resistance, hivyo haisaidii. Nilibaki nimeduwaa nikidhani ndoto zangu kuwa Tanzania na nchi nyingine huku tropical tutakuja kukombolewa kwa umeme wa jua zimakwisha.

Say it again engn... Is it possible to use solar energy for big scale power generation?
 
NAFURAHIA SANA MICHANGO YA KILA MMOJA WENU KWENYE HII THREAD JAMANI!

Sikujua kama tuna wataalam wote hawa wanaoweza kukidhi kiu yetu ya kutaka kujua undani wa hili tatizo sugu la umeme!

Nadhani tumejifunza kwamba kama tutawatambua wataalam wetu humu JF na kuwalenga moja kwa moja kwa heshima kama ilivyofanyika kwenye thread hii basi tutafaidika sana!

Hatutafaidi kama tutarusha "makombora" bila mwelekeo, ndio mwanzo wa kukaribisha yale mazungumzo ya utani befitting jukwaa la Chit Chat.Hili halijajitokeza kwenye hii mada huenda ni kwa vile hakuna asiyeguswa na hili tatizo.

Hongereni nyote wasomaji na wachangiaji... tuendeleeni tafadhali!
 
Samahani ndugu zangu naomba kuuliza swali hili kwani linaniumiza kichwa sana,kwa matumizi madogo ya nyumbani like tv,radio na taa kama 4 hivi kipi ni rahisi kununua generator then ukatumia au kuunganisha solar?naomba majibu ya kitaalam interms of cost and installation kwani nahijaji kimojawapo.thanks
 
Back
Top Bottom